- Thread starter
- #141
(Luke 20 ) ndipo Yesu aliwajibu mafarisayo kuwa mtu akifa anakuwa kama tu malaika. Hawaoi Wala Kuolewa.Naomba uelezee sehemu unasema hizi ni roho za wafu,Yesu alisema roho haina nyama wala mifupa,sasa mbona roho hizi za wafu usemazo hapa inaonekana wazi zina nyama na mifupa?
Alikuwa akiwajibu swali mafarisayo kuwa mtu akifa ana mke na hajazaa mtoto, mtu mwingine akimwoa mke yule, siku ya ufufuo, mke atakuwa wa nani?
Mbinguni watu Walio huko ni Roho, Malaika hawaoi au Kuolewa huko, Mungu ndiye mfalme wetu, sisi ni Wana na Malaika ni watumishi wake.
KUZIMU ni tofauti na Mbinguni, kuzimu wanaingiliana kinyume na maumbile, mchawi mme huzini na wenzie kinyume, mama kuzini na mtoto ni kawaida kabisa, ndomana wanataka TABIA za kuzimu zihamie Duniani.
Wakati huo huo Mungu anataka mfumo wa Mbinguni utumike duniani hivyo vita IPO inaendelea kati ya falme hizi mbili.
Mtu ni Roho, anayo NAFSI na anaishi ndani ya mwili.
Mwili haiwezi kusikia maumivu yoyote Roho ikiondoka ndani ya MWILI mtu akifa.
Maumivu mtu anayosikia yapo katika NAFSI.
Mtu wa ndani, anao mwili yaani Roho ana viungo vyote, mikono, miguu, macho nk nk na ni HALISI kabisa.
Kila kitu ukionacho kinaanzia Ulimwengu wa Roho kabla ya kuja katika mwili.
Ukisomwa (Luke 16:19-31).kisa Cha tajiri na maskini, tajiri alikuwa akiteswa na kufungua moto na akisikia kiu na kuomba aletewe maji,
Nami nikuulize, iweje mtu awe katika mwili wa Roho aombe maji?
Na akinywa maji yayaingia katika tumbo lipi wakati Yu katika mwili wa Roho?
Mbinguni ipo Mito ,Kuna miti, maua, wanyama,maji mito, chakula kama duniani,tofauti tu viko katika mfumo wa kiroho.
Neno la Mungu ni chakula Cha Roho Kwa watakatifu na usipokila unakuwa dhaifu katika mwili wa Roho,unakuwa kimbaumbau, ukishambuliwa na mapepo, utaumia.
So katika Roho Kila kitu kinafanyika kama duniani lakini ni katika ukurasa wa Roho.
KUZIMU zipo silaha, vipi viwanda, hata watu nusu mtu nusu Pepo wanatengenezwa huko, yapo magari, ndege za kichawi na zaidi ya hapo.
Wapo masheikh hutengeneza majini Kwa msaada wa mapepo Kutoka kuzimu.
Mapepo yanakula chakula, Damu ndicho chakula Chao kikuu.
Hivyo, Kwa uchache ujue kuwa, Kila kilicho katika mwili kipo katika Roho.
Amen