INAENDELEA.......,.
IDARA YA WAKE KWA WAUME WALIOZINI KUPITIA LANGO LA NDOTO/ JINI MAHABA.
Mapepo Saba yalikuwa yakimgombania Mwinjilisti aliyekuwa amevaa Pete ya NDOA ambayo haikuteketea katika moto.
Kila Pepo lilidai huyu ni wangu, alikuwa alipitia mateso makali sana kwenye uume wake na korodani zilofanyiwa Kila aina ya mateso.
STORY BEHIND MWINJILISTI MWENYE PETE YA NDOA.
Mwinjilisti huyu alikuwa na NDOA iliyofungwa kihalali Kanisani, alikuwa mwaminifu katika NDOA yake na hakuwahi Kutoka nje ya NDOA Kwa UZINZI.
Siku moja Mwinjilisti alikuwa akitembea barabarani, ghafula macho yake yalitua Kwa mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa nguo za kumbana sana, na alikuwa na umbo lililovutia, na macho yake yalijikuta yakiendelea kumtizama mwanamke huyu Kwa tamaa, akajisemea moyoni mwanamke huyu ningempata,....
Akili ilimrudia na akakumbuka ana mke nyumbani na alipoiangalia Pete yake kidoleni akasema, sitomfuata mwanamke huyu kahaba na akarudi nyumbani.
Baada ya siku kadhaa kupita, akaanza kupata ndoto za kuzini na mtu asiyemjua ndotoni, aliichukia Hali hii, akamshirikisha Mchungaji wake, wakaomba na kukemea Hali Ile. Ilitulia baada ya siku chache, baadae ikaendelea tena, mwanamke aliendelea kumjia na kuzini naye. Pepo yule aliendelea kumwachia uchafu mtu yule Kila alipomjia.
CHANZO CHA NDOTO YA MWINJILISTI.
Siku Ile alipomwona mwanamke yule kahaba na kumtamani,
Kumbe mwanamke yule alikuwa ni kahaba na mchawi, ikumbukwe pia MAKAHABA wengi huenda Kwa Waganga kutafuta nyota ya kufuatwa na wanaume wengi Ili kuzini kupata pesa.
Mwanamke yule kahaba na mchawi, alikuwa na Roho ya Marmaid, Malkia wa kuzimu iliyokuwa ikimwongezea mvuto Ili kuvutia wanaume, kumbuka mwanamke yule hakugeuka na hata hakujua kuwa Mwinjilisti alimtamani.
Roho Ile iliyokuwa ndani ya kahaba, ilikwenda kuzimu Kwa Malkia mkuu wa Baharini, Pepo na kupeleka ombi la kuomba kuchumbiwa na Mwinjilisti ambaye alionekana kumtamani kahaba yule.
Malkia wa kuzimu alikubali ombi Hilo, akaagiza atafutwe ndugu wa Mwinjilisti ambaye ni mchawi Ili afanyike mwakilishi wa familia ya Mwinjilisti ambaye atapokea Mahari ya Jini mahaba yule wa kike.
Alipatikana mjomba wa mwinjilist ambaye alikuwa mchawi, na alipofika Kwa Marmaid mkuu, aliambiwa, Mwinjilisti amempenda Binti yangu, anataka kumwoa, mnatakiwa Kutoa Mahari Ili aoe kwenye familia yetu.
Mchawi yule, mjomba wa nwinjilist, alisema,Mahari itakuwa ni kupunguza maisha ya Mwinjilisti Ili afe akiwa na umri wa miaka 33 pekee.
Nilishangaa kusikia mtu anafungisgwa NDOA bila kushiriki wakati ana NDOA tayari!!!
Marmaid mkuu wa Baharini alipokea Mahari NDOA ikafungwa na ndoto za ngono ziliendelea kumtokea Mwinjilisti.
Siku moja Mwinjilisti aliota ndoto akifanya Tendo na mwanamke asomjua na alimwaga shahawa, alipoamka alishangaa na kusikitika.
Pepo yule wa kike wa mahaba, alichukua mbegu au shahawa za Mwinjilisti na kuzipeleka Kwa Malkia wa Baharini na kumwambia anaomba kuzaa mtoto na Mwinjilisti na alikubaliwa, mbegu za Mwinjilisti zikichukuliwa na kupelekwa kiwanda Cha watoto na zilirutubishwa ndani ya tumbo la Pepo mahaba na baada ya muda, akazaliwa mtoto wa kipepo na Pepo yule wa kike alifurahi sana.
Baadae Walizaliwa watoto wakiume na WA kike wa kipepo ambao hutumika kuja duniani wakiwa nusu mtu nusu Pepo ambao huja kufanya mission mbalimbali duniani za Shetani.
Pepo yule alikuwa na Rafiki SITA ambao pia aliwaalika kushare nae ndani na Mwinjilisti.
Ilipotimia miaka 33, sawasawa na sadaka Mahari ya NDOA, Mwinjilisti alifariki na kutupwa KUZIMU ya moto.
Yesu alisema, 85% ya watu wanaotupwa kuzimu ya moto Huwa hawajui dhambi iliyowapeleka kule.
AINA YA NDOA ZA KIPEPO KIROHO.
1.Malaika waasi WALIOZINI na wanawake binadamu kama ilivyoandikwa enzi za Nuhu.
2. Wachawi wanaozini na wanawake wasio na ulinzi wa Mungu.
3. Roho za watu WAFU zinazotangatanga duniani ambazo zilitolewa kabla ya muda wao wa kufa kufika uliopangwa na Mungu.
4. Mawazo ambayo hugeuka na kurudi kama ndoto.
Kundi hili la NDOA linahusisha.
-Wale wanaoangalia tamthilia zenye picha za hisia za ngono ndani yake.
Mapepo hutoka ndani ya picha hizo na kuwaingia watu hao na baadae wataanza kupata ndoto za mahaba na mapepo ambayo yalipita na kuwaingia baada ya kuangalia picha za ngono kupitia tamthilia.
-Wenye kutizama picha za ngono.
Mapepo hutoka ndani ya picha hizo na kuingia na kufunga nao NDOA, vifo vya kabla ya wakati hutokea zaidi Kwa watu waotao ndoto hizo.
- Wenye kujichua.
Hili nimeliongelea andiko lililopita.
NB: Ndoto ni HALISI.
Mungu hutuma taarifa Kwa watu waangaliao video chafu za ngono, wenye kujichua nk nk kupitia ndoto Ili kuwaarifu watubu lakini wengi hupuuzia au kutoelewa lugha ya picha ilitumika ndotoni.
Wengi huota ndoto wanatembea wako uchi, wengine huona mbwa wakiwafukuza au kulala nao nk nk.
KANUNI SAHIHI ZA KUVUNJA NDOA NA PEPO LA NGON0 NA JINI MAHABA.NK NK.
1. Nenda na Kiri dhambi na tukio Hilo Kwa mtumishi wa Mungu maana huwezi jiokoa pekeako sababu umeshakuwa mtumwa.
2. Mtumishi wa Mungu Afanye maombi ya Ukombozi.
3. Iandikwe barua ya talaka.
Hii ifanyike Kwa kuchukua sadaka ya mbegu Ili MAHARI ilitolewa Kwa niaba Yako na ndugu Yako mchawi aliyekuwakilisha katika NDOA ya kipepo, IRUDISHWE katika Ulimwengu wa kiroho wa kipepo na TALAKA itolewe kuvunja NDOA hiyo ya kipepo IFUTWE. Na sadaka uliyotoa itatiwa Muhuri.
AGALIZO: Epuka video za ngono, hata wanandoa wamekatazwa, tamthilia acheni kuangalia, acheni kujichua, okoka na Ujazwe Roho MTAKATIFU atakayekupa nguvu ya kuacha kutenda dhambi.
YESU AKUMBUSHA NENO LAKE KUHUSIANA NA DHAMBI NA HUKUMU YA NDOA YA NAPEPO NDOTONI AMBAO NI UZINZI.
(Mt 11:17).
Tuliwapigia filimbi, Wala hamkucheza, tuliomboleza, Wala hamkulia.
(Luke 13:3).
Nawaambia ,sivyo, lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.
(Kutoka 20:17).
Usiitamani nyumba ya Jirani Yako, usimtamani mke wa Jirani Yako.
(Ayoub 31:1).
Nilifanya AGANO na macho yangu, basi nawezaje kumwangalia msichana?
(Ayoub 31:9-11)
Kama moyo wangu ulishawishiwa Kwa mwanamke, nami nimeotea Jirani pa Jirani yangu,
Ndipo hapo mke wangu asage Kwa mwingine,
Na wengine wainame juu yake, kwani Hilo limekuwa kosa kuu, naam, lingekuwa ni UOVU wa kuadhibiwa na Waamuzi.
( Zaburi 81:12).
Nikawaacha wakaenenda Kwa ukaidi wa mioyo Yao, waenende katika nashauri Yao.
(Mithali 6:24-25)
Yakulinde na mwanamke mwovu asikupate,
Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni,
Usiutamani uzuri wake moyoni mwako.
(Mathayo 5:28).
Lakini Mimi nawaambia, Kila mtu amtizamaye mwanamke Kwa kumtamani,
Amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
(Yoh 8:44).
Nanyi ni WA baba yenu Ibilisi, na tamaa za baba yenu, ndizo mpendazo kuzitenda
(Ephesians 4:22)
(2 Timothy 2:22)
Lakini zikimbie tamaa za ujanani, ukafuate HAKI na Imani na Upendo, na Amani pamoja na wale wamwitao BWANA Kwa moyo safi.
( 2Timithy 4:3-4 )
Maana utakuja wakati watakapoyakataa nafundisho yenye Uzima, ila Kwa kuzifuata Nia zao wenyewe,
Watajipatia walimu makundi makundi Kwa kuwa Wana masikio ya utafiti,
Nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli na kuzigeukia hadithi za uongo.
( Tito 2:11,12 )
Maana neema ya Mungu iwaokowayo wanadamu wote imefunuliwa,
Nayo yatufundisha kuukataa ubaya na tamaa za kidunia, tupate kuishi Kwa kiasi, na HAKI na utakuwa katika Ulimwengu huu wa sasa.
( Yakobo 1:14-15).
Lakini Kila Mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe, huku ajivuyea na kudanganywa.
( 1Petro 2:11 ).
Wapenzi nawasihi kama wapitaji, na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili, zipinganazo na Roho.
( 2 Petro 3:3)
KUJIPAMBA kwenu kisiwe KUJIPAMBA Kwa nje, yaani kusuka nywele, na kujitia Dhahabu, na kuvalia mavazi.
(. 1Yoh 2:16-17)
Maana Kila kilichomo duniani yaani tamaa ya MWILI na tamaa ya macho, na kiburi Cha Uzima, havitokani na Baba, Bali vyatokana na Dunia.
Na Dunia inapita na tamaa zake, Bali Yeye Atendaye mapenzi ya Mungu, adumu hata milele.
(Yuda 1:16 )
Watu Hawa ni wenye kunung'unika, wenye kulalamika, waendao Kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno yenye kiburi.
(Yuda 1:18)
Ya kwamba waliwambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu.
Amen
ITAENDELEA...........
Cc:
Mzee wa kupambania,
Nakubusu, @Mwandunda,
burning spear,
Tony Cipriano,
Al Watani,
Superfly, @penilogist,
Pendaelli,
Kijungu Moto,
Von Bismarck,
The druid,
Mwalimu wa tuisheni,
fyddell,
Zeus1,
S V Surovikin,
Tim Choice,
kilwa kivinje,
Dexta,
Bush Dokta,
Carlos The Jackal,
Odense,
Mlamba asali,
Emar,
Iceberg9,
Kelvin 35,
alumn,
Chrysanthemum,
Ambition plus,kangesa,kitali,kalpana, lost cousin,
S.M.P2503,
Mshamba hachekwi,
covid 19,
Vito Corleone,
DR HAYA LAND,
Mhafidhina07,
Melancholic,
EDOGUN,
Babu fyee, @Phydum,
madmax,
Abigail Nabal,
Bemendazole,
Spirit of Tanzania, Tausi900,
Gentlemen_
🙏Share ujumbe huu Kwa wengi uwezavyo Ili kuwaepusha na kuzimu ya moto.