alumn
JF-Expert Member
- Jul 15, 2018
- 2,370
- 3,163
Naomba kuongezea katika habari za MWILI, NAFSI na ROHO.
Nafsi ndio kiunganishi ni kiungo muhimu sana kati ya Roho na Mwili pia. Mwili unapokea tu order kutoka katika Nafsi.
Kiujumla kazi kubwa ya Roho ni kumtukuza Mungu. Hilo ndilo haswa kusudi la Mungu toka awali kua Roho imtukuze Mungu.
Sasa kinachokuja kufanyika katika mamlaka zote mbili za Nuru na Giza ni kuikamata NAFSI ili itende sawasawa na matakwa ya hizo Mamlaka mbili.
Hivyo Mwili wenyewe unapokea tu maelekezo ya nini kifanyike ambapo sasa maamuzi yanakua yamefanyika katika Nafsi. Nafsi ni kama Engine.
Ndio maana Ukisoma Zaburi 103: 1-2 Mfalme Daudi anasema eeh Nafsi Yangu umhimidi Bwana, wala usisahau fadhili zake zote. Kumbe kinyume na kumuhimidi Bwana ni Kumuhimidi Shetani. Na hivyo ukimuhimidi Bwana katika Nafsi yako na Mwili wako utaongozwa katika kushinda machukizo yote na Roho yako itakua na Roho wa Mungu ndani yako.
Lakini nimesema kazi kuu ya Roho ni kumtukuza Mungu. Na ndio maana ukisoma Wagalatia 5:16 na kuendelea inasema basi enendeni kwa Roho, wala hamtatimiza kamwe tamaa za mwili.
Mungu ni Roho na anaposema tufanye Mtu kwa mfano wetu ni ilikusudi umtukuze Mungu aliye mfano wako na si vinginevyo.
Lakini sasa tukumbuke ya kua shetani Ibilisi ni Mjanja na Ana akili sana na anayajua maandiko vyema. Kabla hajakufikia kwenye Nafsi yako kwanza anakuachia Mwili wako ukushughulishe tu na dhambi. HAPO HAJAINGIA KUIJARIBU NAFSI YAKO BADO.
Ndio maana ukisoma Warumi 1: 24-32 inasema Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao hata waufuate uchafu hata wakavunjiana heshima miili yao utasoma zaidi ukipata Mda. Hapo unaona ni Mwili wako tu umekutumikisha wala hapo shetani hayupo wala nafsi haijaguswa kabisaa. Dhambi kama ulevi, uzinzi, uongo, punyeto, wizi, n.k ni mambo ya mwili hayo ambayo hata tu kwa maamuzi yako personally na dhamiri yako ikikushuhudia unaweza kuacha. Ndio maana unaweza kukuta Mtu alikua mleviii sana then badae akaacha ukimuuliza anasema aaah niliacha kwa sababu hakukua na faida yeyote niliyopata. Au aah niliacha kwa sababu pesa iliisha. Umeona uamuzi tu.
Na hizi dhambi low standard mimi niziite ndizo zilizoteka watu wengi sasa na ndizo zinazosumbua ( hapa hata shetani hayupo ni kumsingizia tu ni wewe tu na tamaa zako)
Sasa ikitokea hiyo hatua ya hapo juu umeishinda, yaani tamaa za mwili zote umezishinda. Ndipo sasa huyu Bwana Shetani anapoamua kuitumia NAFSI sasa ili kupitia hiyo Nafsi uingie katika dhambi. Na hii nayo ni Level nyingine pia.
Mfano. Ibarahimu anaambiwa amtoe sadaka Mwanae wa pekee na wa kiagano Isaka kwa Mungu. Unaona mfano wa jambo hili? Hili si jambo la kawaida. Hapa NAFSI imeguswa moja kwa moja. HISIA, zimeguswa, AKILI zimeguswa na Utayari au Commitment yaani WILL zimeguswa moja kwa moja. Na ndipo hapa unaona Ibrahim anakubali kumtolea Mungu sadaka na hapo Mungu anambariki.
Kwa hivyo NAFSI ya Mtu ni ya thamani sana. Na shetani akija kukujaribu huku ina maana wewe ni Mtu flani uliye katika viwango Fulani vya juu vya kiimani.
Kuna elimu pana sana hapa. Lakini nakamilisha kwa kusema tu Mwili wa Mwanadamu ni kama Gari inaenda huku na huku sawa na inavyopelekwa na dereva. Nafsi ni kama Engine na Roho ni kama usukani au dereva mwenyewe.
Mkuu Rabbon samahani kama nitakua nimekosea kuongezea Haya ila ni katika kujifunza.