Elections 2010 LIVE ON TV: Kikwete ashinda kuwa rais kwa 61.17%

Elections 2010 LIVE ON TV: Kikwete ashinda kuwa rais kwa 61.17%

ni sahihi lipumba kukabidhi ilani ya cuf?
Amesema haruhusiki lakini anautumia mwanya huo ,sasa kosa lipo wapi ,ikiwa Slaa babu zima ameogopa kuface umma na angeweza direct kuyakataa matokeo hapohapo kama kweli ni mpiganaji lakini wapi hakuwepo ,yaani huku nje unasema umeibiwa ,sasa kama ameibiwa kweli si angeenda hapo na hapo anajua kuwa angetakiwa kusema chochote ,ndio hapo angemwaga mboga ???
 
Tujenge taifa lipi? Hakuna cha kujenga labda una maana kubomoa angalia vizuri ulichoandika
 
Huyo si rais wangu tafadhalini msinihabarishe hayo.
 
mwakilishi wa wagombe (Dr. Ibrahimu Lipumba) anapewa nafasi ya kutoa nasaha zake zilizo jaaa busara. baada ya dr. Silaha kususa

nakusahihisha kidogo , ni Prof. Ibrahim Haruna lipumba !
 
Hongera Lipumba umeweza kuukabili umma na kuonyesha maovu ya tume hadharani ,sijui kwa nini Slaa ameingia mitini ?Hajuiu kama kuna kushinda na kuibiwa ?

Umesahau hata Lipumba 2005 alisusia matokeo na akasema ni kwa sababu anahisi kaibiwa, sasa huyu naye kafanya vivyo
 
Slaa willibrod peter/chadema - 2,271,942 26.34% kwe! kwe! kweeeeee!
ukweli ni kuwa jk umaruufu umeshuka toka 80% mpka 61% hata kama ameshinda lazima ajiulize hizo asilimia zimekwenda wapi!
Nafikiri kwa mawazo yangu ni kuwa kashindwa kupambana na UFISADI thus why! AKUMBUKE PANAPOFUKA MOSHI...................!
 
Ni marekani tu au atafanya Tour ya Dunia nzima subiri tuanze kuhesabu baada ya kuapishwa prove me wrong after? I know this guy very thick
 
Siasa ina machungu yake na kama ni mtu wa kuweka kinyongo basi umepotea njia. kususa ni siasa za maji taka yenye halufu mbaya
Huo ni mtazamo wako, ila kumbuka hakuna tukio la kimapinduzi lililowahi kupewa promo na hakuna mwanamapinduzi aliyewahi kwenda kushangilia mbaradhuli akisherehea unyonyaji na ugandamizaji

Hata angekua Nyerere asingekwenda
 
Mimi mbona napata tafauti?

96,933.00 (1.15%) APPT
5,276,827.00 (62.83%) CCM
2,271,941.00 (27.05%) CHADEMA
695,667.00 (8.28%) CUF
26,388.00 (0.31%) NCCR
17,482.00 (0.21%) TLP
13,176.00 (0.16%) UPDP
8,398,414.00 (100.00%) JUMLA

Weka na zilizoharibika!
 
Mtani wangu Mwiba,

Ukicheka na Nyani, utavua mabua.

Ya bara tuachie wenyewe. Nyie lilieni Zanzibar yenu.

Mmeogopa kumpa kura SLAA ili avunje muungano. Kupe nyie mnafaidi tu vya BURE.

Hakuna wasaliti na watu wanaoipa NGUVU CCM na NEC kama CUF.

Ili kuvunja hii, kwanza ni kuvunja Muungano na CUF ibaki Zenji peke yake.

Hapo tubaki tunabanana wenyewe huku Tanganyika.

SAY NO TO MUUNGANO wa Kupe wa Zanzibar na Wadanganyika.

KAKA, njoo unikatike keki (dada wa miaka 28 eti hana nguvu).
 
Dr.Slaa hawezi kuudhuria kwenye ilo genge la majambazi waliopokonya haki za Watanzania,Mungu yupo na atawahukumu kwahiyo dhambi waliyotenda.
 
Hongereni ccm lakini 20% zimeshuka kwa nini?
 
Inanitia wazimu kuona kuna wengine wanaweza kutoa kashfa kwa upinzania, si elewi kama hawa ni binadamu wa kawaida au mapunguani. Inatisha bado wanaota siasa za chama kimoja, hata Nyerere aliona kukataa vyama vyingi hafiki, akamshauri mzee mzima aruhusu. Kwa maoni, hawa wenye mawazo mgando, wasioona kazi wanayofanya kina Slaa na kuzikebeli si tu wanaumwa bali hawapashwi hata kuishi. Ombeni mwaliko wa kwenda Ikulu mkale pilau na mkwere wakati baba zenu na ndugu zenu wanachemsha majani ya miti ili mradi wawezeishi.
Inasikitisha na kusononesha, mtabeza wapindani mwishoni mtaachia wenye, mwulizeni mramba na Masha
 
1. Kuga peter mziray appt - maendeleo 1.12%

2. Kikwete jakaya mrisho/ccm - 5,276,827 61.17%

3. Slaa willibrod peter/chadema - 2,271,942 26.34%

4. Lipumba ibrahim haruna/cuf - 695,667 8%

5. Rungwe hashim spunda nccr-mageuzi 26,388 0.31%

6. Mgaywa muttamwega bhatt tlp 17,482 0.20%

7. Dovutwa yahmi nassoro dovutwa updp 13,176 0.15%

Huu ni ushindi mkubwa kwa Chadema, kutoka kura chini ya milion 1 mwaka 2005 mpaka over 2m 2010, hata baada ya chakachua bado wameshindwa kupata ushindi wa kishindo
 
Back
Top Bottom