Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Unajitetea bure tu ila kubali ukweli huwez kuwaweka kwenye kikosi chako watu ambao hujawachek kila week live zaidi ya hizo recorded chache, youtube au LFCTV. Kuhusu hiyo LFCTV Ndani ya Azam TV hata sasa hivi naifatilia na wanaonyesha "" 60 MINUTES WITH PATRICK BERGER"".
Toa kikosi chako kwa watu uliowaona kila week live(kuanzia 2000 kwa era yako)
 
Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya England Sven-Goran Eriksson (75), ameeleza baadhi ya mambo ambayo anatamani kuyafanya katika siku zake za maisha zilizobakia.

Mapema jana Kocha huyo mkongwe ameeleza kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya kongosho (pancreas) iliyofikia hatua za mwisho.

Akizungumza na Sky News, Sven amesema mpango wake ni kusafiri na kuhudhuria mechi nyingi.

Aidha mechi anayotamani zaidi awe na nafuu ya afya aweze kuiona ni kati ya kati ya England na Brazil itakayofanyika mwezi Machi huko Wembley.

”Natamani nisiwe na maumivu makali sana, ili niweze kwenda Uingereza kutizama mechi hiyo itakayochezwa Machi 23”.

”Kuamka bila maumivu ni zawadi kubwa sana ambayo watu tunaichukulia kirahisi pale tunapokuwa na afya, lakini tukiugua ndio tunaelewa umuhimu wake”.

Alipoulizwa ikiwa kuna nafasi kwenye soka ambayo aliwahi kuitamani bila mafanikio, alijibu,

β€œKuwa Meneja wa Liverpool, sikufanikiwa , lakini mimi bado ni shabiki wa Liverpool”.

”Nakumbuka nilikuwa nikipishana sana maneno na Sir Alex Fergusson, kuna wakati tulihitaji wachezaji wengi kutoka Manchester United, hii ni kawaida, ile ilikuwa klabu bora sana”

”Namuelewa Fergusson ,alikuwa hapendi tuchukue vijana wake kwa mechi za kirafiki,alikuwa anachukia, lakini tukionana wiki mbili baadaye alikuwa ananisalimia, rafiki yangu , hujambo”.
 

Hilo ni chaguo langu ambalo siwezi kubadilisha sasa shida yako ni nini ndugu?
Mbona tunalazimishana vya kuandika?
 
Wakati Kipara anamuuza Cole Palmer sijui klopp alikuwa wapi
 
Kipa no moja ajae Liverpool anaitwa Pitaluga...mbrazil kama Alison...
Tazama makinda kupitia azam TV kuna channel ya Liverpool tv...wanaonesha mechi za timu za academy...makinda Wengi wazuri wanakuja...Pitaluga ndo atamrithi Allison
Kiukweli mechi za Academy hata kwa mtutu sijakaa kuconcentrate kuangalia.
Huwa naziona sana wanarusha,ila lol
Hazina vibe hata.
 
Kiukweli mechi za Academy hata kwa mtutu sijakaa kuconcentrate kuangalia.
Huwa naziona sana wanarusha,ila lol
Hazina vibe hata.

Mbona mnamkaba sana Miss LiverpoolFc, yeye amesema ni Kelleher tu hao wengine mtajua wenyewe.

Akija kushtuka Kelleher yupo huko Norwich.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…