Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Haya mambo ya working behind the scenes hua yanachosha sana japo vile vile hua yanaweka mashabiki attention maana hatuelewi ni mchezaji yupo anaefuatiliwa kwa karibu nadhan hii pia inawapa muda wanaoshiriki mazungumzo wawe na muda wa ku bargain baada ya idara ya scout kufanya analysis ya wachezaji husika..
Sina imani kabisa na hiki kikosi maana wengine wanaimarisha sana vikosi vyao sisi na huku tupo tunaambiwa wanafanya mchujo kwa hio ni subira na subira yavuta kheri...

YNWA
 

Hii behind the scene faida yake kubwa ni moja tu, unakwepa mfumuko wa bei ambao unaletwa na wakubwa wengi.

Ishu ya Jude ilikuwa tuikamilishe mapema sana kwa bei nzuri kabla ya kumpa headlines na wengine kumfukuzia na wenye pochi wakapita nae.

Kuanzishwa kwa haka kamkakati ni kukwepa hiyo hali, ndio maana imekuwa siri sana. Hata hivyo kwa sasa naona soko limepooza there are no big names, big deals zinatajwa tajwa,

Ngoja tusubiri maana mashabiki wa LFC pressure imepaa juu kwa sasa, hawaelewi nini kinakuja, Slot anakaangwa wanasahau yeye ni mpendekezaji tu hana full authority, FSG wamepoozwa kwa sasa. Naamini bado kuna sajili zitafanyika hasa kwa DM, LCB and RW”,.!!!
 
FSG wako bizy kununua klabu mpya mpaka unajiuliza hawaoni kikosi kimepwaya namna hii kiasi uwezo wa kua contenders haupo tena hata hio Big 4 kuna Uwezekano tukakosa kabisa...
Kile kipigo cha Atlanta ilikua kiwe kama reference point ya usajili dirisha hili...
Ni kweli behind the scenes zinasaidia lakini sio ki vile tazama bei kwa Nunez, Domy, VVD, Allison nk hivyo cha msingi ni identify mchezaji husika na kutazama release clause imekaa aje then ku react..
Tunataka usajili sasa waanze kuingia kwa mfumo mapema.

YNWA
 
Slot on transfers: "The first aim is to work with these players. The disadvantage is that many of them aren't here yet. Positive is that it gives us time to take a good look at the youngsters. Of course Richard and I are trying to improve the squad where possible."
 
Arne Slot:

“The standards are really high to bring in new players. If you inherit a team that’s really good, it’s not easy to find players who are even higher. Richard is working really hard on that.”
 
Arne Slot:

“The standards are really high to bring in new players. If you inherit a team that’s really good, it’s not easy to find players who are even higher. Richard is working really hard on that.”
Mmeshapigwa na kitu kizito kwa huyu kocha...anafanana saba na Boss Klop kwa maneno ya kufariji.
Liverpool kuna uwezekana ikaanza kupata mafanikio ya kurudi nyuma kama enzi za Roger's.
 
Yani mchezaji yupo Bize saluni kuweka lipstick
Tumeipenda wenyewe 🤣🤣🤣hii timu sijui hua wanatuchukulia aje aisee yaani maneno matamu matamu tu huku vitendo ziro kabisa...
Kwa sasa wamewanasa huyo dogo kutoka Chelsea na mwingine kutoka Wolverhampton Wanderers huku Bw Slot akipita kule kule alikopita bwa Klopp na siasa za ku wa please FSG...

YNWA
 
Jana nilimsikiliza Slot kwenye interview, i like that guy yupo so honest na anafunguka vilivyo.

Aliulizwa kuhusu usajili akajibu hivi
"Ukirithi kikosi kipya na kizuri chenye ubora ni ngumu kufanya usajili kwani unashindwa kuchagua aliye juu ya hao ulio nao na atashangaa kama hapatakuwa na usajili.

Data driven so fara inaonesha tuna weakness kwenye mipira ya kutenga both offensively and offensively again kwenye kiungo wa ulinzi kuna udhaifu RE kunahitaji mtu na upande wa LCB pia.

Tunahitaji LCB DM & RW, sasa hapo kuna ishu ya mikataba ambayao Hughes anashughulika nayo Trent, Salahb& Vvd. Tutasajili hiki ndicho naamini kwa sasa ukiangalia Matip na Thiago wameondoka.

Tuendele kusubiri ngoja tuone mechi ya kesho usiku 2:30.

YNWA
 
Mimi ni miongoni mwa wa chache sana naamini hatuhitaji hizi early signings na zishindwe kutusaidia mbelen. Mashabiki kawaida hawana jemw wala baya inategemea na wakati, Nina imani na Arne Slot naamini katika process inayoendelea ndani ya LFC.

Captain Marvelous umesikia point ya Slot kuhusu "atashangaa kama hakutafanywa usajili"?!

Uliwahi kusikia Klopp akisema hata hili neno? Namkubali Slot yupo wazi sana, interview zake zinanivutia...

Arne Slot la la la la.
YNWA
 
Slot Ball EPL are not ready.

Nilitamani tulivyokosa DM wa maana kipindi cha Klopp zaidi msimu jana nilitaman Klopp acheze na double MF pale kati kupunguza mashimo aliyokuwa akiyaacha Endo au Macca, hii ndio kocha mnyumbulifu anavyofanya kuwa na plan B pale A inapoliwa na kirusi, bahati mbaya kwa Klopp ilikuwa tofauti alikomaa na plan yake ile ile bila kujali maneno ya nje.

Nilichokiona jana ni unyumbulifu wa Slot, hakua na natural striker akaamua kucheza na double 10 hapa kama una technician mzuri unafungua low block teams.
Binafsi napenda mpira mzuri zaidi sana wa possession, hua najiuliza kwa nini sikuangukia Arsenal au Barca kwa kipinde kile walikuwa na mpira mzuri, kilichonivuta LIVERPOOL ni Jezi na ile nembo yake.

Je, Slot kutuletea possession football i can say yes he can, jana nimeona hilo la kubuild up kupitia katika kati, changamoto ni kwamba bado wachezaji wapo kwenye system ya Klopp, they are not comfortable bado. Time needed it wont take long sababu utofauti ni mdogo na Klopp style.

Players impressed me alot;

TREY NYONI:-
(what a player, technician one was beautiful to watch, his passes were quality very quality and technical)
It was joy kumuona na mpira unaona raha akipewa unajua imefika mahali salama. He is young with just 17yrs, changamoto ni mwili mdogo kwa EPL ata struggle sana.Thats why at the age if 16+ Klopp alimpa nafasi.

BEN DOAK:-
Young lad huyu Mscotish alishawishi wengi sana miaka hii kabla ya injury yake ile. Wengi ilifikia mahalia wakasema Salah auzwe tuna mchezaji anaitwa Doak(🫠) niliwaelewa wamelewa na kipaji chake, si unajua ukishalewa, huoni husikii? Basi Doak amerudi tena na amekuwa yule yule. Kwa dakika alizocheza nakumbuka ali dribble past kama mara tatu hivi. He is good kwenye ku dribble na he is too direct (wanasema hakwepi mabeki, haogopi).. Asset ya maana hii miaka ya mbele hapo.

Owen Beck:-
Ndio maana Klopp na jopo lake walishawishi arudi kwenye timu, he is so good.. LB wa maana sana huyu future LB akiwa injury free.

Bradley [emoji91][emoji91][emoji91]Huyu bwana mdogo aongeze juhudi zaidi anaweza kusolve kwenye ishu ya RB he is so go good both offensively and defensively.

Eneo ambalo naona halikwepeki kusajili ni DM we must sign defensive midfield. Endo is not enough to carry us next season. He was flop yesterday as a senior player with what he played. Endo umri umesogea kucheza more than 50 matches ni uongo kwa ubora ule ule, DM can solve defensive issue than LCB.

YNWA
 
Hii timu Bora klopp alivyoondoka tu aisee mzee alikua anazingua miaka 9 EPL 1 na timu yake ilikua na uwezo wa kubeba EPL zaidi ya Moja aisee ni bonge Moja la flop
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…