Nilishangaa kuna kipindi huku zililetwa stats za kumlinganisha Suarez na Nunez
Ishu ya Nunez sio bahati wala jambo la kisaikolojia bali ana lack character ya lethal striker kitu ambacho hufundishwi na kocha
Anachokosa Nunez ni ile hali ya kujua apige vipi au achague angle ipi ambayo itampa shida kipa kuokoa, anachofanya Nunez ni kupiga tuu mpira golini, ama akitafuta angle anakosa target
Siku makipa wakiwa hawapo vizuri atafunga kama ile mechi ya kwanza na Newcstle, ila kipa akiamka vizuri ndio yale ya jana
Otherwise timu itengeneze nafasi ambazo Nunez atakua ana tap in tuu mpira uingie golini kama anavyotengenezewaga Halaand
Perspectives.
DARWIN NUNEZ, mpaka sasa ana miezi 18 at LFC.
Tufanya kulinganisha miezi yake 18 na ile 18 ya LUIS SUAREZ at LFC? ni kwaajili ya perspectives.
Maana, LFC fans tunaongea as if Suarez alihit the ground running at LFC, tuonaongea as if, LFC fans walikuwa hawasemi/kuponda kuwa he wasnt good enough kumreplace Torres at LFC, tunasahu na kujisahaulisha sana.
Then, miezi 18 ya kwanza at LFC ya Luis Suarez.
15 goals
3644 minutes
Miezi 18 ya kwanza at LFC ya Darwin Nunez.
14 goals
2949 minutes
Means katika miezi yao 18 ya kwanza, Nunez amecheza fewer minutes kuliko Suarez.
Msimu wake wa kwanza (ofcourse alikuja Janury) 2010/11 alifunga goals 4 katika 13 apps, msimu wake wa pili full, (2011/12) alifunga goals 11 katika 31 apps, msimu wake wa 3 sasa ndiyo akaanza kuevolve, 23 goals in 31 apps, na msimu alioexplode ni 2013/14 ambapo alifunga goals 31 kwenye apps 33, sasa hapa sifananishi ubora wa Suarez na Nunez, nafananisha projections zao, Suarez had to find his feet kwenye league, it took him a while kuadjust his presence kwenye league, na tulikuwepo tuliompa muda.
Na ikumbukwe, kupindi kile ambacho Suarez anajaribu kufind his feet kwenye league, tulikuwa na record signing Andy Carroll, ambaye aliondoka LFC akiwa ni total flop, na baada ya Suarez kuondoka, we signed Balotelli, Origi, Benteke, Lambert etc, katika hizi signings zote aliyekuja kuwa na afadhali ni Origi pekee, then Klopp had to switch Bobby at #9 and the rest was history.
Now we have Nunez, the reason why naamini he will come good, ni vitu anavyo offer uwanjani.
Yes, he's not scoring goals, yes, he misses easy chances, but why hatuangalii vitu vingine anavyooffer? tuna a reliable goal scorer (Salah), na he compliment him a lot, si ndiyo alivyokuwa anafanya Firmino? complimenting Mane & Salah? why ni tofauti kwa Nunez?
Nunez is our counter-trigger, Nunez is one main/pivotal runner, Nunez is our pivotal chance generator, Trent/VVD/Alisson/Konate/Matip ndiyo wanamtumia ku-trigger counters.
Jana, he missed big chances (yes), but he was the PIVOTAL creator wa one first goal, na goal lilikuwa muhimu sana, kabla Newcastle hawajasettle kwenye their game plan, tena baada ya kumiss penalty in the first half.
Newcastle were attacking us kwenye our box, Jones intercepts, mpira unafika kwenye mguu wa Trent, Trent anainua jicho, na kupin-point mpira kwa Nunez, ambaye hapa ameshuka deep kwaajili ya kutrigger counter, mpira unamfikia Nunez, then anm-set up Dom, Dom anadrive/progress kwenda kushoto, sababu ya kudribble ni ku-drag Newcastle MFs/DEfs, anamuachia Diaz, na Dom anaendelea na false runs kwenye box na kufanikiwa kudanganya 3 newcastle defenders, Diaz anapata space ya ku-cut in, na kumpata Nunez, ambaye TAYARI ameshatengeneza a safe channel, mpira unamfikia Nunez, na anapress kwa Salah kwa easy tap in.
So, swali hapa ni kuwa, Haaland ni better goalscorer than Nunez, but Haaland anaweza kufanya alichofanya Nunez jana? yes anaboa kwenye kukosa magoli, but atleast hebu tuwe tunaacknowledge mchango wake mkubwa tu uwanjani, tunatamba na stats za Salah now, but Nunez amechangia kwa asilimia 70%, kitu ambacho Diaz/Jota/Gakpo hawawezi, na ndiyo maana Salah huwa anakuwa at his best akiwa na Nunez upfront.
Again, mbona Nunez anajituma sana uwanjani, anafanya kila alichokuwa anafanya Firmino, suala la kufunga litakuja tu, mpeni jamaa a break Aisee, anasaidia sana team, kama huoni msaada wake its fine.
Kuna msemo huwa anapenda sana kuutumia Gary Neville, "Dont watch the game, SEE the game".