Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Hii sio habari ya kusaidiwa ni issue ya mathematically ndugu.

Kama hii umetafsiri ni kusaidiwa basi huwezi kukataa tayari Chelsea wameshatusaidia jana hivyo tukibeba ubengwa tunapaswa kuwashukuru Chelsea si ndiyo?

HAKUNA TIMU DUNIANI ILIYOWAHI KUBEBA UBINGWA WA LIGI (ISIYO NA KNOCK OUT STAGE) BILA YA KUTEGEMEA MATOKEO YA WENGINE

Narudia tena haipo hiyo Timu na kama unaamini hivyo basi unajidanganya.

Ili ubebe Ubingwa lazima wengine wafungwe na wapinzani wako! Kiufupi kwenye football lazima utaratibu wa "Enemy of your enemy is your friend" lazima utumike.

Hatuwezi wala hakuna uwezekano wa kubeba kombe bila ya kutegemea matokeo ya Timu nyengine! Hii ni principle sio mtazamo wangu.
Kwa ufupi kauli ya kila mtu ashinde mechi zake inapaswa itokee tumebakiza mechi kama 4 hivi halafu tumewaacha wapinzani kwa point zaidi ya 5, hapo ndo tunapaswa kuanza tambo 😄 🤣

Hata hivyo sisi tuna Mungu kama mwenyekiti wangu Malafyale anavyosema hahahah, sijui wao wana nani huko.
 
ile kauli ya kila Mtu ashinde mechi huwa inatoka midomoni tu lakini kiuhalisia moyoni kila mtu anatamani mpinzani wake afungwe.

Ndiyomana unakuta Mtu anasema kila Mtu ashinde mechi zake lakini akifungwa City au Arsenal yeye anafurahi na kushangilia! Sasa unajiuliza huyu anashingilia nini? Si apuuze tu kama anavyopuuza anapofungwa Luton 😂

Mbona Luton akifungwa hashangilii? Kwanini iwe kwa City na Arsenal tu? Hapa ndiyo unakuwa unafiki wa kusema kila Mtu ashinde mechi zake ulipo 😅
 
Mkuu nitazihofia timu nyingne ila sio MURIFE......😂😂😂😂

Mpira haupo hivyo! Saint Anne alipita kila Uzi kujisifu atamfunga Manure pale Anfield hatimae tukaishia kupata sare ya aibu.

Chelsea tumempiga 4 kiulaini tu lakini Man City kaishia kuitafuta Sare.

Hivyo na Manure anaweza kutufunga kirahisi sana na tukatulia tu hasa ukizingatia rekodi yetu ya msimu huu ni mbovu sana kwa hizi Timu kubwa.
 
Heri ingekuwa nyuzi tu,
Nilisumbua mtaa mzima ile siku niliwabeza sana wale nyumbu na kuwakumbushia bao saba tulizowanyuka,kesho yake nikikosa pa kuficha sura yangu
Kila sehemu napigwa spana..sina hamu.
 
Ndio nilikuwa nawatambia hivyo hivyo
Nawaambia Salah tu anayo magoli matatu hapo
Usijistress. Kwenye mpira raha ni ya muda mchache sana na ukiipata kidogo tu tamba. Ni kama sisi unaona jinsi tunazarura kila jukwaa? Tunawatambia maboya kwa sababu tunatembeza vipigo kama FFU. Ila tunajua tukipata hata sare tu, jukwaa letu litajaa watesi wetu mpaka tutalikimbia.
 
Wanasema si tulisema😂

Mie siachi kutamba
Napita kuwakera arse8
 
YNWA🔥
 
Attachments

  • IMG-20240218-WA0020.jpg
    IMG-20240218-WA0020.jpg
    367.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom