Game ya jana naona imetumika ku pad statististics za forwards. Utasikia mchezaji flani ana goal contributions 20+, ataitwa "world class" na kuongezewa hype kumbe alikuwa anacheza na Sparta Prague. Mashabiki wapenda numbers utawaona wakimsifia sana mchezaji wa hivi na kujisemea kwamba wamelamba dume kwa mchezaji huyo.
Faida ya hii ni mchezaji akienda vizuri na vibe, anapata confidence ambayo anaipeleka kwenye Premier league na kujikuta ameongeza magoli na assists zaidi ya matarajio. Mambo yakienda vizuri zaidi mnajikuta mmeshinda kombe.