Livingstone Lusinde anafaa kuwa Waziri wa Wizara ngumu na nyeti nchini

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,119
Reaction score
4,569
Huyu mtu ana akili nyingi sana na ni mzalendo wa dhati mwenye maono mazito juu ya nchi yake. Ni nadra sana kuwa na watu wa aina hii. Tatizo letu watanzania ni kushindwa kuwatumia vizuri watu wa aina hii kwa maendeleo ya taifa letu.

Tangia awe mbunge zaidi ya miaka 10 mfululizo, michango yake bungeni mara zote huwa zilizoshiba na akianza kuchangia bunge zima na nchi nzima husisimuka.

Kutokuwa na cheti cha degree isiwe hoja kwani alichonacho kichwani wengi wa hao wenye vyeti vya madigrii hawanacho vichwani mwao. The man is a real genious. Hakupata fursa ya kuendelea kupata formal education kwa sababu ya ufukara wa kutupwa waliokuwa nao wazazi wake.

Jamii yake ya wagogo ilitambua uwezo wake mkubwa wa akili na wakaamua kumubwaga Malecela aliyekuwa waziri mkuu kwenye ubunge wa jimbo la Mvumi na kumpatia Lusinde. Hapo ndipo jina la Kibajaji lilipatikana kwani tela lilikuwa ni Malecela lakini likapinduliwa na kibajaji.

UDOM, Chuo kikuu kilichoko mkoani kwake sijui ni kwa nini kimeshindwa kutambua akili ya mtu huyu na kumtunukia PhD ya heshima? Watu wa aina hii ndiyo wanaofaa kuongoza wizara zile ngumu zilizowashinda wengi kama ile ya nishati ambayo ilimshinda Lowasa hadi akaachia uwaziri mkuu, akaja Prof Muhongo akavurunda, akaja Ngereja fedha za escrow account zikamuzoa etc.

Wizara nyingine iliyokuwa ngumu ilikuwa ni ya ardhi na makazi. Nayo iliwashinda wengi hadi ilipompata William Lukuvi ambaye naye background yake ni kama ya Kibajaji kwani alitokea kwenye cheti cha ualimu wa primary school hadi kutunukiwa Master degree in political science and economics na Open University of Tanzania (OUT).

Hawa watu ni genious na inafaa tukawatumia vizuri. Michango yao ya mawazo haipaswi tu kuishia bungeni bali inapaswa kufika hadi kwenye Cabinet ambako ndiko kwenye maamuzi ya utekelezaji.

Wizara nyingine ya muhimu sana ambayo imekuwa ngumu kupata mkunaji mwenye uwezo ni wizara ya kilimo. Bashe alijipambanua kupitia michango yake bungeni iliyoshiba kuhusiana na kilimo kama ambavyo Kibajaji amekuwa akijipambanua bungeni. Kwa kuwa Bashe hivyo vyeti vya digrii anavyo, haikumchukua miaka mingi sana kupewa wizara hiyo na leo kila mtu anakubali kuwa wizara ya kilimo imepata mkunaji anayefaa sana.

Angalia leo mchango wake wa namna ya kukabiliana na athari za madhara yatokanayo na majanga kama ya vita ya Russia vs Ukraine, Covid 19 na mengineyo:

 
PhD ya kupewa imeanza lini kuongeza akili? Vyuo vya Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ vitakuwa hopeless and useless vikimpa PhD huyo jamaa.

Labda aandike thesis ya matusi apewe PhD kutokana na thesis hiyo.

Unatudanganya Kibajaji ana Masters, Masters ya wapi? Hii hapa link ya CV yake.



Dr Akili umetuona sisi ni mazwazwa wenzako sio?
 
Sahihi

USSR
 
Huo mfano wa lukuvi ni irrelevant hapo.
Lukuvi alijiendeleza Open University
 
CHAWA CHAWA HASA!!

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
M
Mbona taarifa zimekuwa nyingi
 

1. Inaelekea hujui maana ya honorary degree au kwa jina jingine degree honoris causa. Degree hiyo ya honoris causa haihitaji kuandika thesis wala kushinda mtihani. Na kwa kawaida huwa ya kiwango cha doctorate na mara chache kiwango cha masters. Ni degree ya heshima (for the sake of honor) kwa kutambua mchango wa hekima wa mhusika katika jamii au kwenye sekta mahususi. Hivi nondo zote zenye mshiko ambazo Kibajaji amekuwa akizitoa bungeni na kwenye makongamano mengine, kama zingaliandikwa zote kwenye kitabu kimoja, unadhani kitabu hiko kingalikuwa na kurasa elfu ngapi?

2. Sijasema Kibajaji ana masters degree. Niliyesema ana masters degree ya OUT ni Mh. William Lukuvi aliyeanzia certificate ya ualimu wa primary school kwa sababu ya ufukara wa wazazi wake waliokuwa nao enzi hizo, na si kwa sababu ya kufeli mitihani. Soma vizuri nilichoandika. Na si kweli kuwa Kibajaji huongea matusi bungeni. Hajawahi hata mara moja kumtukana mtu au taasisi ye yote.
 
Samahani mkuu wewe Dokta yako ni ya nini? I mean ya hospitali au doctorate ya PhD?
 
Samahani mkuu wewe Dokta yako ni ya nini? I mean ya hospitali au doctorate ya PhD?
Ninazo tatu. Nina PhD ya medicine, ile ya undergraduate ni MD (Doctor of Medicine) na ile ya tatu ni Doctor of Science. Honoris causa bado sijapewa.
 
Ninazo tatu. Nina PhD ya medicine, ile ya undergraduate ni MD (Doctor of Medicine) na ile ya tatu ni Doctor of Science. Honoris causa bado sijapewa.
✊ Hongera sana kiongozi.
 

Genius NOT Genious !
 
Kibabaji hizo akili azitoe wapi

Hizo ideas si ajabu kaziokotea humu humu J.F na aziwezi kuwa long term solution kwa nchi yoyote isiyozalisha mafuta yake. Maghala ya mafuta ni temporary solution tu.

Angekuwa anasikiliza interview za waziri hiyo ni moja ya agenda yake mara kadhaa ameelezea anatafuta wawekezaji wa kujenga nyongeza ya maghala nchi iwe na uwezo wa kuhifadhi walau three month reserve.

Na kwa upande wangu naweza sema hilo swala nimeliongelea kwa zaidi ya miaka 10 mpaka January alipoliokota JF.
 
HAKUNA KINACHOSHINDIKA CCM APEWE UWAZIRI MKUU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…