Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Huyu mtu ana akili nyingi sana na ni mzalendo wa dhati mwenye maono mazito juu ya nchi yake. Ni nadra sana kuwa na watu wa aina hii. Tatizo letu watanzania ni kushindwa kuwatumia vizuri watu wa aina hii kwa maendeleo ya taifa letu.
Tangia awe mbunge zaidi ya miaka 10 mfululizo, michango yake bungeni mara zote huwa zilizoshiba na akianza kuchangia bunge zima na nchi nzima husisimuka.
Angalia leo mchango wake wa namna ya kukabiliana na athari za madhara yatokanayo na majanga kama ya vita ya Russia vs Ukraine, Covid 19 na mengineyo:
Naunga mkono hoja, kiukweli kabisa huyu ni genius fulani basi tuu!.
Livingstone Lusinde, japo ni darasa la saba tuu, ni kichwa mbaya!, ana uwezo mkubwa na pia ana powers fulani!.
Wanabodi, Kama ambavyo huwa ninajinasibu humu kuwa, japo mimi nina chama, ila sina mtu, kwenye mazuri napongeza, na kwenye mabaya nakosoa, hili ni Bandiko la Pongezi Kwa Mbunge wa Mtera, Mhe. Livingstone Lusinde. Naangalia hapa Clouds TV, Mbunge wa Mtera, Mh. Livingstone Lusinde anahojiwa...