Ushauri mzuri sana Becky, kwa maana ya kijana kujiinua. Lakini mi ningependa kuongeza ushauri juu ya ushauri, atoke wasafi kwa kunegotiate namna ambavyo wote wanaweza kufaidika, yaani isiwe kwa maugomvi, akiwa nje wasafi wamtumie na yeye awatumie ili akuze brand yake nje ya wasafi wakati huko kampuni zote mbili zikiwa katika win-win. Kwamba kwa kazi fulani laizer anapata na wasafi wanapata kitu.
Hiki sijui nyie huwa mnakionaje, binafsi bongo huwa naona biashara nyingi haziendi au zinakufa mapema sababu ya kila mtu kashikilia na kung’ang’ania kijibiashara chake binafsi kidogo kisichokuwa/kisichosogea wala kuongezeka ubunifu, kibiashara kitaenda na kujifia. Najua kuna challenge inayosababisha Joint ventures baina ya wazawa zisifanikiwe, lakini kama vijana wadogo tunatakiwa tulichukue hili kama challenge ya kuingia kwenye sura na ulimwengu mwingine wa biashara. Nimezungumzia hiki katika uwanda mpana wa biashara kwa ujumla naweza nisiwe sahihi katika biashara ya mziki/production ya muziki, wadau mtanisahihisha.
Mtazamo wangu, ni kuwa duniani biashara zote kubwa ni za “mashirikiano”. Kama ipo ya mtu mmoja tu tutate, moja...... mbili.......