Lizer wa wasafi...its time to move on

👍👍👍
 
Amigo heshima yako mkuu!
Ikurudie comrade, pole kwa kifungo kidogo tena cha uonevu wa waziwazi kabisa kwa mambo yao meusi.....
Haya ebu ning'ate sikio nduguyangu, huyu Leizer billionaire wa Tanzanite, imekuaje tena na huko wasafi...???
Maana hapa vijana wananichanganya tu..😇😇
 
Ushauri mzuri...ila muhusika inabidi achukue tahadhari sana katika kuufanyia kazi..vyenginevo majuto yatakuwa mjukuu wake. Nazani ana case studies nyingi tu...Nimemaliza
 
Rebecca labda huna sikio zuri la muziki, au umeathiriwa na promo za media. Jipe muda usikilize miziki tofauti, weka pembeni radio, TV na Instagram.
Laizer anafuata nyayo za Maco Chali wa MJ. Unajua maishani tunazidiana ndoto. S2Kizzy alipopata jina tu hakuchelewa akaanzisha chake ona alipofika.
Kwa Laizer, hakuna producer pale. Ni mbangaizaji tu. Ukubwa wake unategemea zaidi ukubwa wa wasanii anaofanya nao kazi.

The same to Sheddy Clever.

Trust me, akitoka Wasafi na lake halipo.

Truth be told, hana maajabu anabebwa tu.
 

[emoji23]ni kama kwenye magari tu, walianza Noah kila mtu akanunua, wakaja Harriel old model kila mtu akanunua, wakaja altezza na mark x kila mtu akanunua, wakaja verossa kila mtu akanunua
sasa hivi wapo kwenye Harrier ya 2002 na subaru soon zitapita
 
Acha kumpotosha Mkuu ujui anafaidika vipi katika ajira yake hiyo
NB:BORA KIDIGO CHA UHAKIKA KULIKO KINGI USICHOKUA NA UHAKIKA NACHO
Ni bora kidogo cha uhakika,hapo ni mimi na wewe tusio na talent, kabarikiwa kipaji,namshauri tu akitumie fully..
Akili za kimasikini hizi. Matajira wanapanua wigo, they are taking risk. Wanapasua vichwa, hawakai kwenye comfort zone.
Hebu fikiria Toyota angekuwa anategemea soko la Japan peke yake je leo ingekuwa kampuni kubwa?
Labda sija eleweka vizuri au uja nielewa ,na maana sometimes ili mtu afanikiwe ina bidi uwe Risk taker ila siyo kwa kukurupuka
Challenge muhimu Mkuu ila siyo una ingia ulingoni kwa kukurupuka kwa kuwa una jina , muhimu uwe na mikakati thabit, Lizer ni producer mzuri ila siyo the best kuliko wote bongo kinacho fanya anukie ni ilo uwaridi pembeni yake
Unafanya Calculated Risk, na siyo Risk as a Risk for Risk's Sake.

UBAYA NI KWAMBA, WENGI YA WANAO-COMMENT HAPA PENGINE NAO WAMEAJIRIWA KAMA LAIZER ALIVYOAJIRIWA... Na wale ambao bado hawajaajiriwa wapo bize kutafuta AJIRA hizo hizo za kuajiriwa.
SASA CHA AJABU ni kwamba, SISI HATUKO TAYARI KUACHA KAZI ZETU tulizoajiriwa, ila tupo BIZE kumshauri Laizer yeye aache kazi yake ya kuajiriwa.

HII INACHEKESHA SANA!!
MY TAKE; Laizer afanye zote za kuajiriwa na za kujiajiri pamoja, abaki Wasafi hapo hapo huku pia akiendelea kupiga "side hustle" zake nyingine za kujiajiri. Maana yeye mwenyewe alishasema yupo Free kufanya kazi na msanii yeyote wa muziki kama Pesa ipo.
 
💯
 
We umenena vyema zaidi Mkuu
 
💯
 
Wengi mmegamble kusoma ingawa hakuna ajira,

mmeanzisha familia hamjui wala ku calculate mtailisha na nini.

.mmeanzisha biashara mmegamble pia, maana wengi hatuna uhakika biashara ita last next 20 years...

Ninachotaka kusema tuna gamble everyday kwenye decision zetu...

Lizer kukaa kwa Diamond kisa kuna regular income is wrong decision....

Huyo Diamond akipata siombei kifo, Lizer atafanya nini?

Hata move on??

Kwa nini asifanye ku move on sasa hivi?

Plus..

He is talented,

its sick to watch him not using his talent fully....

Mliopo humu mnasema is too risky..

Mkumbuke mimi na wewe hatuna talent...

We have nothing to loose LOL
 
Issue siyo yeye kujiajiri au kuajiriwa. Yule uwezo wake bado mdogo sana.

Anazidiwa mpaka na kina Mocco Genius.
 
Hua nikiona uzi kama huu hua hauchukui muda maneno yatatimia na utaskia kweli Laizer kaondoka
 
Ushauri mzuri sana Becky, kwa maana ya kijana kujiinua. Lakini mi ningependa kuongeza ushauri juu ya ushauri, atoke wasafi kwa kunegotiate namna ambavyo wote wanaweza kufaidika, yaani isiwe kwa maugomvi, akiwa nje wasafi wamtumie na yeye awatumie ili akuze brand yake nje ya wasafi wakati huko kampuni zote mbili zikiwa katika win-win. Kwamba kwa kazi fulani laizer anapata na wasafi wanapata kitu.

Hiki sijui nyie huwa mnakionaje, binafsi bongo huwa naona biashara nyingi haziendi au zinakufa mapema sababu ya kila mtu kashikilia na kung’ang’ania kijibiashara chake binafsi kidogo kisichokuwa/kisichosogea wala kuongezeka ubunifu, kibiashara kitaenda na kujifia. Najua kuna challenge inayosababisha Joint ventures baina ya wazawa zisifanikiwe, lakini kama vijana wadogo tunatakiwa tulichukue hili kama challenge ya kuingia kwenye sura na ulimwengu mwingine wa biashara. Nimezungumzia hiki katika uwanda mpana wa biashara kwa ujumla naweza nisiwe sahihi katika biashara ya mziki/production ya muziki, wadau mtanisahihisha.

Mtazamo wangu, ni kuwa duniani biashara zote kubwa ni za “mashirikiano”. Kama ipo ya mtu mmoja tu tutaje, moja...... mbili.......
 
Sa hivi anafanya kazi ya kumix tu,wasafi wanaimport tu mabeat
Diamond anamletea mabiti ya mfukoni.

Utasikia nataka Beat kama la Joro ya Wizkid.

Beat linachukuliwa unaimbwaibwa ujinga humi, wimbo unaitwa Jeje.

Na kwakuwa media ipo, social media zipo hata kama hutaki utasikiliza tu ngoma zetu.

Ndio maana muziki wa bongo umekuwa takataka kabisa
 
binti kiziwi Mara nyingi upendi kucomment zaidi ya kulike lakini ukicomment tu unaongeaga point haswa Kama umeolewa mume wako ana bahati kubwa Sana ya kukuoa mwanamke Kama wewe by the way hoja Ni nzuri na fikirishi.
 
binti kiziwi Mara nyingi upendi kucomment zaidi ya kulike lakini ukicomment tu unaongeaga point haswa Kama umeolewa mume wako ana bahati kubwa Sana ya kukuoa mwanamke Kama wewe by the way hoja Ni nzuri na fikirishi.
Asante rafiki, nafurahi namna unavyoniona..... na inanipa nguvu ya kujua labda “ni kweli” 😀😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…