Kujadiliana na watu wavivu wa kujifunza kama wewe ni shida huwa mnaingia kwenye mijadala amna ata ABC za industry husika, mnaanza kutukana watu hawajui wakati wewe ndio hujui.
Ata mtu anapojaribu kukuwekea a very easy to read article upate elimu kidogo amsomi kupata premise ya mjadala, sio huu hiyo knowledge inaweza kukusaidia huko mbeleni.
Development planning for the Lake Albert Development Project.
www.tullowoil.com
Link nyingine hiyo nakuwekea Uganda Tullow ndio ilishinda bid 2004 exploration ilianzia 2006 mafuta wamepata 2009. Kama nilivyoeleza awali rarely big companies wanashiriki kwenye upstream exploration hao Total na CNCOOP wameingia kununua share kwa Tullow baada ya kisima kuonekana kina mafuta. Sasa tafuta uone Tullow ni nani hiyo ni government sponsored entity huko UK.
Majadiliano ya pili ya kuanza kutoa mafuta kwenye vitalu na Uganda yalianza 2010 wakaafikiana kwenye technical na commercial aspect kabla 2015, Museveni akaleta hoja mpya za environment na support za local community wakati wanajadili hayo Tullow wakajitoa 2017 kwa kuuza share zao zilizobaki on top ya hoja mpya za Museveni ukaibuka mzozo mwingine wa capital gain tax. Hadi kuafikiana bomba kuanza kujengwa ni 2021 piga hesabu ni miaka mingapi ya majadiliano?
Huo ni mradi wa nchi kavu mkataba wake sio mgumu vile. Sasa unajua environmental concern za marine life kwenye hii miradi with off shore rigs + jumlisha na environmental concern za kujenga LNG hiyo Gas ya baharini inatoka imechanganyika na maji ambayo ni asilimia kubwa, halafu ndio mafuta na Gas.
Umeshajiuliza kama LNG inampango wa kuzalisha 7million tonnes annually ni kiasi gani cha maji machafu yatamwaga? maana kwenye kuchakata inabidi uyatoe maji kwanza ambayo ni very toxic so lazima ujue yanaenda wapi.
Ni hivi watu wanapokuwa wanakosoa kama huna uelewa wa industry yenyewe sometimes bora ufuatilie mjadala au uulize maswali kistaarabu uone wana agenda zao au ni legit concerns; ufafanuliwe kuamua kuliko kuingia kwenye mijadala na kuanza kutukana watu wakati clueless kwenye ABC zake.
Kama nilivyokwambia hayo majadiliano ni tactical and complacency kuzungumza alichozungumza huyo mama mumwambie kazi ya kuendesha nchi inataka umakini sio ya kufurahisha watu.