Liwe somo kuwapa vilaza kama hakina Makamba sensitive sectors. Yeye na kampuni yake hakina Zitto wanachukulia $42 billion ni hela ya mzaha kuirudisha.
Wakitoka hapo wanaongea ujinga wa local contents sijui tutakuwa tunauza kuku mia ngapi kwa siku etc with nonsense.
Muulize sasa hiyo $42 billion ina justy specification za plant au akupe breakdown cost, hawana hayo majibu; ukiwaona sasa wanavyokaa na wawekezaji hayo mapozi yao utadhani watu wa maana wakati atawajui hela yenyewe inarudi vipi.
My guess Tanzania itakuwa imestuka $42 billion ni inflated costs ya mradi. Sehemu kubwa ya hiyo hela itaenda kwa ‘Subsea 7’ kampuni ambayo ni joint venture ya marekani na Norway ni specialised engineering firm ya onshore construction na kutandaza pipes, nyingine inaenda kutoa biashara ya steel kwa makampuni ya Norway ambayo yapo mengi huko kwa kwao na mfaidika mwingine ni LNG construction firm ambayo itakuwa ya kimarekani tu na yenyewe.
Hapo ukidadavua utakuta 90% ya hizo $42 billion zinafaida kwenye uchumi wao wana kila sababu ya ku inflate hizo costs.
Bado sasa hesabu za kurudisha hizo hela ni pasua kichwa na kama sehemu kubwa ya investment ni mkopo with interest ya 6% tu ni shida. Mradi ukianza hela ya investment inatoka kwanza kwenye faida regardless ya hali ya soko (sometimes production is high, sometimes is low). Kuna kanuni zake hapo, if global demand is low kurudisha deni unaweza kujikuta unazalisha na upati chochote zaidi ya kulipa deni tu.
Haya sio mambo ya kukurupuka ni very technical inataka uelewa mpana wa maswala ya finance, oil and gas industry, global politics, etc. Sio mambo ya kukurupuka na kusikiliza ropo ropo za mtu kama Zitto au January ambao uelewa wao wa hayo mambo ni mdogo mno kwa kuwasikiliza.