LNG Project: Njooni tujadili unadhani kwanini mradi wa gesi ya LNG unachelewa na nini chakufanya ili utekelezwe kwa wakati

Mimi nimeeleza kwanini uelewa wao ni mdogo, sasa ili kuonyesha mimi ndio zwazwa ungetuambia ni kiasi gani cha hizo $42 billion dollar zinaingia kwenye mzunguko wa Tanzania.
Unaamini zitto na aliyekua Waziri wa Nishati hajui Hilo!?..acheni ujuaji
 
Wewe ni miongoni mwa watu wema na wakweli katika taifa hili.
 
Wewe unachoelewa $42b ni za nini kwenye huo mradi!?..anakopa nani na analipa nani!?
Unaniuliza maswali ambayo baadhi nimeshaeleza $42 billion sehemu kubwa inaenda kwa contractors ambayo ni makampuni ya Norway na Marekani; nimekutajia na moja kabisa hapo ni Subsea 7.

Ni hivi mnakaa huko Twitter na kuongea petty issues na kudhani hizi investments ni rahisi sana.

We unadhani kwanini miaka zaidi ya 15 tangu vitali vipatiane bado wanasubiri.
 
Ni hoja gani umeanza nayo hadi uwahamasishe wengine kukusapoti? Rudi weka hoja kwenye mada yako, zaidi ya hapo ni mihemko tu uliyo nayo
 
Haya sio kweli tujikite kwenye mambo ya msingi sio kuwasema viongozi. Tujadili mkataba unasemaje, na terms zikoje, stake ilikua ngapi? na Nk.
Ni sawa, nimekuelewa boss ila kwa 25- 30% sio mwanzo mbaya kwani hatuna cha kupoteza na kama ni mkataba hata uwe wa miaka 50 ikifika itakuwa mali yetu kwa 💯 na wakati huo tutakuwa na vijana wetu waliopelekwa nje kusoma ili waje kushika top jobs hapo

Oman walikuwa na mkataba wa mafuta na wazungu kwa 50 years na sasa imeisha na 💯 ni wao na vijana wamesoma ndio wanaofanya kazi zote bila kutegemea watu wa nje hiyo wanaiita nationalization yaani kazi zote kubwa wanashika wao baada ya kusomeshwa na serikali kwa bidii zote
Naungana nanyi na kila la kheri
 
Hizo 26%-30% mmezitoa wapi ?
 
Hii nchi inahitaji at least mwaka mmoja watu wazichape maana sio kwa unyonyaji huu unaofanywa na wawekezaji wakishirikiana na viongozi wetu.
 
Nakumbuka Gas and petroleum Engineering enzi za jiwe Siasa ilifanya kazi kweli kweli sasahivi kimyaaa🤣🤣
 
Kwasababu Zitto amesema basi ni ukweli? [emoji3]
Akisema kitu kikawa tofauti na ukweli haswa katika suala Kama Hilo,anashusha credibility yake na kutia shakani biashara yake ya siasa,Sasa huyo anadai Waziri wa wizara husika hajui kitu kuhusu biashara na mikataba ya gas Ila yeye anajua,huo ni ujuaji wa kijinga!
 
$42b ni gharama ya mradi(capital) ilikua uanze kazi,ambapo makampuni husika yatakopa yajuako,mkataba haujaingiwa,unajadiliwa,we unauliza kiasi gani kitaenda kwenye uchumi wa tz!?..Kama mna bidhaa na malighafi za ujenzi wa miundombinu hakikisheni nyie ndiyo mnatoa,Kama hamna ni obvious vitatoka wanakojua wao,mradi wa maji ya Victoria mkia wa tabora mabomba yalitoka wapi!?..maana hela alitoa mhindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…