LNG Project: Njooni tujadili unadhani kwanini mradi wa gesi ya LNG unachelewa na nini chakufanya ili utekelezwe kwa wakati

Unataka kufanya space exploration wakati wananchi wako bado wanajisaidia porini? Wanao wachagua hao wanasiasa si sisi wenyewe?

Amandla...
 
Gesi inayotajwa hapa sio ya kupikia mchuzi na vitumbua. Inatajwa gesi nyingi ya ndani na kuuza nje ikiwa liquified inayotumika kwenye viwanda na mitambo kuzalisha umeme. Hilo suala la kuchemshia mihogo hata wafanye nchi nzima sio hata 5% ya uzalishaji, very negligible kibiashara. Hatuwezi zungumzia $42 billion alafu tukawaza njaa za tumboni.

Qatar wanaendelea mradi wao wa expansion ya production. Watajenga plants, watajaribu kulinda mazingira, watajenga tanks na miundombinu nyingine kwa jumla ya $28 billion zitazidi kidogo sababu ya inflation na delay ya COVID-19. Mradi wao utazalisha tani milioni 33 za gesi ukianza, bado kuna nyongeza miaka ijayo.

Sasa linganisha Qatar wanaojenga mradi very efficient, una mbwembwe nyingi sijui kupunguza madhara ya mazingira, una teknolojia kubwa na ya gharama na watatumia around$30 billion.

Naomba kuuliza mnisaidie. Sisi tutumie $42 billion kabla ya inflation na cost overrun;

Kuanzisha mradi wa kuzalisha kiasi gani cha gesi kwa mwaka?
Kama wanataja gharama za mradi, capacity ya mradi ni ipi. Huwezi nitajia bei ya gari tu bila kutaja specifications.

Faida za moja kwa moja ni zipi?
Nchi nyingine kama Urusi, Qatar, Marekani, Iran, Norway kwa kutumia makampuni kama haya yanayokuja kwetu wanataja uwepo wa miradi ya ziada kama faida ya LNG kuna Helium plants kuzalisha, kuzalisha sulphur kuuza viwandani, kuongeza uzalishaji wa umeme, wengine kama Norway miradi yao iko booked production kabla haijaanza waliishapata 80%+ ya soko la gesi itakayozalishwa. Sisi matarajio na malengo yetu ni yapi?

Nilisikia faida ni kama kuzalisha ajira, sasa kwani kupata mayaya kwa ajili ya wageni wazungu na kupata mafundi mchundo ni lazima tutumie $42 billion?
Kuongeza sijui apartments mara soko la bidhaa za ndani kama saruji. Hatuwezi kopa zaidi ya trilioni 90 TZS na hatujui faida direct, tunaambiwa faida za ziada. Unawezaje lima mahindi ekari 20 ukiweka akili zako zote kwenye kuvuna pumba na magunzi badala ya unga wenye thamani kubwa.

Justification ya kutumia $42 billion siioni kabisa hata kama sina utaalamu. Mbona wengine wanatumia hela chini ya hapo na wanafanya makubwa yanayotajwa.
 
Mkataba gani wa hovyo wa gas ulisainiwa awamu ya 4!?..uhovyo wake ni upi!?
Rejea mswada wa dharura uliopelekwa bungeni tena kwa speed ya 5G awamu ya 4 kupitisha mikataba ile ya hovyo ya Gas tena walipewa kitu kdg, wabunge wa Upinzani wakaipinga sana na siku ya kupiga kura wabunge wa upinzani walitoka NJE!
 
Mkuu kama una marafiki wanajua kama wewe tunaomba wavute waje hapa walete michango.
 
Tushampa Rostam tender taifa gas.
 
LNG (Liquified Natural Gas) yaani gesi asilia iliyokatika hali ya kimiminika baada ya gesi asilia iliyo katika hali ya gesi kupoozwa katika - 162 Degree centigrade.

Lengo la kuibadilisha ni ili iweze kusafirishwa katika masoko ya kimatiafa yaliyo mbali kirahisi na kwa wingi.

Karibuni katika mjadala.
 
Kitu cha kwanza tuandae VIJANA WETU VIZURI SANA

AT LEAST 5000-Hi IQ and very well paid.

Wazalendo ambao pesa haitakuwa tatizo but to make a business successful.

Wanaweza kusomea Norway,Germany au Australia.

Maeneo ya kusoma:

GAS AND OIL TECHNOLOGIES
GAS AND OIL BUSINESS PLAN/Management.
GAS AND OIL TAXATION.
-FERTILISER
-PET RASINS
GAS AND OIL RESEARCH AND PROFUCT DEVELOPMENT.

OTHERS.

Tunakwama sana kuendeleza RASILIMALI zetu kwa Sababu hatuna RASILIMALI watu!

HATUJAANDAA VIJANA.

Na wakiandaliwa wanakuwa Frustrated na mishahara midogo!



Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Rejea mswada wa dharura uliopelekwa bungeni tena kwa speed ya 5G awamu ya 4 kupitisha mikataba ile ya hovyo ya Gas tena walipewa kitu kdg, wabunge wa Upinzani wakaipinga sana na siku ya kupiga kura wabunge wa upinzani walitoka NJE!
Sheria ya mikataba kupitiwa bungeni ilitungwa kipindi cha mwendazake huko nyuma mikataba ilikuwa ni siri na ngumu kujua nini kiliendelea
 
Anachomaanisha wanataka kushirikiana na Exxon Mobil kuiba gas hiyo kwa hoja ambazo sio za kiuwekezaji.

Bwana huyu anataka, akina Zitto na Makamba waeleze faida ya moja kwa moja ambayo taifa itapata na namna ya kurudisha mkopo huo kwa mkopeshaji. Bila shaka umeelewa mkuu?
 
Hapo wapo JK, Makamba, Rostam na Abdul
 
Tulitakiwa kuanza utekelezaji hata kabla ya Mozambique.
mpaka mtu ajue tumechelewa au tumewahi anatakiwa kujua kinachoongelewa.
Mi naona shida yetu ni utashi wa kisiasa.
Angalia hata hii PNG ambayo tunayo tayari hapa nchini,ni wangapi wananufaika nayo?

Matumizi ya nishati hii muhimu kwenye magari,walau hapa DSM ni kidogo sana
kwa sababu ya kutotangazwa.
 
Karibuni karibuni watu mliopo huko wizarani, kwenye mashirika mbalimbali, kwenye taasisi za umma na binafsi tunaombeni michango yenu.

Huu ni mjadala wa mwaka 2024.
 
Jamaa wanapiga hela ndefu sn
Acha watu wenye akili wachambue mada na sisi tuelewe,

Wewe uwezo wako ni hoja za CDM na mambo kama hayo,

Nakuomba sana usituharibie mjadala, hapa hakuna mambo ya masihara,

Nadhani umeelewa , kwa hiyo tulia kwanza,

Hoja za upeo wako ni nyingi tu zinakuja,

Kuw mvumilivu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…