"Long Distance Relationship" yako ilidumu kwa muda gani au huataki hata kusikia mahusiano ya mbali?

"Long Distance Relationship" yako ilidumu kwa muda gani au huataki hata kusikia mahusiano ya mbali?

hahaha its either one or both parties are cheating or the man has mastered the art of shaking hands with the one eyed milkman
 
Mwaka 2007 nikiwa narud zangu hom, yeye alipandia bus Arusha tukiwa tunarudi Mwanza na Akamba bus, tumesafiri usiku kucha, asubuh iliyofuata tumefika Magu akaniomba simu apige kwao waje kumpokea nikampa. Akaniomba namba yangu nikampa, tukawa tunawasiliana hatukuweza kuonana tena, nikarudi shule na yeye akarud shule mawasiliano yakaisha hadi alipomaliza form 4 akanitafuta tena mawasiliano yakarud. Penzi likanoga, kipindi nipo chuo yeye akawa form 5 Loreto, nilipomaliza Dip ikanibid nirud Mwanza nikaungane na wangu wa ubani. Mapenzi yale yalikuwa matamu sijawahi pata ya namna ile.

Penzi lilikuja ingia mdudu alipoingia chuo semister ya pili, ilikuwa ni tar 25. July 2012 ndio penzi letu lilikatizwa na yeye aliponiambia hanipendi tena yatupasa kuachana. Oyaa! Sikieni tu kuachwa na mtu ambae ushamtia nafsini, moyoni na akilini. Alijua kunitesa yule binti, nilimuomba msamaha kwa nisichokijua kwa miaka 2 ila alishikilia msimamo wake kuwa hana mapenzi na mimi yeye alishaga move on. Eeeh! Hapo sasa nilizibuka akili nikakung'uta vumbi nikasonga.

Baada ya lile tukio nimekuja kuwa mtu mmoja imara sana kihisia na kimahusiano na mwenye roho ya chuma cha pua kimahusiano. Strength always is found in difficult situations
 
Back
Top Bottom