joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Mbona Kenya wamewaambia ukweli?, hapa Tanzania walitukatia misaada baada ya kuona uchumi haufanyi vizuri, nchi nyingi tu zimeelezwa ukweli na kuombwa zirekebishe sera zake za uchumi?, kwanini Tanzania waseme uchumi upo vizuri na kukubali kumwaga mapesa?, kwahiyo huo UNAFIKIA wanaufanya Tanzania pekee isiwe Kenya na nchi zingine?.Sasa unajuaje kwamba hawana mengi zaidi ya kusema ila wanajizuia kwa sababu za kidiplomasia?
Kwa nini wanasema uchumi utashuka?
Nimetoa maelezo ya kina sana kuhusu neno "excution of fiscal plans", haina maana uchumi utafanya vibaya, ila kutokana na kuchelewa kwautekelezaji wa fiscal plans za mwaka huu kutokana na marekebisha makubwa yanayofanywa nchini ya kiuongozi, baadhi ya fiscal plans inaweza isikamilike ndani ya mwaka huu, huwezi kufanya mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiuongozi kiasi hiki na ukategemea kasi ya uchumi ibaki vile vile, na WB wametumia neno soften kumaanisha pressure au acceleration ya mwendo kupungua, huwezi kubadilisha gear wakati mguu bado umekanyagia pedal ya accelerator.