Hapa bongo ninadiriki kusema hakuna bondia wa kizazi hiki anayehujumiwa wazi wazi kama Loren Japhet.
Kwa haraka haraka ninaweza nikakutajia fights tatu alizohujumiwa wazi wazi mpaka mashabiki tukabaki mdomo wazi.
Fight ya kwanza aliyohujumiwa bila aibu ni ile fight dhidi ya Muhsin Alkasus kwenye hii fight Muhsin alipigwa vibaya mno Yani kama punch bag jamaa alipochoka kumpiga akaanza kumchezea show gemu na wengi tuliiona kabisa jamaa amescore vya kutosha round zote cha ajabu Muhsin ndiye akatangazwa eti ndo kashinda.
Fight ya pili aliyohujumiwa ilikuwa dhidi ya Juma Choki ,hii fight mpaka sasa hakuna shabiki yoyote aliyekubaliana na uamuzi wa majaji.
Fight ya tatu ni hii ya jana dhidi ya Nasibu Ramadhan (Pacquiao) wengi ndo hapa tukabaki mdomo wazi.
Hii ni aibu sana, majaji watende haki kijana wana muhujumu sana
View attachment 2689779