Low Profile ni Mbinu itakayokusaidia katika mapambano ya Maisha

LOW PROFILE NI MBINU ITAKAYOKUSAIDIA KATIKA MAPAMBANO YA MAISHA

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Nilisema, usitafute Wala usilazimishe kuheshimiwa na kîla Mtu.

Nikasema, siô lazima kîla Mtu akuheshimu, nikimaanisha siô kîla heshima ni muhimu kwako.

Nasema, kîla heshima inakuja Kwa Wakati wake.

Usipende kuonekana au kukuonyesha mbele za Watu kama Mtu Mkubwa, Mtu WA muhimu, Mtu wa Maana. Hiyo haitakusaidia zaidi itakusumbua Hapo baadaye.

Penda kuwa mtu wa Kawaida, hata kama unajijua unauwezo Fulani, unacheo Fulani, unangugu Fulani, usipende kuonyesha uwezo wako au umuhimu wako sehemu àmbayo Hakuna ulazima wa kufanya hivyo.
Onyesha uwezo wako pake àmbapo unahitajika na kûna huo ulazima wa kuuonyesha.

Umemaliza chuo Kikuu upo zako mtaani, ishi Maisha yako kama Watu Wengine wa mtaani. Siô lazima Watu wajue umesoma kama hakuna ulazima wakujua.

Kama Elimu yako itahitajika Hapo mtaani ndîo waweza kuitumia.

Watu watakutambua tuu kupitia actions zako, maneno yako watajua huyu Kijana au huyu Binti anauwezo Fulani.

Low Profile itakusaidia kuwa Flexible. Utakuwa unabadilika badilika Kulingana na Hali na mazîngira. Tofauti na kujipa high profile Kwa kujiona wamaana, wahadhi, mwenye umuhimu àmbapo kûna ishu utakuwa umejiwekea mipaka kutokufanya.

Mfano,
Kufika na kufika unajifanya unaelimu, sijui umetoka familia za kishua, au una connections za wakubwa. Hii itakusumbua sehemu kwani utashindwa kufanya Baadhi ya ishu zako.

Mfano,
Umemaliza chuo Kikuu umewambia Watu wewe unandugu weñye vyeo vikubwa hivyo unaconnection za Kazi.
Baada ya kuhitimu, Muda unasonga ajira Huna, kujiajiri unaona aibu Kwa sababu mtaji Mdogo hauwezi kufungua biashara kûbwa zinazoendana na hadhi uliyojipa.

  • Kuuza Karanga hutaki,
  • Kuuza Dagaa hutaki,
  • Kuuza juisi hutaki.
  • Kuwa dalali hutaki.

Mwisho unaingia kwèñye mtego wa mateso.

Hata kama unaconnection Huwezi kujipa High profile, connection zinaweza kukatika Kwa ghafla mahali àmbapo haujatarajia. Unashindwa kubadilika Kwa sababu tayari unaona NI fedheha kuwa chini.

Wakati nasoma chuo Kikuu pale UDSM, Kûna wanafunzi walikuwa wakihangaika kubadili nguo na viatu pamoja na Simu kwa kujipa high profile, kujipa hadhi wengi wao malengo yao makuu yakiwa ni kuwavutia Wanawake.
Jambo ambalo wengi liliwagharimu Sana. Bumu kuisha mapema, kusumbuliwa na Wanawake haohao àmbao wanawafanya wavae nguo za kîla namna ili wawavutie.

Binafsi sikuwa na nguo nyingi waliosoma na Mimi wanajua Hilo. Kiasi kwamba unaweza kuzikariri nguo zangu. Hiyo Kwangu haikuwa shida na Saikolojia ya Watu wanakuzoea vile utakavyojiweka. Watoto Wakali unachukula, na bado unaishi Low Profile, Low Key.

Mtu afanye Jambo Ikiwa analipenda na siô kufanya Jambo Kwa kujionyesha Kwa Watu au kujipa umuhimu au hadhi. Hiyo itamgeuza kuwa mtumwa.

Mfano, Mtu àmbaye yupo Low Profile hawezi kuwaza atavaa nguo gàni isipokuwa ataweza nguo iliyosafi.
Lakini anayejipa umuhimu, au hadhi lazima awe mtumwa Kwa Watu wengine. Kwani ataona akirudia nguo Fulani Watu watasema Amerudia na ataonekana Hana Pesa.

Wewe Mtu akikuona Huna Pesa unapungukiwa kitu gàni?

MTU akikuona Huna Elimu au Akili unapungukiwa Jambo gàni.

Wakati Fulani nilikuwa najifunza Kushona Nguo, Binti mmoja alikuwa akija pale ofisini mara, akawa ananitazama, kumbe alikuwa na yake. Siku Moja akaniuliza, mbona wewe ni kijana mdogo mwenye mvuto (akimaanisha handsome) why umechagua Kazi hii. Ati yeye anaona nimepotoka, hakujua ninasoma, fundi alipomwambia ninasoma Chuo Kikuu akabaki ameng'aka.

Low Profile itakupa Pesa.
Low profile itakufanya uishi vizuri mtaani.
Low profile itakusaidia kukupa data mbalimbali za kiintelejensia kuhusu fursa zitakazokusaidia kwèñye Maisha yako.

Low profile itakusaidia kupata Mchumba au mwenza Sahihi Kabisa.

NI kupitia Low Profile Watu unawajua tàbia zào vile walivyo. Yaani uhalisia wa Binadamu.

Ukishajua uhalisia wa Watu Maisha hayawezi kukusumbua Kwa sababu Maisha ni michakato ya Watu kuchangamana na kuzalisha màtukio na Matokeo.

Low profile itakufanya Watu wasijue upo kwèñye Wakati mgumu au wakati wa bata. Yaani hautabiriki.
Ukiwa na Pesa Watu hawajui ukiwa hauna Pesa Watu hawajui. Waô wanakuona upo vilevile Siku zote.

Tafsiri ya Low profile ni kujiepusha na mashindano na Watu yasiyo na ulazima, yasiyo na tija.

Low profile hata Kazini itakuepusha na vita kutoka Kwa Watu visivyo na umuhimu.

Kama hujajipa hadhi au kujiona wa Maana, au Bora niambie ni kitu gàni kinakufanya uone aibu kufanya Kazi hata ya kipato cha elfu tatu au tano Kwa Siku ujipatie kipato umeona Bora ukae tuu bila Kazi. Huoni kama unajipoteza?

Moja ya sifa ya Mzazi Bora hata kama yeye anahadhi Fulani atamfundisha Mtoto wake kuwa Low Profile.
Huo ndîo ulinzi Namba Moja Kwa Mtoto. Hata Siku Mzazi akiwa hayupo Mtoto anauwezo wa kupigana vita yoyote na akashinda.

1. Kuwa Low Profile, low Key
2. Soma mazîngira na Watu
3. Tumia mazîngira na Watu kupata Yale unayoyaona ni muhimu kwako.
4. Linda heshima na uaminifu utakaopewa na Watu lakini kamwe usilazimishe kuheshimiwa na kuaminika.
5. Usipende kupigana vita mara Kwa mara kama Hakuna ulazima, kama ukiweza piganisha maadui zako wapigane wènyewe Kwa wènyewe.
6. Shiriki kusaidia Watu wanyonge lakini weñye HAKI.
7. Saidia Watu weñye nguvu kutenda Haki.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Kwanini mtu "upambane na maisha? kwani ulijileta mwenyewe hapa duniani?

Mfumo wa maisha kamili tayari Muumba wetu katupa, tuufate tu huo, hatuna haja ya kupambana wala kujiumiza vichwa. Kila kitu tumeumbiwa sisi tukitumie na vipi tuishi tumeshapewa Mwongozo.

hatuna kabisa sababu ya "kupambana" na maisha.
 
Naam Mkuu
Kwa lugha ya kiimani wanasema kuwa Humble.

Mbinu hiyo imetumika na Kina Musa, Yusuph, Daudi na Ibrahim na wôte walitoboa.

Hata viongozi wakubwa wa Sasa wale weñye tambo na kelele nyingi na mikwala wanashindwa kirahisi kuliko wale watulivu
Uko sahihi kabisa. Hata biblia inasema tusiwe kama mafarisayo wanaopenda kukaa viti vya mbele. Na zaidi kuna andiko jingine linasema kaa viti vya nyuma na pale mwenyewe akikuona na kukuhamishia kiti cha mbele basi utajisikia vizuri. Ukikimbilia vya mbele halafu akaja mwenye heshima kukuzidi na ukahamishiwa nyuma utaumbuka. Hii yote ni kutuasa tu-play low profile. Hata mimi ni mtu wa aina hiyo na kuna wakati nakwepa kufuatana na jamaa yangu fulani ambaye ni mtu wa kujitweza vibaya sana.
 
Nimeelewa zaidi hapo ulipogusia kuwa kanuni hii itafanya uwafahamu watu wako wa karibu vizuri. Maana wengi hupenda kujikweza na kuweka kila kitu hadharani hata pasipo na sababu ya msingi.

Na wengi watajiweka Mbali na wéwe Kwa Sababu wataogopa shida zako kumbe Wala huna shida kihivyo
 
Uko sahihi kabisa. Hata biblia inasema tusiwe kama mafarisayo wanaopenda kukaa viti vya mbele. Na zaidi kuna andiko jingine linasema kaa viti vya nyuma na pale mwenyewe akikuona na kukuhamishia kiti cha mbele basi utajisikia vizuri. Ukikimbilia vya mbele halafu akaja mwenye heshima kukuzidi na ukahamishiwa nyuma utaumbuka. Hii yote ni kutuasa tu-play low profile. Hata mimi ni mtu wa aina hiyo na kuna wakati nakwepa kufuatana na jamaa yangu fulani ambaye ni mtu wa kujitweza vibaya sana.

Yesu huyo Mzee wa Falsafa za kujizima data na kujifanya Hana power
 
Ahsante mkuu wacha nikae hapa, nina Demu wangu alijifunza kutumia jf kutokana na mimi kuspend muda mwingi huku kias nikawa sina muda nae. Siku hiz anasema jf kuna Mtibeli ana nondo sana ndo zinaniharibu akili.🤣

Hongera sana.

Mwambie wewe ni Ndugu yàngu😀😀
 
Kwanini mtu "upambane na maisha? kwani ulijileta mwenyewe hapa duniani?

Mfumo wa maisha kamili tayari Muumba wetu katupa, tuufate tu huo, hatuna haja ya kupambana wala kujiumiza vichwa. Kila kitu tumeumbiwa sisi tukitumie na vipi tuishi tumeshapewa Mwongozo.

hatuna kabisa sababu ya "kupambana" na maisha.

Ya Mungu muachie Mungu yakaisari muachie kaisari.

Mungu hahusiki na kîla kitu.
Yapo àmbayo amewaachia viumbe wake wafanye Kwa utashi waô
 
Hiyo ni Moja ya mbinu Bora

Lakini nakushauri
Usitumie njia Moja tu
Hata mkwara Kuna sehemu unakuvusha
Wanasema, pesa huna hata mkwala?

Vijana changanya mbinu
Tusiamin katika uhalisia na unyonge pekee

Unaweza pata favor ya kupata pesa na kula pisi kali Kwa kuvimba tu
 
LOW PROFILE NI MBINU ITAKAYOKUSAIDIA KATIKA MAPAMBANO YA MAISHA

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Nilisema, usitafute Wala usilazimishe kuheshimiwa na kîla Mtu.

Nikasema, siô lazima kîla Mtu akuheshimu, nikimaanisha siô kîla heshima ni muhimu kwako.

Nasema, kîla heshima inakuja Kwa Wakati wake.

Usipende kuonekana au kukuonyesha mbele za Watu kama Mtu Mkubwa, Mtu WA muhimu, Mtu wa Maana. Hiyo haitakusaidia zaidi itakusumbua Hapo baadaye.

Penda kuwa mtu wa Kawaida, hata kama unajijua unauwezo Fulani, unacheo Fulani, unangugu Fulani, usipende kuonyesha uwezo wako au umuhimu wako sehemu àmbayo Hakuna ulazima wa kufanya hivyo.
Onyesha uwezo wako pake àmbapo unahitajika na kûna huo ulazima wa kuuonyesha.

Umemaliza chuo Kikuu upo zako mtaani, ishi Maisha yako kama Watu Wengine wa mtaani. Siô lazima Watu wajue umesoma kama hakuna ulazima wakujua.

Kama Elimu yako itahitajika Hapo mtaani ndîo waweza kuitumia.

Watu watakutambua tuu kupitia actions zako, maneno yako watajua huyu Kijana au huyu Binti anauwezo Fulani.

Low Profile itakusaidia kuwa Flexible. Utakuwa unabadilika badilika Kulingana na Hali na mazîngira. Tofauti na kujipa high profile Kwa kujiona wamaana, wahadhi, mwenye umuhimu àmbapo kûna ishu utakuwa umejiwekea mipaka kutokufanya.

Mfano,
Kufika na kufika unajifanya unaelimu, sijui umetoka familia za kishua, au una connections za wakubwa. Hii itakusumbua sehemu kwani utashindwa kufanya Baadhi ya ishu zako.

Mfano,
Umemaliza chuo Kikuu umewambia Watu wewe unandugu weñye vyeo vikubwa hivyo unaconnection za Kazi.
Baada ya kuhitimu, Muda unasonga ajira Huna, kujiajiri unaona aibu Kwa sababu mtaji Mdogo hauwezi kufungua biashara kûbwa zinazoendana na hadhi uliyojipa.

  • Kuuza Karanga hutaki,
  • Kuuza Dagaa hutaki,
  • Kuuza juisi hutaki.
  • Kuwa dalali hutaki.

Mwisho unaingia kwèñye mtego wa mateso.

Hata kama unaconnection Huwezi kujipa High profile, connection zinaweza kukatika Kwa ghafla mahali àmbapo haujatarajia. Unashindwa kubadilika Kwa sababu tayari unaona NI fedheha kuwa chini.

Wakati nasoma chuo Kikuu pale UDSM, Kûna wanafunzi walikuwa wakihangaika kubadili nguo na viatu pamoja na Simu kwa kujipa high profile, kujipa hadhi wengi wao malengo yao makuu yakiwa ni kuwavutia Wanawake.
Jambo ambalo wengi liliwagharimu Sana. Bumu kuisha mapema, kusumbuliwa na Wanawake haohao àmbao wanawafanya wavae nguo za kîla namna ili wawavutie.

Binafsi sikuwa na nguo nyingi waliosoma na Mimi wanajua Hilo. Kiasi kwamba unaweza kuzikariri nguo zangu. Hiyo Kwangu haikuwa shida na Saikolojia ya Watu wanakuzoea vile utakavyojiweka. Watoto Wakali unachukula, na bado unaishi Low Profile, Low Key.

Mtu afanye Jambo Ikiwa analipenda na siô kufanya Jambo Kwa kujionyesha Kwa Watu au kujipa umuhimu au hadhi. Hiyo itamgeuza kuwa mtumwa.

Mfano, Mtu àmbaye yupo Low Profile hawezi kuwaza atavaa nguo gàni isipokuwa ataweza nguo iliyosafi.
Lakini anayejipa umuhimu, au hadhi lazima awe mtumwa Kwa Watu wengine. Kwani ataona akirudia nguo Fulani Watu watasema Amerudia na ataonekana Hana Pesa.

Wewe Mtu akikuona Huna Pesa unapungukiwa kitu gàni?

MTU akikuona Huna Elimu au Akili unapungukiwa Jambo gàni.

Wakati Fulani nilikuwa najifunza Kushona Nguo, Binti mmoja alikuwa akija pale ofisini mara, akawa ananitazama, kumbe alikuwa na yake. Siku Moja akaniuliza, mbona wewe ni kijana mdogo mwenye mvuto (akimaanisha handsome) why umechagua Kazi hii. Ati yeye anaona nimepotoka, hakujua ninasoma, fundi alipomwambia ninasoma Chuo Kikuu akabaki ameng'aka.

Low Profile itakupa Pesa.
Low profile itakufanya uishi vizuri mtaani.
Low profile itakusaidia kukupa data mbalimbali za kiintelejensia kuhusu fursa zitakazokusaidia kwèñye Maisha yako.

Low profile itakusaidia kupata Mchumba au mwenza Sahihi Kabisa.

NI kupitia Low Profile Watu unawajua tàbia zào vile walivyo. Yaani uhalisia wa Binadamu.

Ukishajua uhalisia wa Watu Maisha hayawezi kukusumbua Kwa sababu Maisha ni michakato ya Watu kuchangamana na kuzalisha màtukio na Matokeo.

Low profile itakufanya Watu wasijue upo kwèñye Wakati mgumu au wakati wa bata. Yaani hautabiriki.
Ukiwa na Pesa Watu hawajui ukiwa hauna Pesa Watu hawajui. Waô wanakuona upo vilevile Siku zote.

Tafsiri ya Low profile ni kujiepusha na mashindano na Watu yasiyo na ulazima, yasiyo na tija.

Low profile hata Kazini itakuepusha na vita kutoka Kwa Watu visivyo na umuhimu.

Kama hujajipa hadhi au kujiona wa Maana, au Bora niambie ni kitu gàni kinakufanya uone aibu kufanya Kazi hata ya kipato cha elfu tatu au tano Kwa Siku ujipatie kipato umeona Bora ukae tuu bila Kazi. Huoni kama unajipoteza?

Moja ya sifa ya Mzazi Bora hata kama yeye anahadhi Fulani atamfundisha Mtoto wake kuwa Low Profile.
Huo ndîo ulinzi Namba Moja Kwa Mtoto. Hata Siku Mzazi akiwa hayupo Mtoto anauwezo wa kupigana vita yoyote na akashinda.

1. Kuwa Low Profile, low Key
2. Soma mazîngira na Watu
3. Tumia mazîngira na Watu kupata Yale unayoyaona ni muhimu kwako.
4. Linda heshima na uaminifu utakaopewa na Watu lakini kamwe usilazimishe kuheshimiwa na kuaminika.
5. Usipende kupigana vita mara Kwa mara kama Hakuna ulazima, kama ukiweza piganisha maadui zako wapigane wènyewe Kwa wènyewe.
6. Shiriki kusaidia Watu wanyonge lakini weñye HAKI.
7. Saidia Watu weñye nguvu kutenda Haki.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Huu mkakati wa low profile umenipa utajiri wa Viwanja kwa bei rahisi.Naongea na Wananzengo kwa kujifanya mimi ni daraja lao huku nikikusanya data za kujitajirisha!!
 
Back
Top Bottom