Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Moja ya vitu ambavyo vitampa wakati mgumu mh Lowasa ni swala la Richmond.

Ikumbukwe kuwa Lowasa alijiuzulu Uwaziri Mkuu kwa kashfa ya mitambo ya ufuaji wa Umeme ya Richmond.

Mpaka sasa Lowasa hajawahi kuzungumzia kuhusu kashfa hiyo na ndio itakayo muweka kwenye wakati mgumu kipindi cha kampeni.

Ushauri wangu kwa El, Huu ndio wakati wa wewe kuwaambia Watanzania kuwa Richmond ilikuwa ni ya nani?.
Na usipowaambia basi usijaribu kusimama Jukwaani kwani kashfa ya Richmond itakusulubisha.

Haiwezekani Mtu una kashfa kubwa namna hiyo tena iliyotikisa Nchi wakati huo alafu sasa unapiga Kifua kuwa utakuwa Rais wa Nchi.

Huu ni ushauri wangu kwa El.
 
mwenzenu naomba usiku kucha lowasa apitishwe na ccm ili iwe rahisi kutumia maovu yake katika kampeni za mtaa kwa mtaa huku dr au prof akijinadi bila shida

enyi miccm sikieni killio changu tumewachoka
 
Wewe hujui ni ya nani hadi uambiwe na Lowasa?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Moja ya vitu ambavyo vitampa wakati mgumu mh Lowasa ni swala la Richmond.

Ikumbukwe kuwa Lowasa alijiuzulu Uwaziri Mkuu kwa kashfa ya mitambo ya ufuaji wa Umeme ya Richmond.

Mpaka sasa Lowasa hajawahi kuzungumzia kuhusu kashfa hiyo na ndio itakayo muweka kwenye wakati mgumu kipindi cha kampeni.

Ushauri wangu kwa El, Huu ndio wakati wa wewe kuwaambia Watanzania kuwa Richmond ilikuwa ni ya nani?.
Na usipowaambia basi usijaribu kusimama Jukwaani kwani kashfa ya Richmond itakusulubisha.

Haiwezekani Mtu una kashfa kubwa namna hiyo tena iliyotikisa Nchi wakati huo alafu sasa unapiga Kifua kuwa utakuwa Rais wa Nchi.

Huu ni ushauri wangu kwa El.

Ni sawa kabisa lowasa sasa atutajie mwizi mwenzie
 
Ni sawa kabisa lowasa sasa atutajie mwizi mwenzie

No kweli kabisa. Kuna wanaojaribu kusema ni Rostam, lakini Rostam asingefanikiwa kama pasingekuwepo na complies na kama mwenzetu ni accomplice kwa Rostam nalo aliseme kama ni maneno tu atwambie uswahiba wake na Rostam ni wakuhusu nini? Mtaji WA hisa za Rostam ktk VodaCom ni malipo yatokanayo na Richmond, je EL na yy anaingizaje humo hisa zake?
 
Kakudanganya nani kuwa Lowasa atafika kwenye hatua ya kampeni? Nakuhakikishia kuwa tutamchinjia Lowasa baharini hata kwenye top five hatakuwepo
 
Mkuu ebu acheni Ujinga wengine hapa tunatumia akili na sii masaburi... Sasa kama habari hii ni yakweli.. Lowassa alijuaje na kutaka kuuvunja mkataba ikiwa mkataba ulikuwa wa JK rais wake....

Halafu JK kusema tu alikuwa akipata ushauri wa makatibu wake (watendaji wa kiserikali) inaonyesha wazi JK alikuwa akifuata sheria na taratibu za kiserikali laa sivyo asingewahusisha makatibu wakuu kama alivyofanya Lowassa na ushahidi upo akiwaamrisha hao makatibu na waziri wafuate maagizo yake....Tafuta jingine!

Hayo ya 1997 we are interested ni kujikosha na kutafuta huruma za JK...Hata mahakamani mkosa baada ya kupatikana na kmakosa, hupewa muda wa kuomba, kujieleza kabla ya kuhukumiwa kifungo..

we ndio punguwani kabisa.kwani alipovunja mkataba na city water ilkuaje?hujui vitu kaa kimya kima we
 
Lowasa hawezi kusimama hadharani akaikana Richmond ataumbuka kwa sababu hata kama sio yeye lakini ni Ccm na yeye ndie alikuwa mtendaji mkuu wa Ccm,nisawa nakuikwepesha Epa na Ccm haiwezekani kuelewa hata kwa mnywa gongo!
 
Lowassa amekana rasmi kuwa yeye hahusiki na mkataba wa Richmond!

images

Nanukuu:

Mwisho wa kunukuu

Hii leo si sahihi hata yeye (Lowassa) kuhukumiwa kwa kuzingatia kile kinachodaiwa kuwa ni mtizamo wa umma dhidi yake unaompa sura ya ufisadi, jambo ambalo amedai kwamba siyo la kweli.

Chanzo: Mwananchi

2015 ni mwaka wa kazi na asiye fanya kazi na asile,nadhani EL Anaweza kutufikisha kule tutakako kama atapewa nafasi,tunaelewa kuwa kila binadamu ana mapungufu yake na mapungufu hayo hayawezi kumnyima mtu haki yake ya kupiga ama kupigiwa kura
 
mwizi ni mwenyekiti,hii haimhusu lowassa kabisa,
TEAM lowassa
 
Last edited by a moderator:
mwenzenu naomba usiku kucha lowasa apitishwe na ccm ili iwe rahisi kutumia maovu yake katika kampeni za mtaa kwa mtaa huku dr au prof akijinadi bila shida

enyi miccm sikieni killio changu tumewachoka
Kwanini alitudanganya kuwa yeye ndiyo muhusika wa richimond? Angekana sikuileile kuwa hausiki tungemsaka mwizi wetu yeye kawakingia mgongo alafuleo anataka kutuona Mbu mbumbu siyo? Kama kakutuma umsafishe humu hutaweza kichwa chake kimechafuka ungaa
 
Maneno mazito lakini chini ya uongozi shupavu wa Dr Prof Col Kikwete lolote linaweza kutokea hasa tukifuatilia rekodi zake za nyuma usije shangaa akifungua uzinduzi wa kampeni Jangwani na kutuaminisha waTanzania Lowassa ni jembe.Umesahau serekali anayoiongoza ilikuwa imemshtaki Mramba ni yeye binafsi aliyekwenda Rombo kumnadi Mramba kwamba ni kiongozi safi,mchapakazi,muadilifu.....Utakuja kuniambia natamani isiwe hivyo lakini ndio hivyo tena.

Kakudanganya nani kuwa Lowasa atafika kwenye hatua ya kampeni? Nakuhakikishia kuwa tutamchinjia Lowasa baharini hata kwenye top five hatakuwepo
 
Mh.Lowassa yuko safi hana doa wala kasoro,uwezo wake na nguvu ya kukubalika ndio unaomfanya ashambuliwe na wasaka tonge la urais ccm.
 
Moja ya vitu ambavyo vitampa wakati mgumu mh Lowasa ni swala la Richmond.

Ikumbukwe kuwa Lowasa alijiuzulu Uwaziri Mkuu kwa kashfa ya mitambo ya ufuaji wa Umeme ya Richmond.

Mpaka sasa Lowasa hajawahi kuzungumzia kuhusu kashfa hiyo na ndio itakayo muweka kwenye wakati mgumu kipindi cha kampeni.

Ushauri wangu kwa El, Huu ndio wakati wa wewe kuwaambia Watanzania kuwa Richmond ilikuwa ni ya nani?.
Na usipowaambia basi usijaribu kusimama Jukwaani kwani kashfa ya Richmond itakusulubisha.

Haiwezekani Mtu una kashfa kubwa namna hiyo tena iliyotikisa Nchi wakati huo alafu sasa unapiga Kifua kuwa utakuwa Rais wa Nchi.

Huu ni ushauri wangu kwa El.

Mkuu naungana na wewe, issue ya richmond ndio karata ya mwisho naya ushindi kwake ikiwa ataitumia vizuri. Yaani naamini siku Mh EL atakapo sema ukweli nchi itatikisika na hapo nuru na giza vitakapotengana na hapo ndipo Mgombea anayefaa kuliongoza taifa atakapoonekana kwa kila mtu katikati ya hilo giza na nuru.
 
No kweli kabisa. Kuna wanaojaribu kusema ni Rostam, lakini Rostam asingefanikiwa kama pasingekuwepo na complies na kama mwenzetu ni accomplice kwa Rostam nalo aliseme kama ni maneno tu atwambie uswahiba wake na Rostam ni wakuhusu nini? Mtaji WA hisa za Rostam ktk VodaCom ni malipo yatokanayo name Richmond, je EL na yy anaingizaje humo hisa zake?

Wewe utuambie urafiki wako na hao ambao ni marafiki za ko ni WA nini? Acha ulevi na bange we timu maembe. Unachukua wapi urafiki wa mtu mwingine? Mtaangaika sana mwaka jamani.
 
Lowasa kaficha siri kwa heshma ya serikali Rais kung'atuka sio jambo dogo kwa maana issue ya Richmond ilitokea muda mfupi baada ya uchaguzi na serikali ilisha-spend a lot of money-akitoka Rais ujue ni uchaguzi mwingine na ni a lot of money pia' Lowasa aliona familylah bora atoke yy kuepusha mauchaguzi mengine
 
Siku kama ya Leo tarehe 7 mwezi februari 2008 nchi yetu ilikuwa katika hali ya sintofahamu katika kile kilichoitwa sakata la Richmond. Sasa ni miaka saba imepita zipo siri nzito zimejificha nyuma yake lakini siku hadi siku tunayaona mabadiliko na kukua kwa Imani ya Watanzania.

Baada ya Alhamis ile ambayo naiweza kuiita ni Alhamisi ya ushindi wa mahafidhina walio jaa damu ya watanzania kwa Maneno mafupi naweza sema kwa Lugha ya kiingereza (You can win a battle but you loose a war) mambo kadhaa sasa yamewekwa hadharani juu ya hayo na kupoteza mwelekeo wa taifa.

UKWELI WA SERIKALI KUSHINDWA KESI DHIDI YA RICHMOND.
Katika shauri la serikali lilofunguliwa dhidi ya iliyoitwa kampuni hewa ya Richmond, kama ilivyo njia fupi ya mfitini baada ya maelezo marefu ya kifitina ya Tume ya mwakyembe serikali iliishtaki Richmond kwa kupata mkataba kwa ulaghai , Richmond walijieleza mahakamani kwa vielezo vyote na kushinda kesi na hata serikali ilipo kata rufani ilishindwa tena , hii siri mahafidhina hawaitaki kuizungumza sababu mahakama ilithibitisha mkataba kuwa ulipatikana kihalali.

SIRI YA SERIKALI KUTOLIPA HATA SENT TANO KWA RICHMOND HADI LOWASSA ANAJIUZULU.
Lowassa aliamua kujiondoa katika serikali huku serikali ikiwa haijapata hasara hata ya sent moja kwani binafsi Edward Lowassa alijijua ni mtu safi na amejiuzulu kwa sababu ya tatizo la uwaziri Mkuu, Kwani malipo kwa Richmond yalisimamishwa hadi pale walipo shinda kesi mahakamani.

SIRI KUHUSU MITAMBO YA KUZALISHA UMEME YA DOWANS INAYO TUMIKA HADI LEO.
Mahafidhina wale wale kwa kutumia bunge la Samwel Sita walisema mitambo ile ya Richmond haiwezi kununuliwa na serikali kutoka Symbion kwani haiwashi kibatari huku Dr Rashidi akiwa amewaita wakaguzi huru kutoka Ujerumani na wakauthiditisha kuwa ipo imara, wakasababisha kujiuzuru kwa Dr Rashid na kuumbuliwa na Hillary Clinton na Obama kwa kuikubali walipo itembelea. laitani wangeinunua kama Dr Rashidi alivyo shauri tungelikuwa tunaokoa garama za capacity charge Toka kwa DOWANS.

KUSHUKA KWA UFAULU MARA KADHAA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI.
Wasomi na wataalamu mbali mbali wanao amini katika Vision au Creativity huamini njia pekee ya kufikia lengo la aliebudini ni kuwa mmoja ya watekelezaji , Edward Lowassa ni mmoja ya walio kuwa na dhamira ya dhati ya Elimu ,alisimamia shule za kata kujengwa nchi nzima takribani shule elfu moja toka 2006 hadi 2008, Kujiuzulu kwake kuna siri nzito ya Serikali ya kushindwa kujenga vyumba vitatu vya maabara,hili tunafichwa kuwa serikali imeshindwa kufikia lengo.

KUONGEZEKA KWA WIZI SERIKALINI NA UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA.
Hapa ndipo ilipo siri nzito ya takribani miaka saba sasa, Edward Lowassa alikataa kushiriki michezo michafu, mahafidhina waliozoea kula kwa takribani miaka miwili ya Uwaziri Mkuu mianya ya Rushwa ilizibwa na kiasi cha kufanya waunde na waandae zengwe la kumtoa katika nafasi, na wote walio shiriki katika kumng'oa Lowassa madarakani wanahusika katika masakata ya wizi hivi karibuni kuanzia ,Pesa za Congo kwa watu kuchukua pesa na kuwapeleka wanajeshi wetu vitani, Escrow, Nguzo za Kinyerezi, Vitambulisho vya taifa NIDA, Bandari na Vibali vya sukari.

MWISHO.
Watanzania wenzangu hebu tufumbuke macho, mtanzania mwenzetu anahatarisha maisha yake, furaha yake ya kuwa Tanzania , anapambana Siku zote kuufuta umasikini. Tutafakari siku ya Leo Tar 7/02 /2015 kwa maisha ya watanzania kwa maisha na mustakabali Wa Taifa . Ni imani yangu siku ya Leo itaonyesha tashwira ya taifa hili kuelekea Maamuzi na Matumaini Mapya na Edward Lowassa 2015.
 
Back
Top Bottom