Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Mkuu mi nawashangaa sana humu mashabiki wa Lowassa. Maana kama ni mpira upo half time, halafu yuko nyuma kwa goli
moja,... kwa vile mpira bado unadunda lolote linaweza kutokea kwenye CC, ila si jambo la kushangilia kabisa kwa mashabiki wa Lowassa kwa issue ya gamba kurudishwa CC. Wangeiua na kuizika palepale kwenye Nec.

Kumbuka azimio la gamba ndio litawaongoza wajumbe wa CC na azimio la kujivua gamba halikutamka ushahidi wa kimahakama, limeongelea wale "wanao tajwatajwa kwenye kashfa" na wananchi.. Kama bado kuna mtu anategemea ushahidi wa kimahakama you better go figure chenga ya mwili aliyopigwa Lowassa.

CC haina wenyeviti na makatibu wa mikoa(watu wake ni almost 3/4 ya kundi hili), haina wabunge wake(ambao ni wote kumi wanaowakilisha bunge Nec), haina wajumbe wa UVCCM except Kaimu Mwenyekiti Malissa(Nec alikua na wajumbe 10 kati ya 12 wa UVCCM), kwa kifupi he has a mountain to climb. Sanasana amebaki Malissa, Pindi Chana, na January Makamba, Khatib haeleweki, Wassira haeleweki na Mwenyekiti haeleweki. Wajumbe wa CC waliobaki wote si watu wa njaa ya kumtumikia mtu binafsi...

mpira hauko half time! Umemalizika! EL aliipongeza NEC kurudisha hilo swala CC halafu huko watamwita ajieleze, na jambo la pili, mbona Lowasa tu ndiye anajadiliwa sana kwenye hili swala? Akipona itakuwaje? Waliyomhukumu watazungumza nini tena? Tuwe 'neutral.'
 
Lakini twende mbele turidi nyuma... kuna lipi geni haswa ambalo leo hii limetushtua sana.. Dr.Slaa aliwapeni list ya Mafisadi na tukaambiwa yote yaliyokuwemo tukabisha na kumwita mdini sasa haya ya vikao vya CCM ndio tunategemea kuupata ukweli kutoka huko?..Hivi kweli Lowassa hawezi shtakiwa bila idhini ya rais? hawezi kuitwa bungeni na kamati ya bunge kuhoijiwa kama raia kutokana na ushahidi mdogo uliopo maanake MarekaniUK na nchi zote zilizoendelea ikitokea tuhuma kama hizi mshitakiwa huitwa na wale wenye ushahidi mdogo huitwa pia wakahojiwa hadi kieleweke. Kama atakutwa na makosa bunge hukabidhi kesi hiyo vyombo vya sheria..

Majuzi tu tuliona wale ma CEO wa Mabenki wakiitwa, Shell Bp, Mwenye gazeti la uzushi wote hawa wakiitwa bungeni na kuhojiwa iweje kwetu kila mkosa maadam ni kiongozi wa serikali basi akijiuzulu imetosha! na maadam hatuna ushahidi basi hawezi shtakiwa wala kujibu tuhuma hizo bungeni?...Kina Rostam, Meghji, Karamagi, Msabaah na wengineo wote leo wanatucheka na kuweka mfano mbaya sana wa uongozi kwamba ukishikwa pabaya jiuzulu tu utakuwa msafi na mambo yanakwisha.

kuioji watuhumiwa siyo kazi ya bunge.
 
Mkuu ebu acheni Ujinga wengine hapa tunatumia akili na sii masaburi... Sasa kama habari hii ni yakweli.. Lowassa alijuaje na kutaka kuuvunja mkataba ikiwa mkataba ulikuwa wa JK rais wake....

Halafu JK kusema tu alikuwa akipata ushauri wa makatibu wake (watendaji wa kiserikali) inaonyesha wazi JK alikuwa akifuata sheria na taratibu za kiserikali laa sivyo asingewahusisha makatibu wakuu kama alivyofanya Lowassa na ushahidi upo akiwaamrisha hao makatibu na waziri wafuate maagizo yake....Tafuta jingine!

Hayo ya 1997 we are interested ni kujikosha na kutafuta huruma za JK...Hata mahakamani mkosa baada ya kupatikana na kmakosa, hupewa muda wa kuomba, kujieleza kabla ya kuhukumiwa kifungo..

Kwa hiyo tunachoambiwa hapa ni kuwa hatufahamu ukweli kuhusu Richmond, yaani Lowassa anatakaa ndani ya Kikao kuwa Richmond si yake lakini hasemi ni ya nani, na anasema rais ndiye aliyemkataza kuvunja mkataba. Na JK anadai kuwa makatobu walimshauri.....bado kuna swali how did we get there, who got us to Richmond na kwanini wahusika hawajaadhibiwa? Kuna uwezekano kweli Rais na Waziri Mkuu wasijui mkataba unaoingiwa na serikali. Fool can't fool me again.
 
we uko nchi gani bwana...huyo rais gani atakaempeleka gerezani mwenzake katika tanzania hii???na asimalize muda wake wa katiba ipi hasa itakayomtoa madarakani?labda jeshi liasi,wabongo kwa kupenda ku create fear isiyokuwepo hatujambo,tuliambiana hapa oooh jk akishika madaraka mkapa atanyea debe!kiko wapi?kwa mfumo wa ccm ulivyo mwenyekiti ana nguvu nyingi sana kupita maelezo jk muoga tu mwenyewe au ana ajenda ya siri na huyo lowassa wake,lakini kumshughulikia hashindwi hata chembe,hata wale uv ccm hawajui tu kwamba kugombana na mwenyekiti wa ccm ni hatari sana kwao kama mwenyekiti angekuwa strong,anaweza kuuvunjilia mbali huo umoja wao kama alivyotishia juzi!ipo mifano huko nyuma na wala haitakua mara ya kwanza,ngoja tuwakumbushe nyie vijana!

CCM inaweza kufanya kama ilivyopata kufanya huko nyuma:

Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, UVCCM iliweka msimamo uliokuwa unachagiza wagombea vijana wapewe nafasi ya kuwania urais. Majina yaliyokuwa yakitajwa wakati huo ni pamoja na ya kina Kikwete na Lowassa, waliokuwa wakiungwa mkono na kina Anne Makinda na wengineo. Joto lilipozidi, uongozi wa juu wa UVCCM uliondolewa na hali ikabaki salama.
Baadhi ya waliokuwa katika uongozi wa UVCCM wakati huo ni pamoja na John Guninita ambaye leo ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam. Vijana wengine wa enzi hizo ni pamoja William Lukuvi ambaye sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu, Leonidas Gama ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Muhammed Seif Khatibu, John Henjewele na Said Mwambungu ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Aidha, wachambuzi hao wanasema hata ?kujivua gamba? kulikwishakufanyika ndani ya CCM japo kwa msamiati mwingine, lakini wenye maana karibu na huo.
?Mwaka 1984 walisema hali ya kisiasa ilikuwa imechafuka na kuchafuka huko kukaondoka na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi. Baadaye mkono huo wa CCM ukamfikia Maalim Seif Shariff Hamad na wenzake.
ni zamani siyo sasa na hali ya upinzani ilivyo.
 
Mkuu ungweka kabisa hivi: Lowassa, Sumaye wabwatuka CCM
  • WALIA KUCHAFULIWA NA MAKADA WENZAO,NEC YARIDHIA GAMBA KUREJESHWA CC
Neville Meena na Habel Chidawali, Dodoma Thursday, 24 November 2011
salamu-lc.jpg
MAWAZIRI Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, jana walishambulia kwa maneno makali wajumbe wawili wa Sekretarieti ya CCM kwamba wamekuwa wakikivuruga chama na kusababisha mgawanyiko uliopo. Lowassa aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu, kutokana na kashfa ya Richmond ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumzia suala hilo wakati wa mjadala wa hali ya siasa, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichomazika jana mjini Dodoma. Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zinasema Lowassa alianza kubwaga moyo wake baada ya NEC kuridhia ombi la Kamati Kuu ya chama hicho (CC) kwamba suala la mageuzi ndani ya CCM maarufu kama kujivua gamba lirejeshwe katika kamati hiyo ili lifanyiwe kazi kwa taratibu za kawaida za kinidhamu baada ya wahusika kukataa kuachia nafasi zao. “Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,”Lowassa alinukuliwa akihoji. Lowassa alinukuliwa akiwataja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, John Chiligati kwamba wamekuwa wakitukana watu ovyo kwa fedha wanazopewa na CCM. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Lowassa alitumia dakika saba kumshambulia Nape kwamba amekuwa akifanya mambo nje ya utaratibu na kwamba mwenendo huo umekuwa ukikibomoa chama badala ya kukijenga. Baada ya maneno ya Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Sumaye alisimama na kuhoji sababu za chama hicho kunyamazia ukiukwaji wa taratibu ambao umekuwa ukifanywa na watendaji hao. “Mwenyekiti huyu bwana (Lowassa) amesema kwamba amechafuliwa kwa miezi saba, sasa kama leo tunasema kwamba tunarudi kwenye utaratibu wa kamati za maadili, hao waliomchafua watafanywaje?” Sumaye alinukuliwa akihoji. Hata hivyo, taarifa za ndani ya kikao hicho zilimnukuu Kikwete akisema kwamba viongozi hao watakuchukuliwa hatua za kinidhamu kama watakuwa wamefanya hivyo. Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwasihi wajumbe kuachana na suala hilo na badala yake kuchangia maeneo mengine ya taarifa hiyo ya hali ya siasa iliyowasilishwa na Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje ya CCM, January Makamba. Kikwete alinukuliwa akihitimisha hoja hiyo kwa kusema kwamba: “Jamani hapa tunajenga chama, watu wanasubiri kusikia tukimaliza kikao chetu kwa ugomvi, naomba tumalize kwa amani na twendeni tukajenge chama chetu”. Richmond yatajwa Vyanzo vyetu vilimnukuu Lowassa akizungumzia suala la Kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond kwamba yeye aliamua kuvunja mkataba baina ya kampuni hiyo, lakini Rais KIkwete alimwambia subiri baada ya kuwa amepata ushauri wa Makatibu Wakuu. Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), alinukuliwa akisema: “Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?”. “Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,”alinukuliwa akihoji Lowassa. Kadhalika kada huyo wa CCM alinukuliwa akimkumbusha Rais Kikwete kwamba: “Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo”. Lowassa alisema kama alivyozungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa walipokutana jijini Dar es Salaam, tatizo kubwa analolifahamu la vita ya sasa ni urais wa 2015. “Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 walipoleta tuhuma za mtizamo wa umma dhidi yako, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,”alinukuliwa Lowassa katika maelezo yake ndani ya NEC Alisema kwa kuzingatia mazingira hayo, hii leo si sahihi hata yeye (Lowassa) kuhukumiwa kwa kuzingatia kile kinachodaiwa kuwa ni mtizamo wa umma dhidi yake unaompa sura ya ufisadi, jambo ambalo alidai kwamba siyo la kweli. Baada ya Lowassa na Sumaye kuongoa, kada maarufu wa chama hicho, Kingunge Ngombale Mwiru alisimama akitaka kuongelea dhana ya gamba ndipo Mkapa alipomshtua Kikwete kwamba hoja hiyo ifikie mwisho. Baadhi ya wajumbe waliiambia Mwananchi kwamba wakati Lowassa akiongea Mkapa alionekana kufurahi. Kujivua gamba Kufuatia uamuzi huo wa NEC hivi sasa mpango wa kujivua gamba ulioasisiwa na chama hicho, Aprili mwaka huu unarejeshwa CC ambapo watuhumiwa wote wa makosa mbalimbali watafikishwa mbele ya Kamati za maadili na kuchukuliwa hatua kwa taratibu za chama hicho. Mpango wa kujivua gamba ulilenga kuwashinikiza watuhumiwa wa ufisadi kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama hicho na sasa unarejeshwa Kamati Kuu (CC) ili ichukue hatua zaidi kwa wale waliogoma kujiuzulu. Hatua hiyo inatokana na kuwapo ukimya ambao unaashiria kutokuwapo viongozi na makada ambao wako tayari kujiuzulu nyadhifa zao kwa hiari yao kama ilivyotarajiwa. Tangu kupitishwa kwa mpango huo maarufu kwa jina la kujivua gamba katika kikao cha NEC kilichopita cha Aprili mwaka huu, ni kada mmoja tu, Rostam Aziz aliyechukua hatua za kujiuzulu ubunge wa Jimbo la Igunga na ujumbe wa NEC, lakini wengine wamekuwa kimya hadi sasa. Katika kikao cha Aprili NEC hiyo ya CCM ilipitisha maazimio 26, lakini kubwa ni lile lililokuwa likihimiza vita dhidi ya ufisadi kuendelea na kutoa mwito kwa watu wanaotajwa na jamii kuhusika na ufisadi ambao wako ndani ya chama kujitathmini kisha kuchukua hatua za kuachia madaraka waliyonayo. Sehemu ya mwisho ya azimio hilo inasomeka: “Wasipoachia madaraka chama kiwachukulie hatua mara moja”. Mmoja wa wajumbe wa CC ambaye ameomba jina lake kuhifadhiwa alisema: “Tunawaomba NEC waturuhusu jambo hili tulifanyie kazi sisi (CC) na litafanyiwa kazi kupitia taratibu za kawaida za chama kwa kuzingatia kanuni na taratibu za maadili za chama hicho”. NEC yawakaanga kina Jairo Katika hatua nyingine, NEC imeunga mkono hatua zilizopendekezwa na Bunge dhidi ya watumishi wa umma waliotajwa katika ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, iliyoanika uozo wa matumizi mabaya ya fedha za Umma ndani ya Wizara ya Nishati na Madini. Kamati hiyo katika ripoti yake iliyowasilishwa mwishoni mwa Mkutano wa Tano wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita mjini Dodoma, iliwataja Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (aliyesimamishwa), David Jairo na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kwamba wanastahili kuchukuliwa hatua. Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, huku wabunge wakipendekeza pia kuondolewa madarakani kwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Adam Malima
Mkuu, Mh. Lowasa asiwe na uoga watanzania tumemkubari awe Rais wetu 2015, kama atapendekezwa na Chama chake, ila kama anaona kuna mizengwe basi atoke CCM ajiunge na chama chochote na awe mgombea Urais tutampatia kura zetu hata akitaka kuwa mgombea binafsi tutampatia.
 
mpira hauko half time! Umemalizika! EL aliipongeza NEC kurudisha hilo swala CC halafu huko watamwita ajieleze, na jambo la pili, mbona Lowasa tu ndiye anajadiliwa sana kwenye hili swala? Akipona itakuwaje? Waliyomhukumu watazungumza nini tena? Tuwe 'neutral.'

Inaonekana uelewa wako wa siasa za ndani ya CCM ni mdogo sana au haupo kabisa.

Lowassa ataitwa akajieleze kwenye kamati ya maadili, hii kamati haina mamlaka ya kufanya uamuzi wa mwisho wa kujivua gamba. Mamlaka hayo ni ya nec na nec wamekubali kuipa CC. Halafu tujiulize kama lile azimio la kujivua gamba lilitaka ushahidi wa kimahakama au lilitaka nini? ukishapata jibu...GO FIGURE!

Why Lowassa anasakamwa?!... hivi unaishi bongo au unafuatilia siasa za bongo au uko NEPTUNE?
 
Lowassa angewajibu kamati ya Mwakyembe bungeni, au angewapeleka mahakamani, WaTanzania sio Mabwege tena, Suala la umeme lilikuwa la dharura iliyosimamiwa na Waziri Mkuu Mwenyewe sio Wasaidizi wake!

Pesa za Richmond zilibiwa kwa kutumia Sheria, So ni Sheria tu ndio inaweza kumsafisha Lowassa sio vikao vya chama. Kwa kusema kwake kwamba Wapinzani hawamsemi, anasema kwamba ameshawagawia mgawo or What? LOWASSA WATANZANIA WOTE SIO MABWEGE TENA!


Yaani unasema JK hayumo....kwa nini hapelekwi gerezani, unajua ni aibu kumkuta teenager ana kamasi zinamshuka kama mtoto wa miaka 4?? CCM wote wezi!! iacheni Tanzania huru!!
 
kweli mlijipanga...mliandaa mpaka ngonjera na mashairi kumpongeza jamaa kwa kusema tu "alipiga simu"!!!!pongezi nyingine bwana...hivi huyo mwanaume wenu wa shoka (kwa mujibu mwenzenu mmoja-sofia simba)anawalipa kiasi gani na kwa style gani wenzetu na sisi tuje huko????na hapo bado kakaenu kubenea j5!kazi hiyo kuizuia kamati isimchinje mshkaji baada ya kupewa kibali cha kufanya hivyo na nec juzi!
We umelipwa shilingi ngapi kutoa mawazo yako hapa?
 
Hatimaye CCM imevaa GAMBA. Ngonjera, usanii, na uwendawazimu wa viongozi na watendaji wa CCM umejidhihirisha. Mahakama, takukuru, usalama wataifa polisi wangefanya kazi walizofundishwa bila kutumiwa kama TV haya yote yangekuwa historia. DPP yuko kwa ajili ya wewe usiye na kadi ya CCM au CCM ikikuchoka.
 
Kalamu yangu nashika, shairi nakutungia
Kamanda umeongea, kiwingu umeondoa
Hukutaka kusinzia,makosa kuyarudia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa


Mwananchi nimesoma, la jana nilinunua
Machoya yakatuama, dukuduku umetoa
Uliyosema Dodoma, Kwakweli yanavutia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa


Richmond kupasua, mapema uligundua
Kikwete ukamwambia, mkataba kuondoa
Rais akakataa, nini alitegemea?
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa


Nape akashikilia, lile asilolijua
Mikoani kaambaa, uzushi kang’ang’ania
Jinalo kulichafua, wewe ukavumilia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa


Mapema nilitabiri, falsafa nikapinga
Magamba sikukariri, kuvuana sikuunga
Ukweli niliukiri, mantiki iso kunga
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa


Beti sita nakomea, kalamu naweka chini
Mengi nimeongelea, soma tena kwa makini
Yatazidi kutokea,kusini kaskazini
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa.

View attachment 42198
 
Mpira uwanjani, yawezekana kumbe kuna gamba gumu zaidi na ambalo wengi hawakulijua ambalo kwa maelezo ya el lin tabia ya kuwa mbele ili watu wasilitilie shaka. el katoa jibu kazi kwa kamati ya maadili.
 
CCM wanacheza game ya kumrudisha EL kwenye chati. 2015 for presidency
 
CCM wanacheza game ya kumrudisha EL kwenye chati. 2015 for presidency

uko sahihi mkuu. wamesahau kuwa vimemo kutoka kwa huyohuyo vikienda kwa msbh vilianikwa wazi na kamati ya mwakye. watz wepesi kusahau sana.
 
Nimelipenda vina na mizani vimeenea. Nashauri utume gazetini walichape
 
Gamba no 1 ni jk si aabiwe tu.
Si afadhali lowasa kuliko jk amabaye is a dodging president. Jk kete za kucheza zinazidi kuisha angalia sana ******. Mareh nyerere alisema urais si lelemama kina jk hawakuamini wakaona yeyote anaweza. Sasa experiment ya urais kwa kutumia jk imetoa majibu!
Ni wazi sasa wenye vichwa vya panzi kama jk msitie mguu ni noma
 
Huu muda ulioupoteza kuuandika hili shairibubu kwa huyu kafiri aliyelisababishia taifa hili HASARA kubwa, ungeutumia kucheck na kusahihisha homework za vijana wako nngekuona wa maana sana.
 
kuioji watuhumiwa siyo kazi ya bunge.
Naelewa ndio maana nikatoa mikfano ya nchi za wenzetu walioanza huu utawala wa mihimili mitatu. wao kamati za bunge zinahoji watuhumiwa kulingana na kosa lililopo aidha kwa sababu ya wanataka kuelewa miaya iliyokuwepo wapate kutunga sheria ama kubadilisha vipengele ambavyo pengine vimepelekea kutokea kwa hali hiyo.

Na kama umefuatilia vizuri sehemu zote hizi bunge lao limekaza sheria ili jambo hilo lisitokee tena na kama kulikuwa na ubadhilifu wa kisheria iliyopo wakishtakiwa na serikali yeyyewe. Shell Bp wamepelekwa mahakamani na kutozwa faini kubwa kwa ile spill ya offshore. Lakini ilitanguliwa na kuitwa viongozi wake bungeni kujibu tuhuma za kwamba yaliyokoe yametokana na uzembe wa sherika hilo..

Kwa nini na sisi tuloiga mfumo huu tusiwe na utaratibu ambao bunge na kamati zake zinaweza kumwita mtuhumiwa yeyote kuja kujibu report iliyofanyiwa utafiti na serikali badala ya kuiacha hiyo report irudi kwa rais ambaye ndiye huchagua kifanyike kitu gani..Leo hii hatma ya RACHEL wote tunasubiri CCM waamue kama kwamba makosa aloyafanya yalikuwa ya kichama..

Kujivua gamba imekuwa swala la CCM kujivua gamba...hii kweli inaingia akiliini?
 
we uko nchi gani bwana...huyo rais gani atakaempeleka gerezani mwenzake katika tanzania hii???na asimalize muda wake wa katiba ipi hasa itakayomtoa madarakani?labda jeshi liasi,wabongo kwa kupenda ku create fear isiyokuwepo hatujambo,tuliambiana hapa oooh jk akishika madaraka mkapa atanyea debe!kiko wapi?kwa mfumo wa ccm ulivyo mwenyekiti ana nguvu nyingi sana kupita maelezo jk muoga tu mwenyewe au ana ajenda ya siri na huyo lowassa wake,lakini kumshughulikia hashindwi hata chembe,hata wale uv ccm hawajui tu kwamba kugombana na mwenyekiti wa ccm ni hatari sana kwao kama mwenyekiti angekuwa strong,anaweza kuuvunjilia mbali huo umoja wao kama alivyotishia juzi!ipo mifano huko nyuma na wala haitakua mara ya kwanza,ngoja tuwakumbushe nyie vijana!

CCM inaweza kufanya kama ilivyopata kufanya huko nyuma:

Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, UVCCM iliweka msimamo uliokuwa unachagiza wagombea vijana wapewe nafasi ya kuwania urais. Majina yaliyokuwa yakitajwa wakati huo ni pamoja na ya kina Kikwete na Lowassa, waliokuwa wakiungwa mkono na kina Anne Makinda na wengineo. Joto lilipozidi, uongozi wa juu wa UVCCM uliondolewa na hali ikabaki salama.
Baadhi ya waliokuwa katika uongozi wa UVCCM wakati huo ni pamoja na John Guninita ambaye leo ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam. Vijana wengine wa enzi hizo ni pamoja William Lukuvi ambaye sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu, Leonidas Gama ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Muhammed Seif Khatibu, John Henjewele na Said Mwambungu ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Aidha, wachambuzi hao wanasema hata ?kujivua gamba? kulikwishakufanyika ndani ya CCM japo kwa msamiati mwingine, lakini wenye maana karibu na huo.
?Mwaka 1984 walisema hali ya kisiasa ilikuwa imechafuka na kuchafuka huko kukaondoka na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi. Baadaye mkono huo wa CCM ukamfikia Maalim Seif Shariff Hamad na wenzake.
ni zamani siyo sasa na hali ya upinzani ilivyo.

unataka kutuaminisha kwa nguvu kwamba sasa hivi hali ya upinzani iko juu kuliko mwaka 1995 mrema na nccr yake walivyokuwa wanaitesa ccm?!!!!!!!mbona upinzani huu ni kama cha mtoto kwa ule wa 1995 ambapo kina Guninita walivuliwa gamba kwa kuwasupport kina kikwete!

 
Back
Top Bottom