Ni muda mrefu kidogo umepeta toka waziri mkuu wa kwanza wa awamu ya nne ndugu Edward Ngoyai Lowasa ajiuzulu wadhifa wake. Kila mara huwa najaribu kutafakari na kuwauliza watu mbalimbali kama kuna anayeweza kunifafanulia kosa la mkubwa yule. Nilimwamini sana na pia niliamini sana utendaji wake wa kazi, Hata hivyo hadi sasa imani yangu kwake haijapotea kabisa kwani kuna mambo yanayofanywa na serikali ambayo yananifanya niamini kuwa alikuwa mtu makini katika kutenda shughuli zake.
sina uwezo wa kumpamba sana ila naomba kama kweli alikosea kuileta kampuni ya Richmond/ Dowans, imekuwaje sasa kampuni hiyo ibadilishwe jina na kuja kuzinduliwa na Rais Mkuu wa Dunia?