Miezi miwili na ushee iliyopita mgombea huyu aliulizwa na wahariri wa magazeti iwapo atahama CCM kama haitamchagua kugombea urais mwaka huu. Jibu lake lilikuwa kwamba hatahama CCM kamwe kwa sababu ilimlea, na kwamba huyo ambaye hamtaki ndani ya CCM ndiye ahame chama hicho!
Hata hivyo, kabla mwezi haujakatika mgombea huyu akakihama chama hicho na kujiunga na chama cha Upinzani, na chama hicho kikamteua kugombea urais, na sasa kuna -vijana wanamshabikia! Kimsingi aliongopa katika jibu lake lile na taswira aliyojijengea ni ya mtu asiyeaminika katika kile anachosema.
Ingekuwa ni Wazungu au sisi watu wenye kufikiri sawasawa, tusingemshabikia -katika mbio zake za urais kwa sababu ni mtu mwongo, kigeugeu na asiyeaminika, mtu asiyeweza kusimamia maneno yake mwenyewe.
Lakini kwa uwezo wetu mdogo wa kufikiri, baadhi yetu- tunamzawadia mgombea huyo kwa kumuunga mkono kwenye kampeni yake ya kuusaka urais kwa udi na uvumba!
Uongo na ukigeugeu kama huo pengine ungevumilika kama nafasi yenyewe anayowania si urais. Lakini urais ni kazi yenye heshima, utukufu, uadilifu nk. Ni kazi ambayo haimfai mtu mwongo na asiyesimamia maneno yake mwenyewe.
Vijana wetu hawajiulizi, kama huyu alidiriki kutudanganya jana, kwa nini asiendelee kutudanganya hata leo au hata baada ya kuingia Ikulu.
Tutamwamini vipi katika hayo anayodai kuwa atatutendea akiingia Ikulu kama huko nyuma aliwahi kutudanganya kwa kushindwa kusimamia maneno yake mwenyewe? TAFAKARI: