Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Sikuona jipya kwenye maelezo yake kamwe hajakidhi kiu ya waliokuwa wanamsikiliza kaeleza yale yasiokuwa ya msingi nakuzua maswali mengi kuliko majibu.

Ametilia mkazo katika kuvitisha vyombo vya habari akasahau kuwa katika enzi za wanamtandao yeye pamoja na maswahiba wake ndio walikuwa magwiji wakununua magazeti na vyombo vya habari halafu wakaanza kuwachafua maasmu wao wakisiasa leo hii mchimba kisima kaingia mwenyewe! Nani amtoe RA au JK wanamtandao wenzie.

Ama kweli leo ndio nimeamini mkuki kwa nguruwe ni sponji lakini kwa binadamu ni chuma tena chenye ncha kali.

Mzee wetu Salim A Salim yaangalie manyangau sasa yanatiana vidole machoni walana wao kwa wao kumbe malipo ni hapahapa duniani na bado tutashuhudia mengi
 
hahahahaha....... No comment bora umetoa kilichopo moyoni japo wengi wao hawaoniiii kula na kipofu ucmshike mkono babu...... Jambo uclilolijua ni ucku wa giza lowasa hamjui ila mnalazimisha kumjua
 
Sikuona jipya kwenye maelezo yake kamwe hajakidhi kiu ya waliokuwa wanamsikiliza kaeleza yale yasiokuwa ya msingi nakuzua maswali mengi kuliko majibu.

Ametilia mkazo katika kuvitisha vyombo vya habari akasahau kuwa katika enzi za wanamtandao yeye pamoja na maswahiba wake ndio walikuwa magwiji wakununua magazeti na vyombo vya habari halafu wakaanza kuwachafua maasmu wao wakisiasa leo hii mchimba kisima kaingia mwenyewe! Nani amtoe RA au JK wanamtandao wenzie.

Ama kweli leo ndio nimeamini mkuki kwa nguruwe ni sponji lakini kwa binadamu ni chuma tena chenye ncha kali.

Mzee wetu Salim A Salim yaangalie manyangau sasa yanatiana vidole machoni walana wao kwa wao kumbe malipo ni hapahapa duniani na bado tutashuhudia mengi

Cha Msingi, angesema ya Kwake Moyoni sasa hivi bado mapema maana akisubiri mpaka wakati muafaka anaousema yeye na wanyoosheane vidole na kuchafuana zaidi na zaidi atakuwa too late, na hakutakuwa na mtu au watanzania wa kumsikiliza na kumuamini.
Hii Movie ni tamu, sijui nani atabaki, Kazi Kweli Kweli
 
Binafsi naona anasafisha njia kugombea uraisi 2015.

Ingekuwa Jema kwake na kwa Watanzania kama anataka kujinyooshea njia yeye ya Urais 2015 kwa kusema Ukweli, Watanzania wa leo sio wa Miaka ya nyuma, Watanzania wa leo wana mwamko na uelewa wa mambo. Hoja ni Moja tu Ajibu Issue muhimu zilizoelekezwa kwake ikiwa bado mapema kabla mambo hayajaharibika, maana tutamuuliza ulikuwa wapi muda wote huo mpaka ukasubiri dakika ya mwisho, na tulikuwa na kiu ya kujua mapema ????
 
Ndugu Lowasa sipendi kuukosoa uamuzi wako ulioamua kuutoa kwa wanahabari, lakini nachelea kutoitendea haki nafsi yangu kama sitakuhoji hili,
Ikumbukwe hapo juzi tu kwa utashi wako na kwa kujiamini uliiweka jamii wazi kwamba utauweka wazi mustakabali mzima juu ya mkataba feki wa Richmond na dadaye Dowans, pia ulitanabaisha kuueleza uma ukweli na ni ukweli kabisa unaoufahamu juu ya yote hayo.
Sasa mkuu huoni kama ulichozungumzia siku ile ni mengineyo? Ukaacha ajenda kuu ambazo ulizitangaza mwenyewe?
Tukueleweje bw Lowasa?
ulinyamazishwa, ulikatazwa, uliombwa, ulionywa au tuelewe lipi mkuu!
yaseme kabla muda haujakuishia ndugu.
 
tuelewe kwamba ni kigeugeu, kwa mtindo huu wasanii wapo wengi kwenye chama cha magamba!
 
Hakuna tofauti kati ya aliyosema Millya na haya ya Lowasa, hii ina maana gani?

Kazi ipo kwa Nape na asome alama za Nyakati, sijui Kikwete vipi hapa tena?
 
Ndugu Lowasa sipendi kuukosoa uamuzi wako ulioamua kuutoa kwa wanahabari, lakini nachelea kutoitendea haki nafsi yangu kama sitakuhoji hili,
Ikumbukwe hapo juzi tu kwa utashi wako na kwa kujiamini uliiweka jamii wazi kwamba utauweka wazi mustakabali mzima juu ya mkataba feki wa Richmond na dadaye Dowans, pia ulitanabaisha kuueleza uma ukweli na ni ukweli kabisa unaoufahamu juu ya yote hayo.
Sasa mkuu huoni kama ulichozungumzia siku ile ni mengineyo? Ukaacha ajenda kuu ambazo ulizitangaza mwenyewe?
Tukueleweje bw Lowasa?
ulinyamazishwa, ulikatazwa, uliombwa, ulionywa au tuelewe lipi mkuu!
yaseme kabla muda haujakuishia ndugu.

either he is a liar, or he is a coward!!
 
mie sikuona cha maana ktk hotuba yake.......kweli anayeua kwa upanga naye hufa kwa upanga
 
Amebakiza jina moja tu tz,rais wa jamhuri ya muungano,na mkewe aitwe first lady ndicho wanachopigania
 
Kwani Lowasa alipewa nafasi hiyo ya kuleta ujumbe wake kwa umma kama nani?
 
this silver hair hana maana badala ya kuzungumzia suala la richmond lililomtoa kwenye ofis anapiga porojo za kujikampenia urais 2015. hii inadhihrisha jinsi gani afai kuwa presidaa 2015. coz nina uhakika akiruhusiwa tutakua na richmond nying na umaskini kuzidi, its time for him to stay quite an ale pensheni ya uPM na sio kukimbilia kijiti asichokiweza
 
Yaani amewaita wanahabari hadi Monduli kuwaambia atawachukulia hatua wakimwandika vibaya? Kama ni mtu wa principle yeye kimya kimya angekuwa anakwenda mahakamani dhidi yao, badala ya kuwaita na kuwatangazia kwanza. Angekuwa anafanya kama vile wafanyavyo akina Rostam, Manji, Mengi na wengine.

EL anakuwa kama Mtikila au Mrema siku hizi -- wanasema wanakwenda mahakamani halafu kimya!!. Mwenye nia ya kwenda mahakamani hufanya hivyo bila ya kutangaza, unatangaza ya nini?
 
mimi nachangia katika masuala yafuatayo:

Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge na mtu aliyepata kuwa Waziri Mkuu ninatambua na kuiheshimu kwa dhati kazi hiyo kubwa inayofanywa kwa weledi mkubwa na taasisi mbalimbali za dola zenye wajibu wa kuhakikisha ulinzi na usalama wa viongozi wetu na taifa kwa ujumla....

Mchango wangu: ndugu yetu lowasa hivi kweli kwa akili zako na uzoefu na upeo wako unaweza kuthubutu kusema taasisi za dola zinafanya kazi kwa weledi mkubwa,. ni weledi gani ulitumika katika kuzuia ajali ya MV Spice (huko Zanzibar) na baada ya ajali kutokea kwenda kuokoa wananchi na ndugu zetu zanzibar. Hivi ni weledi gani unatumiwa na polisi katika kukabiliana na vitendo vya ujambazi. ni weledi gani unatumiwa na vyombo vyetu, mtu unaenda kutoa taarifa ya tukio la jinai, polisi anakudai kwanza rushwa. ni weledi gani unatumika polisi wanaua watu hovyo kwenye migodi (ref. issue ya mkoa wa Mara). Ni weledi gani umetumiwa na TAKUKURU kushughulikia vitendo vya rushwa hasa kagoda. Ni weledi gani umetumiwa na DPP kufikisha mapapa wa rushwa mahakamani ikiwemo kagoda. Ni weledi gani unatumiwa na vyombo vya dola katika kutokomeza bidhaa feki!! mbona usalama wa taifa umekuwa legelege kulinganisha na kipindi cha Mwl baba wa taifa. Mbona vyombo vya dola pamoja na taasisi za serikali zinashindwa kuwashughulikia wafanyakazi wa ardhi na kutoa upendeleo kwa viongozi na watu wenye uwezo katika upatikanaji wa ardhi. Mbona vyombo vya dola vinashindwa kuchukua hatua muafaka kwa halmashauri zinazofuja fedha za umma-- (ref: habari ya Mrema alivyokuwa anasema jana kwenye taarifa ya habari kuhusu ufisadi katika halmashauri na watu hawachukuliwi hatua za maana)

"Ndugu wanahabari nazungumza nanyi baada ya kurejea nikitokea katika nchi za
Nigeria, Malaysia, Singapore, India, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ambako nilipata fursa ya kujifunza mambo mengi lakini moja muhimu likiwa ni namna vyombo vya habari (kwa maana ya waandishi wa habari) na wanasiasa wanavyotumia muda wao mwingi kujadili masuala yanayogusa maisha na maendeleo ya watu wao.".....

Mchango wangu: huwezi kuzugumzia maendeleo ya watu kama nchi imetawaliwa na rushwa. utapataje maendeleo wakati tunatakiwa tuwazawadie dowans USD 94 millions, tutapataje maendeleo kama Kagonda aliyetuibia zaidi ya billion 40 amesamehewa. tutaachaje kujadili watu kama, watu hawachukui maamuzi magumu (kama ulivyoyaita).

nakuomba ndugu lowasa uache unafiki, sisi watanzania tumeelimika na hatudanganyiki ng'0.
 
Sasa huyu gamba EL mbona kama anjichanganya. yeye ameanza kuwalaumu waandishi wa habari lakini baadaye anawalumu zaidi viongozi wenzake wa ccm wanaomchafua yeye kwa njia moja au nyingine.

Habari kwamba kuna waasi au kundi la wana ccm wanataka kumhujumu kj mwakani asichaguliwe kuwa m/kiti zilisemwa na kada wa ccm nape tena mchana kweupe, na waandishi wakaripoti kama nape alivosema.
Sasa hapo EL kwa akili ya kawaida tu wa kulaumiwa ni nani kati ya nape na waandishi wa habari
 
Mimi kwa upeo wangu huwa najaribu kuchunguza kwa kina makosa ya lowasa katika uongozi lakini bado sijawahi kuona kosa kubwa ambalo linawazidi wengine maana kuna wenye makosa makubwa zaidi katika uongozi na bado wapo madarakani
Pia nimekuwa nikijaribu kufuatilia ufisadi wake kwa kweli ushahidi kamili hamna!! Hela alizonazo na mali ni za kawaida sana kwa mtu ambaye amefanya kazi sehemu nyeti za serikali kama yeye kwa muda mrefu namna hiyo ukilinganisha na wenzake
Lingine ni kwamba siyo siri Tanzania tumepoteza mwelekeo siku nyingi na kama tukiendelea hivi hatutakaa tuwe na maendeleo yetu wenyewe..... Bunge linatumia muda mrefu sana kufuatilia na kujadili nani kaiba nini au fulani ana mali gani badala ya kujadili matatizo ya wananchi.
Western country wanapokuja kuomba tenda nchini ukiwa mzalendo nawe umeomba hiyo tenda hua wanahonga waandishi ili uanze kuchafuliwa kuwa fedha na uwezo wako ni wa kifisadi and atlast mikataba ya uwekezaji wanapewa wageni na wazalendo walio na hela za kuwekeza nchini kwetu zinaozea kwenye mabank ya nchi za nje maana tanzania hamtaki kuwapa fursa za kuwekeza nyumabni....wakati umefika ndugu zangu tuwabebe wazalendo wawekeze mali zao ndani ya nchi ili kukuza ajira kwa vijana wetu na kuongeza mzunguko wa hela yetu.
Mwisho mzee lowasa kashastaafu uwaziri mkuu tumwache apumzike kwa amani na tutafute namna ya kumaliza matatizo yetu ya uchumi na si kelele za ufisadi kila siku.
 
Back
Top Bottom