Elections 2015 Lowassa: Sina pesa, hizi nachangiwa na marafiki zangu

Elections 2015 Lowassa: Sina pesa, hizi nachangiwa na marafiki zangu

Kila anapochangia...anasema yeye hana pesa ila amechangiwa na marafiki zake.Haya huwa anayazungumza anapokuwa anatoa mchango wake wa fedha nyingi sana kwenye vikundi.

Watanzania hizo ni pesa zenu ambazo zilikuwa zimeibiwa sasa zinarudi na ninacho waomba mzipokee kwa mikono miwili lakini mnajua wp mtatoa kura yenu lakini kama mtaafanya makosa kumpa kura mtu ambaye ameleta pesa kwenu ila apate kura madhala yake ni makubwa sana.

Wafanya biashara ni marafiki zake na hao ndio wanao pambana kumweka madarakani je atawalipa nini akishakuwa rais?
Nangojea kwa hamu kubwa sana atapoanza kulipa marupu rupu ya hao wafanyabiashara na matajiri wake ( watu wake) , hakika wa TZ tutalia na kusaga meno.
 
Mburaa!! hebu afanye uungwana kidogo tu atupe listi ya marafiki zake tukaangalie records zao pale TRA :whistle:

Wakati Mheshimiwa Samweli Sita alipotoa Mchango kanisani, Aliwataja waliomchangia bila kuficha. La kushangaza Mheshimiwa Edward Lowasa Kila anapochangia huwa anasema ni fedha toka kwa Marafiki. Serikali na makanisa/misikiti inaaminije kuwa hizi si pesa chafu?

Tunakumbuka jinsi serikali ilivyombana Wakili maarufu Median Mwale na hela zake chafu. Je, Serikali imefanya nini kujua kuwa hela anazochangiwa lowasa huwa hachangiwi na mafisadi, majangili na/au wauza madawa?

Ushauri kwa lowasa, "uwe unataja waliokuchangia kama alivyofanya Samuel Sitta"
 
Anachangiwa halafu atawalipaje??hili ndilo swali lililo bahind the scene'


Pia nini hasa nia ya hao marafiki zake kumchangia?
Ni vema sasa tukamshinikiza awataje hao marafiki zake, waliko na kiasi cha pesa wanachomchangia.......!
 
Labda ni WALIBERALI WANAMPA HUKO
UJERUMANI ANAKOENDA BAADA YA MIEZI 6!

Lowassa kuwa muwazi kwasababu kuna siku tutakutaka utuonyeshe hao marafiki zako wamekuchangia kupitia account gani na lini na wanatoka wapi na kwa kusudi gani, na utazirudishaje hela zao hapo mbeleni.

Wazo Langu Kwako
Usinunue Mbeleko Mke Hajazaa, maana unaweza kununua mbeleko ikawa mtoto si riziki. Pia kuna mimba za miaka mitatu siku hizi usiwe na haraka.

Mwisho ni kwamba watu wanazitaka hela zako na maumivu yao ya RICHMOND bado wanayapata.
.
 
Nerere Huko aliko Mungu amrehemu aliona mbali sana.
 
anao uwezo wa kushawishi watu wakaona tatizo wakachanga kidogo walichonacho, hata wakati Kikwete anagombea urais mwaka 2005, Lowasa pale Arusha aliwashawishi marafiki zake wakamchangia Sh milioni miatatu (M 300). Mnalikumbuka hili? kama aliweza kufanya hivyo kwa wakati ule kwa nini leo akiongoza mchango wa nyumba za ibada, au mchango wa kupunguza umaskini wewe unamwonea wivu? na wewe buni mpango wako utushawishi ili tukuunge mkono. "Acha wivu wa kike" (Msekwa, 2003)

Umesema kweli,ukiwa na watu hao ndo wenzio hata ukipata shida au jambo la heri watakuwa nawe.....
 
Wakati Mheshimiwa Samweli Sita alipotoa Mchango kanisani, Aliwataja waliomchangia bila kuficha. La kushangaza Mheshimiwa Edward Lowasa Kila anapochangia huwa anasema ni fedha toka kwa Marafiki. Serikali na makanisa/misikiti inaaminije kuwa hizi si pesa chafu?

Tunakumbuka jinsi serikali ilivyombana Wakili maarufu Median Mwale na hela zake chafu. Je, Serikali imefanya nini kujua kuwa hela anazochangiwa lowasa huwa hachangiwi na mafisadi, majangili na/au wauza madawa?

Ushauri kwa lowasa, "uwe unataja waliokuchangia kama alivyofanya Samuel Sitta"

Lakini si unakumbuka jinsi Mr Alcohol Padlocks alivyokanudha kushirikiana na mr Six?. Wengine wanapenda wanapotoa sadaka zao iwe ni siri yao na Mungu wao, kwa hiyo wanamkataza mjumbe waliemtuma asiwataje hadharani.
 
hizo pesa ni za kwake. anaogopa akisema zake mtamuliza katoa wap.
hili swali lipo siku nyingi na aliliuliza Mwalimu na mpaka leo halijajibiwa. Anachosahau ni kuwa mpaka pale litakapokuwa limejibiwa ndipo tu wenye akili timamu watamuelewa
 
Hizi alpha alpha zina uhusiano naye!! Nilifunga mdomo ila nimekumbushia tu

:lalala:
 
Sheikh Fisadi Lowassa tupe list ya majina ya huo mtandao wako mwenyewe unawaita "marafiki" na kiasi kilichochangwa na kila mmoja wa hao "marafiki zako". Kisha tueleze imekuwaje miaka yote uliyokuwa madarakani hawakuwahi kukuchangia hata senti hadi miaka michache kabla ya kinyang'anyiro cha kugombea Urais 2015.
 
Lowasa wataje kwa majina yao hao rafiki zako wanaokuchangia kisha nijibu maswali yafuatayo:-
!.Kwa nini wanakuchangia wewe badala ya wao kuwachangia wananchi kwenye shughuli za maendeleo?
2.Hizi hela utawarudushiaje,au wanakupa bure?
3.Au 10% ya Richmond ndiyo rafiki zako?

Wewe Lowasa ni mtu hatari sana,huna upendo wowote kwa wananchi lia unawalazimisha hao matajiri wakupe hela hizo ili utoe rushwa kwa wananchi kwa njia ya harambee ili wakuchague kuwa rais 2015 na ndipo uwarudishie matajiri hela zao kwa kuwapa tenda kubwa serikalini kama za Richmond.
Kwa taarifa yako urais hutaupata na usiwafanye watanzania wajinga maana lengo lako ni kuiweka nchi mikononi mwa wenye hela.
Kwa taarifa yenu,ninyi mnaoitwa takukuru,harambee anazofanya Lowasa makanisani na sasa kwa wamachinga ni RUSHWA.Mkamateni na mwulizeni hizo hela kapata wapi?
 
Kila anapochangia...anasema yeye hana pesa ila amechangiwa na marafiki zake.Haya huwa anayazungumza anapokuwa anatoa mchango wake wa fedha nyingi sana kwenye vikundi.

Watanzania hizo ni pesa zenu ambazo zilikuwa zimeibiwa sasa zinarudi na ninacho waomba mzipokee kwa mikono miwili lakini mnajua wp mtatoa kura yenu lakini kama mtaafanya makosa kumpa kura mtu ambaye ameleta pesa kwenu ila apate kura madhala yake ni makubwa sana.

Wafanya biashara ni marafiki zake na hao ndio wanao pambana kumweka madarakani je atawalipa nini akishakuwa rais?

Kama ni mkweli awataje hao marafiki zake wanaomsaidia kumwaga hizo pesa kwa watu, ili tujue kuwa ni fedha za mafisadi ama la. Na pia tujiulize hao marafiki zake ambao wanampa hizo pesa na bila shaka ni wafanyabiashara watazirudisha vipi hizo fedha? maana nijuavyo hakuna mfanyabiashara wa kweli na halali anayetoa fedha yake bila kutegemea faida.

Nataka Lowasa ajue kuwa walitupata huko nyuma lakini sasa hatudanganyiki.
 
Lowasa mwizi kama wezi wengine.Yeye narafiki yake karamagi walimchangia kikwete ili awe raisi.Haya maisha magumu yanayotukumba sasa watanzania,yeye anahusika
 
Watanzania mnakumbuka mwl jk nyerere alishawakataa jeikei na roho hasa! Mambo ya jeikei mnayaona maisha yamekuwa magumu zaidi ya maelezo haya akiingia leigwanani naye akusanye mabilioni aliyoyatoa si itakuwa balaa!
 
wakati mheshimiwa samweli sita alipotoa mchango kanisani, aliwataja waliomchangia bila kuficha. La kushangaza mheshimiwa edward lowasa kila anapochangia huwa anasema ni fedha toka kwa marafiki. Serikali na makanisa/misikiti inaaminije kuwa hizi si pesa chafu?

Tunakumbuka jinsi serikali ilivyombana wakili maarufu median mwale na hela zake chafu. Je, serikali imefanya nini kujua kuwa hela anazochangiwa lowasa huwa hachangiwi na mafisadi, majangili na/au wauza madawa?

Ushauri kwa lowasa, "uwe unataja waliokuchangia kama alivyofanya samuel sitta"


pesa chafu unazijua ,,inawezekana hata wewe mshahara wako ni pesa chafu,,,kuna watu wanafanya kazi kwenye hotel kubwa,,,na mishahara wanayolipwa baadhi inatokana na na watu kufanya mapenzi kinyume na maumbile,,,ukisema pesa chafu unakosea sana,,,,mi namkubali sana lowasa maana faida ya michango yake ni direct and not indirect
 
Hao marafiki wanamchangia hayo mamilioni ya pesa kwa malengo/matarajio gani. Kama ni kwa ajili ya kwenda kutoa kwenye makanisa na misikiti kwa nini hao anao dai ni marafiki zake wasipeleke hiyo michango wao wenyewe. Na kwa nini nguvu zake zote ameelekeza kwenye misikiti na makanisa na sio maeneo mengine kama elimu, maji na afya.

Mara nyingi michango yake anatoa pesa taslimu zikiwa kwenye bahasha ya khaki, hii inaonesha wazi kuwa pesa zake haweki benki na hii ni moja ya viashiria vya pesa chafu zinazopatikana ama kutengenezwa kwa njia haramu.

Huyu mtu ni mchafu kuanzia yeye binafsi, waliomzunguka na rasilimali zake zote na hawezi kutakata hata akijimwagia sabuni/dawa gani
 
namkubali sana lowasa na pesa zake zinaupako,,,,,maana matunda yake yanaonekana wazi bila kubaguwa dini, chama,,kabila,,mkoa, wilaya wala jimbo ,,tofauti kabisa na manyangumi wengine ambao pesa zao ni kwaajili yawatu wa jimbo lake tu,,hiyo yote ni kwaajili yakuaandaa mazingira yakutokosa kura wakati wa uchaguzi,,,,2015 mpaka kieleweke
 
Back
Top Bottom