Elections 2015 Lowassa: Sina pesa, hizi nachangiwa na marafiki zangu

Elections 2015 Lowassa: Sina pesa, hizi nachangiwa na marafiki zangu

Kila anapochangia...anasema yeye hana pesa ila amechangiwa na marafiki zake.Haya huwa anayazungumza anapokuwa anatoa mchango wake wa fedha nyingi sana kwenye vikundi.

Watanzania hizo ni pesa zenu ambazo zilikuwa zimeibiwa sasa zinarudi na ninacho waomba mzipokee kwa mikono miwili lakini mnajua wp mtatoa kura yenu lakini kama mtaafanya makosa kumpa kura mtu ambaye ameleta pesa kwenu ila apate kura madhala yake ni makubwa sana.

Wafanya biashara ni marafiki zake na hao ndio wanao pambana kumweka madarakani je atawalipa nini akishakuwa rais?

Ipe mda hiyo mkuu. Ngoma bado mbichi sana.
Tutalijadili baadae ila kwa sasa wacha mda uchukue mkondo wake.
 
mpe mda mkuu.
let time take its course. Kwa sasa its kinda too early to judge and comment hizi harakati.
 
Ushauri kwa mh lowasa. Ili kukata mzizi wa fitina kwamba unachangia harambee ili upate kuungwa mkono katika mbio za urais, basi 2015 usichukue form kabisa. Utakuwa umewajibu vizuri wote wanaokuzushia mambo. Ukichukua form tu umekwisha mwanawane.
 
Anachangiwa halafu atawalipaje??hili ndilo swali lililo bahind the scene'
Ni swali gumu lakini lina maana sana , na hasa ukizingatia kiasi ambacho mpaka sasa keshachangiwa na kesha kitumia kusaidia jamii. Ila mimi siamini kama anataka kuwa rais maana hajasema hata siku moja ila naona anafanya bidii kutekeleza ilani ya chama chake kimatendo kwa kuyaendeleza makundi mbalimbali. Na kama akifanikiwa kiasi hiki nadhani anampa nafasi pia mgombea wa chama chake atakayewekwa 2015 kutumia michango ya mwanachama mwenzake kujipigia debe. Kumbe nadhani haya yote yana baraka toka chama chake, yeye badala ya kuzunguka na kupiga porojo kama za akina Nape, anafanya kwa vitendo, mie nampongeza sana. Inafaa ccm wengine waige moyo huu wa kujitoa na kujisahau kwaajili ya wengine. Nakumbuka kuna wakati nilikuwa Monduli, alitoa mbuzi na ng'ombe tukala nyama choma na mamorani. Ok, acha niendelee kubeba mabox ,nilipita kidogo kuchungulia.
 
Lowasa nakushauri ushughulike na Afya yako zaidi kuliko Urais, maana utakufa siku sio zako, Urais hupati na Ugonjwa unakutesa.Bora upumzike.
 
Akienda kwa wamachinga anawapiga propaganda tu ............. kwa nini asiwambie marafiki zake wawachangie wamachinga 500 kila week ili wapate mitaji badala ya kuzipeleka makanisani kila siku ambako wauumini wanachangia kwa sadaka zao kila week!!
Huyu ni strategic. Kwa wamachinga Mwanza na pia kule Moshi kwa waalimu anatanguliza Milioni 20 za kuandaa harambee na anweka Kamati ya maandalizi. Anatoa ahadi Harambee hiyo itatoa bilioni moja! Kwa hiyo anawaacha wakitarajia kupata hizo bilioni...
 
Sasa kama hana pesa anamtangazia nani au ni kujishuku kwa kugundulika ujanja wake, hana lolote anajisumbua tuu hawezi kuwa Rais wa nchii hii pamoja na tamaa yake ya Urais iliyopitiliza hadi kumwa damu ya raia wasio na hatia na kutaka kuwaua viongozi wa upinzani.
 
Kila anapochangia...anasema yeye hana pesa ila amechangiwa na marafiki zake.Haya huwa anayazungumza anapokuwa anatoa mchango wake wa fedha nyingi sana kwenye vikundi.

Watanzania hizo ni pesa zenu ambazo zilikuwa zimeibiwa sasa zinarudi na ninacho waomba mzipokee kwa mikono miwili lakini mnajua wp mtatoa kura yenu lakini kama mtaafanya makosa kumpa kura mtu ambaye ameleta pesa kwenu ila apate kura madhala yake ni makubwa sana.

Wafanya biashara ni marafiki zake na hao ndio wanao pambana kumweka madarakani je atawalipa nini akishakuwa rais?

Tunachojua kama watanzania ni kwamba ccm wote ni mafisadi. suluhisho ni CDM tu basi. haya ni makubaliano ya kudumu
 
Ushauri kwa mh lowasa. Ili kukata mzizi wa fitina kwamba unachangia harambee ili upate kuungwa mkono katika mbio za urais, basi 2015 usichukue form kabisa. Utakuwa umewajibu vizuri wote wanaokuzushia mambo. Ukichukua form tu umekwisha mwanawane.

Ha ha ha aitakaa itokee wapambe wake awalali kazi yao nikumpamba mzee mpaka eti aingie ikulu
 
Pema pasijapo pema paki pema si pema tenaaaa so muda wa utawala wa ccm bado.......co jipangee and deal na KATIBA now
 
Najua kuna watu makini hapa jamvini wanaweza kutupatia hesabu kamili ya mapesa aliyachangia mpaka sasa.
Kwa wepesi wetu wa kusahau tunaweza kujikuta tunampa nafasi ya uongozi wa juu kabisa hapa Nchini huyu jamaa.
Ni vizuri tukafahamu kuwa kama tutafanya hivyo basi kwa mara ya kwanza tutakuwa tumepata Rais ambaye Urais wake utakuwa na Wabia ambao anawataja kila siku kwa jina la "Rafiki zangu" Haiwezekani watu wamchangie mamilioni yote yale apate Urais halafu atawale peke yake!
 
Ikulu kuna biashara gani hata mtu akope na akalipe akishaingia ikulu?
Ikulu ni mahali patakatifu............................
 
kila anapochangia...anasema yeye hana pesa ila amechangiwa na marafiki zake.haya huwa anayazungumza anapokuwa anatoa mchango wake wa fedha nyingi sana kwenye vikundi.

Watanzania hizo ni pesa zenu ambazo zilikuwa zimeibiwa sasa zinarudi na ninacho waomba mzipokee kwa mikono miwili lakini mnajua wp mtatoa kura yenu lakini kama mtaafanya makosa kumpa kura mtu ambaye ameleta pesa kwenu ila apate kura madhala yake ni makubwa sana.

Wafanya biashara ni marafiki zake na hao ndio wanao pambana kumweka madarakani je atawalipa nini akishakuwa rais?

kwa kauli ya baba wa taifa mtu anayeisaka ikulu kwa kutumia pesa anapashwa 'aogopwe kama ukoma'!!
 
Kuna mtu mmoja alitoa kauli zifuatazo.......
> Ikulu pana kitu gani hata watu wapakimbilie..?
> Ikulu ni mahali patakatifu...
> Ukiona mtu anakimbilia Ikulu kwa kutumia pesa mwogope kama ukoma.
> Akisema mimi nafaaa kuwa rais...muulize wewe unasema au wananchi wanakutaka?!
> Ikulu si mahali pa kukimbilia
> Je kama watamwingiza kwa pesa atazilipaje?
> Kama mtu una akili afu mtu akakueleza mambo ya kijinga nawe ukakubali atakudharau kwelikweli!
> Mwenye Masikio na Asikie
 
Lowassa ni Mtu hatari sana, inasikitisha ni kwa kiasi gani watanzania hawamuenzi baba wa taifa maana alishamkataa gaidi huyu!!! Ok kama hilo haliwezekani basi ifike wakati tumtake huyu jamaa atuambie ni nani hao marafiki zake, maana mapesa yote haya anayopewa na marafiki zake atayalipaje atakapoingia ikulu???????????????

Kila anapochangia...anasema yeye hana pesa ila amechangiwa na marafiki zake.Haya huwa anayazungumza anapokuwa anatoa mchango wake wa fedha nyingi sana kwenye vikundi.

Watanzania hizo ni pesa zenu ambazo zilikuwa zimeibiwa sasa zinarudi na ninacho waomba mzipokee kwa mikono miwili lakini mnajua wp mtatoa kura yenu lakini kama mtaafanya makosa kumpa kura mtu ambaye ameleta pesa kwenu ila apate kura madhala yake ni makubwa sana.

Wafanya biashara ni marafiki zake na hao ndio wanao pambana kumweka madarakani je atawalipa nini akishakuwa rais?
 
Ya kaisari mpe kaisari..ya mungu mpe mungu..unafikiri wachungaji na masheeh zote wanapeleka kanisani? Subutu
 
Mburaa!! hebu afanye uungwana kidogo tu atupe listi ya marafiki zake tukaangalie records zao pale TRA :whistle:

Ahahaha, hii safi sana, inawezekana wakawa na fedha chafu, kwa nini wajifiche, awataje?
 
Mimi nakerwa na maeneo fedha hizo zinakorudishwa.makanisa na misikiti kujengwa na fedha haramu,hii ni fedheha kubwa kwa waumini wa Tanzania.kabla ya kusafisha serikali,tuanze kusafisha nyumba zetu za ibada kwa kuondoa viongozi wa dini wenye ubia na mashetani otherwise mtaabudu mashetani mkidhani mnaabudu Mungu.
 
Mnakumbuka kauli hii ''nimeonewa sana,Nimedhalilishwa kama haya ni kwa ajili ya cheo cha Uwaziri Mkuu basi naachia ngazi.Je hawa aliowalalamikia kumdhalilisha siku kaukwaa Urais itakuwaje?.
 
Back
Top Bottom