Elections 2015 Lowassa: Sina pesa, hizi nachangiwa na marafiki zangu

Elections 2015 Lowassa: Sina pesa, hizi nachangiwa na marafiki zangu

ndugu wana-jamvi.

ninaomba kwa ishma na taadhima nidadis kidogo ili kupata kujuwa, japo kiduchu. huyu mzee hana biashara yoyote ambayo ni reputable, namaanisha hana kiwanda, hana vitega-uchumi vinavyotambulikana na kila mtu kama vile:

Bwana Yusuph Manji (Quality Group)
Bwana Reginald Mengi (IPP, Bonite)
Bwana SSB 'Bakhressa' (AZAM)
Mohamed Dewji (MeTL)

hao niliowataja hapo juu nikisikia 'ametoa milioni mia moja kwa kikundi fulani au kwenye harambee' sipatwi na shaka yoyote kwa sababu wana biashara zinazoeleweka. asa huyu mtu anayeitwa waziri mkuu mstaafu anapata wapi hayo mahela?

kama mTanzania nina nia, sababu na uwezo wa kujua.
 
Sumae ana majibu juu ya swali lako kwani kuna kauli aliitoa hivi karibuni nafikiri inalijibu swali lako vizuri sana.
 
anapata kwa marafiki zake......hao marafiki ndio wanampa hizo pesa........
 
anapata kwa marafiki zake......hao marafiki ndio wanampa hizo pesa........

na hao marafiki zake wanamsaidia ili waje walipwe nini?. Wao kama kutoa misaada makanisani wameshindwa? Mbona walengwa wa misaada hiyo ni wale wenye uwezo wa kupiga kura ama wenye ushawishi kwa wapiga kura. Mbona hatumuoni akitoa misbda kwa ombaomba/ yatima walemavu nk?
 
nilijua Pasco utajitokeza. em funguka kidogo kuhusu miradi ya bosi wako. miradi yenye hadhi ya nyota 5 a.k.a 'Reputable'

siyo miradi ili mradi tu
 
Last edited by a moderator:
ndugu wana-jamvi.

ninaomba kwa ishma na taadhima nidadis kidogo ili kupata kujuwa, japo kiduchu. huyu mzee hana biashara yoyote ambayo ni reputable, namaanisha hana kiwanda, hana vitega-uchumi vinavyotambulikana na kila mtu kama vile:

Bwana Yusuph Manji (Quality Group)
Bwana Reginald Mengi (IPP, Bonite)
Bwana SSB 'Bakhressa' (AZAM)
Mohamed Dewji (MeTL)

hao niliowataja hapo juu nikisikia 'ametoa milioni mia moja kwa kikundi fulani au kwenye harambee' sipatwi na shaka yoyote kwa sababu wana biashara zinazoeleweka. asa huyu mtu anayeitwa waziri mkuu mstaafu anapata wapi hayo mahela?

kama mTanzania nina nia, sababu na uwezo wa kujua.

Mkuu Ongwise, no wonder umejiunga jf tangu 2010 na kupost zaidi ya mara 300, ila hukuwahi kupewa thanks hata moja, hiyo moja unayoiona .ni yangu , mimi ndio nimekupatia!.

Kiukweli kuna watu humu wanawashwa sana na majina fulani fulani hadi inakuwa kama "mania!". Kila anapotoa fedha huwa anasema wazi hizo fedha kazitoa wapi!.

The man is talented in mass mobilization. Akiendesha harambee tuu watu wanajitoa kuchangia! hii inamaanisha akiwa!, Watanzania watajitoa kujiletea maendeleo!, kinyume cha hali ilivyo sasa watu wanasubiri waletewe maendeleo kama ilivyo tabia za watu wa Pwani, umwinyi umwinyi!. Kaskazi ni kazi tuu!.
 
nilijua Pasco utajitokeza. em funguka kidogo kuhusu miradi ya bosi wako. miradi yenye hadhi ya nyota 5 a.k.a 'Reputable'

siyo miradi ili mradi tu
Pasco lazima ajitokeza kwa sababu Lowasa alimsaidia sana siku alipopata matizo ughaibuni. Lowasa ana miradi mingi (overt and covert) yenye kuchurn out pesa nyingi kuliko hao uliowataja kwa pamoja
 
nilijua Pasco utajitokeza. em funguka kidogo kuhusu miradi ya bosi wako. miradi yenye hadhi ya nyota 5 a.k.a 'Reputable' siyo miradi ili mradi tu
Siyo bosi wangu!. For the past ten years, I've been my own boss!, situmwi na mtu wala simtumikii mtu bali huyu jamaa namkubali sana kwa uwezo wake! ambapo ndani ya CCM, he is the one and only anayeweza kuinusuru na tsunami ya 2015!.
P.
 
Pasco lazima ajitokeza kwa sababu Lowasa alimsaidia sana siku alipopata matizo ughaibuni. Lowasa ana miradi mingi (overt and covert) yenye kuchurn out pesa nyingi kuliko hao uliowataja kwa pamoja
simsupport kwa sababu alinisaidia, bali huyu jamaa namkubali sana kwa uwezo wake, uchapaji kazi wake, na uwezo wa kuchukua maamuzi magumu bila kumungunya maneno, kama alivyowatimua City Water, na kile kitendo cha kishujaa sana kwa kukubali kulibeba zigo la dhambi ya Richmond ili kina fulani waokoke!. Ni kwa kuteswa kwake wao waliponywa!.
P.
 
Lowassa ni mchapa kazi ila tukimpa kuongoza nchi hii jasho la damu litatutoka maana ni mpaka arudishe hizo pesa za harambee na faida kwa hao "marafiki" zake, atengeneze maisha yake na familia yake kama afanyavyo Kikwete sasa, atengeneze biashara na marafiki na foreigners na labda cha maana atakachofanya ni kumalizia project yake ya shule za kata.
 
Pasco lazima ajitokeza kwa sababu Lowasa alimsaidia sana siku alipopata matizo ughaibuni. Lowasa ana miradi mingi (overt and covert) yenye kuchurn out pesa nyingi kuliko hao uliowataja kwa pamoja

Mkuu utakua humtendei haki Pasco unaposema kua anamtetea Lowasa kwa sababu amewahi kusaidiwa na EL. Ikiwa hivyo itabidi wengine waamini kua wanaompinga EL nao kwa njia moja au nyingine wamenufaika na wapinzani wa EL.
 
Kila anapochangia...anasema yeye hana pesa ila amechangiwa na marafiki zake.Haya huwa anayazungumza anapokuwa anatoa mchango wake wa fedha nyingi sana kwenye vikundi.

Watanzania hizo ni pesa zenu ambazo zilikuwa zimeibiwa sasa zinarudi na ninacho waomba mzipokee kwa mikono miwili lakini mnajua wp mtatoa kura yenu lakini kama mtaafanya makosa kumpa kura mtu ambaye ameleta pesa kwenu ila apate kura madhala yake ni makubwa sana.

Wafanya biashara ni marafiki zake na hao ndio wanao pambana kumweka madarakani je atawalipa nini akishakuwa rais?

Nahisi hili sakata la wauza unga kukamatwa litakuwa na madhara makubwa sn kwa wana siasa hasa ktk wakati huu wa maadalizi ya Wagombea uraisi na wakati wa kampeni 2015 kwani wengi wa hawa majamaa ni mitaji yao, wakiingia madarakani wanawapa vibali.
 
Maneno mengine natoa tahadhali kwa wasomaji wawe makini ikiwa ni pamoja na kukaa jirani na maziwa kwani statement nyingine ni sumu hivyo ukimeza kama ilivyo umekwisha. Pesa ya rushwa haiwezi kutumika kuzuia rushwa. wananchi kuweni na msimamo wenu kama lowasa anafaa na anawafaa kwa kuiba na baadaye kilichopatikana akala na ninyi nadhani huyu si mwizi mbaya, angalia wenzetu Moshi wanavyowaenzi akina Mramba, Msuya nk
 
Mkuu utakua humtendei haki Pasco unaposema kua anamtetea Lowasa kwa sababu amewahi kusaidiwa na EL. Ikiwa hivyo itabidi wengine waamini kua wanaompinga EL nao kwa njia moja au nyingine wamenufaika na wapinzani wa EL.

Ha ha ha lowasa anatoa sana pesa kwa watu wake wa karibu anao jua hawa wanamsaidia
 
jamani mnasahau mradi wake wa richmond dowans ndo unaomwingizia pesa nyingi si alishnda kesi dhidi ya tanesco...watanzania msiwe wasahaulifu mapema hivi.
 
wewe hujui kuwa Lowasa ndiye aliye iingiza nchi mkenge wa Richmond na Dowans? Wewe hujui kuwa Lowasa huyo huyo ni miongoni mwa-wafaidika wa mabilioni ya EPA? Je, hujui pia hata ile mvua ya kutoka Thailand iliyokuwa ijaze mabwawa ya Mtela na Kidatu ulikuwa mpango wa Lowasa kupola mabilioni? wewe unaishi nchi gani? ZINDUKA na muogope Lowasa kama UKOMA.
 
Si amesema anayatoa kwa marafiki jamani? Au?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Zimeandikwa sana habari za Lowassa humu, lakini nami napenda nigusie kwenye suala la UKWASI wa huyu mtanzania mwenzetu.

Mwanasiasa wa muda mrefu ambaye amepata kuwa Waziri mkuu wa Jamhuri, kabla ya kulazimika kujiuzulu, amekuwa akihusudiwa sana na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kuchangisha fedha kwenye shughuli nyingi. Iwe ni kwenye ujenzi wa shule, zahanati, makanisa, misikiti n.k.

Swali la msingi la kujiuliza ni kuwa, mbali ya kuwa yeye ni mhamasishaji mahiri, lakini pia huchangia pesa nyingi binafsi Kutoka katika mifuko yake mwenyewe. Mathalani, juzi juzi tu hapa katika harambee pale KKKT Kijitonyama, jamaa huyu alitoa shilingi Milioni kumi. Na amekuwa akichangia hivyo karibu katika kila harambee anayoitwa kuchangia. Kama kuna chombo cha habari chenye kutunza kumbukumbu vizuri ya shughuli anazohusishwa, haiyumkiniki huyu jamaa, amechangia mamilioni ya shilingi za kitanzania, kwenye shughuli hizi.

Je anapata wapi fedha hizi zote? Je, kama ni mtaji ameukopa mahali, na kwakuwa ana lengo la kwenda Ikulu (wapambe wake wamesema), akipata hiyo Ofisi kuu, atazilipaje hizo pesa?
 
Back
Top Bottom