Elections 2015 Lowassa: Tusipopata mabadiliko CCM Wananchi watatafuta nje ya CCM

Elections 2015 Lowassa: Tusipopata mabadiliko CCM Wananchi watatafuta nje ya CCM

Kwahiyo na yale mafisadi yoote nyuma ya Lowassa yanahamia CDM? toooba! acha nimeze panadol kichwa kitulie kwanza ntarudi kesho.
 
It's unthinkable how he can now join the opposition after CCM gave him the finger.

The guy that they [the opposition] have spent years bashing for being one of the most corrupt senior government officials.

Hard to imagine but that's politics for you.

It indeed can make strange bedfellows.

But I'll believe it when I see it.
 
mimi ni mwana ukawa hai, na sina ndoto ya kuwapigia kura ccm hata wakisimamisha malaika, kwa mstakabali mwema wa nchi hii na ili tupate mageuzi ya kweli ni shariti ccm ipasuke kwanza, kwa muktadha huo, sioni tatizo tukimpokea lowasa mwaka huu na tumfanye kuwa mgombea urais ili tuizike ccm mazima, nakumbuka hata yeye alisema mageuzi sio lazima yaletwe na ccm ila tunaweza kuyapata nje ya ccm, karibu ukawa nitakuwa ni mmoja wa watakaokupokea siku hyo, ni mawazo yangu tu wadau... nawasilisha
 
Nimefuatilia matangazo ya jion ya shirika la utangazaji la amerika(VoA) inaonekana kuna ajenda ya siri inaendelea kati ya Chadema na lowasa kama habari hiz zitakuwa ni kweli au kuna mpango huo lowasa inabidi asiwe mgombea urais ili kuepusha Chadema na double standard hasa tukilejea tuhuma za lowasa
 
Wewe dada mbona matusi?jamaa kakuomba ujio wa nyuma?.

Swissme

Lowasa akijiunga Ukawa landscape ya uchaguzi itachange ghafla. Hivi km uwezekno wa kuingoa CCM tukiwa na Lowasa kuna ubaya. CCM wanahofu sana na hii kitu. Upinzani watakuwa wajinga sana kumkataa Lowasa.
 
Hivi wewe unadhani lowasa anaweza kuhama ccm? Ebu acheni uzushi, ndiyo maana siku hizi mitandao ya kijamii haiaminiki kwasababu ya kuvamiwa na wachangiaji uchwara, wazandiki na waongo na stori za kutunga.
 
Hawa Chadema si ndio walikuwa wanasema Lowassa fisadi? Kweli Tanzania hamna upinzani wote waganga njaa tu.
 
Yaani Dr. Slaa angekubali tu, hivi kwanini haelewi kuwa akichukua nchi, Dr. Slaa anaweza kuwa Waziri wa Fedha, Mbowe Waziri Mkuu kisha Lowassa Rais...

Nchii ya Tanzania ingebadilika mwaka mmoja tu, kuwa kama Ulaya...

Dr. Slaa ana nn lakini..!?

Ogopa sana vizee vifupi,havishauriki.
 
Hivi wewe unadhani lowasa anaweza kuhama ccm? Ebu acheni uzushi, ndiyo maana siku hizi mitandao ya kijamii haiaminiki kwasababu ya kuvamiwa na wachangiaji uchwara, wazandiki na waongo na stori za kutunga.

majitu ya ccm kuendelea kukomaa na ccm ndio maana tunachelewa kuendelea, watu kama kangi, ester bulaya, filipokunjombe, n wazur ambao wapo katikat ya majizi mambwa mwitu wasio na huruma na nchi hata kdogo, badala ya kwenda ukawa yamekomalia humo
 
Lowassa akihamia Chadema kura yangu ni kwa ccm tu, kuanzia diwani hadi Rais.

Nakuunga mkono Dk.Slaa bora uachane na Chadema tu, ili kulinda heshima yako.

Watu tumeiamini Chadema bila Lowasa iweje leo muamini Lowassa ndio wa kuwavusha, Tatizo wanasiasa ni tamaa ya madaraka.

Na Lowassa akijiunga Chadema atakuja na mamluki kibao na huo ndio utakua mwisho wa upinzani imara Tanzania.

Kabla ya yote Mbowe na Chadema wamsafishe Lowassa kwanza kuwa huko ccm ameonewa na ni mtu safi na hausiki na Richmond.

Wanasiasa muache kutuchezea watanzania.

Tangu lini uko CHADEMA?
 
wakimpokea Mamvi itabidi watu wawe karibu na Padre Slaa asije kujinyonga bure kwa mawazo
 
Taarifa zinaeleza kuwa hali ndani ya CHADEMA imezidi kuwa tete mpaka sasa baada ya Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa, kutishia kurudisha kadi ya Chadema na kuachana na siasa za Chama hicho kama Mbowe ataendelea kumshawishi na kumuomba Lowassa ajiunge na Chama hicho ili awe Mgombea wao wa Urais.

Dr. Slaa ameonyesha msimamo huo muda mfupi kabla ya Lowassa hajaahirisha mkutano aliotaka kufanya na Waandishi wa Habari Nyumbani kwake Masaki kuhusiana na hatima yake hiyo.

Slaa amekihakikishia chanzo chetu cha habari kwamba yeye humuungi mkono Mbowe kwenye mpango wake huo wa kumtaka Lowassa.

Kijana mmoja wa Chadema ambaye yupo karibu na Mbowe amethibitisha kwamba Mbowe yupo tayari hata kumfukuza Chama Slaa ili Lowassa awe Mgombea wao. anasema Mbowe anaamini kwamba Lowassa ataipeleka Chadema madarakani.

Kwa sababu ya mpasuko huo, timu ya mkakati ya Lowassa imeamua kuahirisha mkutano wao na waandishi wa habari uliokuwa ufanyike leo saa tano asubuhi hii kama ambavyo Mbowe ameomba ili kwanza wamalize tofauti zilizojitokeza Kati yake na Slaa.

Ikumbukwe kwamba hivi Sasa Slaa ana mvutano mkubwa na viongozi wenzake wa UKAWA ambapo analazimisha yeye ndio awe Mgombea.

Tayari Mzee Edwin Mtei ametumiwa ndege ili aje Dar haraka kumshawishi Slaa akubali kumpisha Lowassa kugombea urais.

Kweli sio bure umejiita mapengo maana Uzi wako una mapengo kweli kweli na una nia mbaya. Chadema wanapiga vita ufisadi halafu wamkaribishe fisadi? Be serious! Isitoshe mtu mmoja hawezi kuteua mgombea hata angekuwa mwenyekiti!
 
Back
Top Bottom