Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
... Utampokea Peke Yako Na Mama Yako
Wewe dada mbona matusi?jamaa kakuomba ujio wa nyuma?.
Swissme
Yaani Dr. Slaa angekubali tu, hivi kwanini haelewi kuwa akichukua nchi, Dr. Slaa anaweza kuwa Waziri wa Fedha, Mbowe Waziri Mkuu kisha Lowassa Rais...
Nchii ya Tanzania ingebadilika mwaka mmoja tu, kuwa kama Ulaya...
Dr. Slaa ana nn lakini..!?
Hivi wewe unadhani lowasa anaweza kuhama ccm? Ebu acheni uzushi, ndiyo maana siku hizi mitandao ya kijamii haiaminiki kwasababu ya kuvamiwa na wachangiaji uchwara, wazandiki na waongo na stori za kutunga.
Lowassa akihamia Chadema kura yangu ni kwa ccm tu, kuanzia diwani hadi Rais.
Nakuunga mkono Dk.Slaa bora uachane na Chadema tu, ili kulinda heshima yako.
Watu tumeiamini Chadema bila Lowasa iweje leo muamini Lowassa ndio wa kuwavusha, Tatizo wanasiasa ni tamaa ya madaraka.
Na Lowassa akijiunga Chadema atakuja na mamluki kibao na huo ndio utakua mwisho wa upinzani imara Tanzania.
Kabla ya yote Mbowe na Chadema wamsafishe Lowassa kwanza kuwa huko ccm ameonewa na ni mtu safi na hausiki na Richmond.
Wanasiasa muache kutuchezea watanzania.
Taarifa zinaeleza kuwa hali ndani ya CHADEMA imezidi kuwa tete mpaka sasa baada ya Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa, kutishia kurudisha kadi ya Chadema na kuachana na siasa za Chama hicho kama Mbowe ataendelea kumshawishi na kumuomba Lowassa ajiunge na Chama hicho ili awe Mgombea wao wa Urais.
Dr. Slaa ameonyesha msimamo huo muda mfupi kabla ya Lowassa hajaahirisha mkutano aliotaka kufanya na Waandishi wa Habari Nyumbani kwake Masaki kuhusiana na hatima yake hiyo.
Slaa amekihakikishia chanzo chetu cha habari kwamba yeye humuungi mkono Mbowe kwenye mpango wake huo wa kumtaka Lowassa.
Kijana mmoja wa Chadema ambaye yupo karibu na Mbowe amethibitisha kwamba Mbowe yupo tayari hata kumfukuza Chama Slaa ili Lowassa awe Mgombea wao. anasema Mbowe anaamini kwamba Lowassa ataipeleka Chadema madarakani.
Kwa sababu ya mpasuko huo, timu ya mkakati ya Lowassa imeamua kuahirisha mkutano wao na waandishi wa habari uliokuwa ufanyike leo saa tano asubuhi hii kama ambavyo Mbowe ameomba ili kwanza wamalize tofauti zilizojitokeza Kati yake na Slaa.
Ikumbukwe kwamba hivi Sasa Slaa ana mvutano mkubwa na viongozi wenzake wa UKAWA ambapo analazimisha yeye ndio awe Mgombea.
Tayari Mzee Edwin Mtei ametumiwa ndege ili aje Dar haraka kumshawishi Slaa akubali kumpisha Lowassa kugombea urais.
Kwani lazima niwe mwanachadema ili nihoji mambo ya Chadema.?Tangu lini uko CHADEMA?