Elections 2015 Lowassa: Tusipopata mabadiliko CCM Wananchi watatafuta nje ya CCM

Elections 2015 Lowassa: Tusipopata mabadiliko CCM Wananchi watatafuta nje ya CCM

Taarifa zinaeleza kuwa hali ndani ya CHADEMA imezidi kuwa tete mpaka sasa baada ya Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa, kutishia kurudisha kadi ya Chadema na kuachana na siasa za Chama hicho kama Mbowe ataendelea kumshawishi na kumuomba Lowassa ajiunge na Chama hicho ili awe Mgombea wao wa Urais.

Dr. Slaa ameonyesha msimamo huo muda mfupi kabla ya Lowassa hajaahirisha mkutano aliotaka kufanya na Waandishi wa Habari Nyumbani kwake Masaki kuhusiana na hatima yake hiyo.

Slaa amekihakikishia chanzo chetu cha habari kwamba yeye humuungi mkono Mbowe kwenye mpango wake huo wa kumtaka Lowassa.

Kijana mmoja wa Chadema ambaye yupo karibu na Mbowe amethibitisha kwamba Mbowe yupo tayari hata kumfukuza Chama Slaa ili Lowassa awe Mgombea wao. anasema Mbowe anaamini kwamba Lowassa ataipeleka Chadema madarakani.

Kwa sababu ya mpasuko huo, timu ya mkakati ya Lowassa imeamua kuahirisha mkutano wao na waandishi wa habari uliokuwa ufanyike leo saa tano asubuhi hii kama ambavyo Mbowe ameomba ili kwanza wamalize tofauti zilizojitokeza Kati yake na Slaa.

Ikumbukwe kwamba hivi Sasa Slaa ana mvutano mkubwa na viongozi wenzake wa UKAWA ambapo analazimisha yeye ndio awe Mgombea.

Tayari Mzee Edwin Mtei ametumiwa ndege ili aje Dar haraka kumshawishi Slaa akubali kumpisha Lowassa kugombea urais.
Alaa imekuwaje tena sii niliwasikia wana CDM wakisema Lowassa ndiye mfadhili wa ACT? Au ilikuwa kuwapotezea CCM maanake hii habari kubwa!..
Lowassa hawezi kushinda Uchaguzi mkuu hata kwa nini, atachezewa kama alivyochezewa CCM, kumbukeni anashindana na CCM sio UKAWA wala Chadema. Kama waliweza kumkata jina lake bila maelezo watashindwa nini kumnyima Urais!. Kwanza wanaweza kufungua kesi yake ya Richmond as soon as anatajngaza kujitoa CCM!. Sikumbuki kama madai hayo yaliisha fungwa kabisa...
 
Nimeshangaa sana,wanajf ambao miaka yote kazi yao ni kusema lowasa ni fisadi na cdm hakipokei mafisadi leo wanageuka kumuona lowasa malaika?kweli siasa ni unafiki
 
mtake msitake hata siku moja upinzani huwezi kushika dola ya nchi hii bila kupata wanachama mashuhuri au viongozi kutoka CCM na waliokuwa na nafasi za juu serikalini. Hawa wanaijua fitina, wanajua nini cha kufanya kukabiliana na wizi wa kura ambao ndio kimekuwa kilio cha muda mrefu, uzoefu katika dola na mikakati ya kukiletea chama ushindi. mi nadhani lengo la wanamageuzi wengi ni kuiondoa CCM madarakani na hili haliwezi kufanikiwa bila nguvu kutoka nje.

Ni sawa na unapambana na adui ambaye ni wazi kabisa amekuzidi nguvu then ghafla anatokea mtu ambaye ana nafasi ya kukusaidia na ambaye aliyekuwa adui yako tangu enzi kwa hiyo asikusaidie kummaliza adui kisa nyie ni maadui. tuache hizo jamani, siasa ni zaidi ya utashi wa kawaida. kuiondoa CCM madarakani ni kazi ngumu kuliko pengine kumwondoa Lowassa au kiongozi yeyote baadae

Ndugu umesema kweli tupu.
 
Haa haaa hii ni Israel+Hamas vs ISIS au kama ilvyokuwa Israel+Fatah vs Hamas ....dah adui wa adui ni rafiki wakati mwingine,,,Lakini kiukweli ikitokea basi Chadema imeisha maana ni raisi kuchafuka sana.Nilishasemaga ACT sio tawi la Lowasa kwani likeanzishwa na Zito kwa msaada wa TISS ( Anti EL wing)
 
Wamelia pamoja, wamepigwa mabomu pamoja Watanzania wamelia,wameuwawa na wengine wako magerezani kwa ajili yenu. Leo hii mfarakane kwa ajili ya mtu mmoja ambae wala hamkuwa na matumaini nae. Kaeni muwafikirie Watanzania hao waliofungwa, waliopoteza viungo, ndg zao.
 
Unaandika kana kwamba woote tunatumia akili yako kuwaza. . . . .
 
Nadhani nitakuwa mtu wa Mwisho kuamini hayo matarajio ya Magamba!Wakifanikiwa kuwagombanisha nitaacha kabisaaa kufuatilia Siasa za Bongo!
 
Yaan Chadema naipendaa sana lkn hawa wamenipaa elimu kumbe sisi kushabikiA wao imekuwa tatizo????ndo maana wako kimya mda mrefu kumbe kuna kitu nyuma ya pazia
 
Usiamini propaganda zinazoletwa kuwa hawapatani. Ni uongo kama ule wa Ibilisi na unamalengo mabaya. Viongozi wa Chadema sio kama wa ccm, hawana unafiki
 
tatizo democrac hakuna ndani ya chadema.ni ubabe tu kila cku silaha,mboe, ni shiida.wanatakiwa waandae watu wapya hao wamesha fedy.na.sasa wanatapatapa yule walie muacha wenzao aliyewaloga had watumishi watukanane na kumsahau mungu kwasa7bu ya kitu kidogo wanataka kumchua wao!AIBU hii kwa madicteta hawa.
 
Duh ! Kwa hiyo wewe umeamini kabisa kwamba huo upuuzi uliokuwa unaenezwa jana ni kweli ?!

Wamelia pamoja, wamepigwa mabomu pamoja Watanzania wamelia,wameuwawa na wengine wako magerezani kwa ajili yenu. Leo hii mfarakane kwa ajili ya mtu mmoja ambae wala hamkuwa na matumaini nae. Kaeni muwafikirie Watanzania hao waliofungwa, waliopoteza viungo, ndg zao.
 
Usiamini propaganda zinazoletwa kuwa hawapatani. Ni uongo kama ule wa Ibilisi na unamalengo mabaya. Viongozi wa Chadema sio kama wa ccm, hawana unafiki

Kama hakuna mtifuano unawaza kutuambia kwanini mpaka sasa ukawa hawajatangaza mgombea urais kama hali ni shwari? Ilitakiwa ajulikane siku 3 nyuma
 
tatizo democrac hakuna ndani ya chadema.ni ubabe tu kila cku silaha,mboe, ni shiida.wanatakiwa waandae watu wapya hao wamesha fedy.na.sasa wanatapatapa yule walie muacha wenzao aliyewaloga had watumishi watukanane na kumsahau mungu kwasa7bu ya kitu kidogo wanataka kumchua wao!AIBU hii kwa madicteta hawa.

Kwa jinsi unavyoandika tu inaonyesha hujui unachoandika!
Silaha
Mboe
 
Habari ya kugombana ililetwa humu na magamba. Sio ya kweli.
 
Mkuu unawezaje kuamini propaganda za kiwango cha chini hivyo ?!. Kama unaweza kuchotwa na propaganda cheap kwa kiwango hicho, je zikija zile advanced itakuwaje mkuu ?!

Yaan Chadema naipendaa sana lkn hawa wamenipaa elimu kumbe sisi kushabikiA wao imekuwa tatizo????ndo maana wako kimya mda mrefu kumbe kuna kitu nyuma ya pazia
 
Yaani Dr. Slaa angekubali tu, hivi kwanini haelewi kuwa akichukua nchi, Dr. Slaa anaweza kuwa Waziri wa Fedha, Mbowe Waziri Mkuu kisha Lowassa Rais...

Nchii ya Tanzania ingebadilika mwaka mmoja tu, kuwa kama Ulaya...

Dr. Slaa ana nn lakini..!?

na makao makuu ya Jamhuri yawe Arusha! Hii dhana ya kuona watu fulani wa nchi ni bora kuliko wengine mnaitoa wapi?
 
CHADEMA be careful. Mikakati ya kukimaliza chama hicho ni mingi na ya aina mbalimbali ikiwemo mitandao kama humu JF. Mtachanganywa sana ki-saikolojia, kisiasa, kijamii na hata kiuchumi. Mtapata harrassment za kila aina ili muwe frustrated, mgombane wenyewe kwa wenyewe na baadhi yenu mtahongwa ili kufanikisha mmesambaratika. Kaeni macho sana kwa kila mnalofanya na mnalosema. Wamo mbwa mwitu ndani yenu wamevaa ngozi ya kondoo. Muaminiane kwa uangalifu sana.
 
Huyo lowasa aende tu chadema hawezi kufanya ccm isishinde uchaguzi mkuu,huo ni uchu wa madaraka,na anajua akitoka ccm ndiyo kaisha kisiasa,ana mifano hai ya waliojifanya kuondoka ccm walipo sasa kisiasa,mbaya zaidi ana akili za kushikiwa huo hawezi kupanga mambo yake mpaka ashauriwe na washauri wake wasio mshauri vizuri,miaka aliyonayo ni bora ale pensheni ya uwaziri mkuu,vinginevyo atakufa kwa pressure
 
Back
Top Bottom