Elections 2015 Lowassa: Tusipopata mabadiliko CCM Wananchi watatafuta nje ya CCM

Elections 2015 Lowassa: Tusipopata mabadiliko CCM Wananchi watatafuta nje ya CCM

Nasubiria official statement ili macho yatoke kabisa cause now yamekuwa makubwa tu
 
Una kiherehere kama muuza gongo; si usubiri wenye Ukawa wenyewe watangaze; kwani wewe ndio umekuwa afisa habari wa UKAWA?! kupenda sifa kutakuponza Dude!! Mwanamme huna kifua cha kuhimili mambo kama Demu?! mdomo unakuwashawasha kuropoka tu!?

Hahahaa ngoja nijiandae mbavu zangu kabisa kwa majibu atakayokupa GENTAMYCINE
 
Last edited by a moderator:
kweli nimeamini hakuna upinzani wa kweli,CHADEMA WANAFIKI,huyo ROWASA kisa katoka kaskazini,?kweli nimeamini CHAGADEMA mradi wa wanakaskazini,
 
ni sawa akienda, sio dhambi kwa mungu! anatumia demokrasia na uhuru wake wa katiba wa kuchagua au kuchaguliwa...
 
watu wako CCM kimaslahi zaidi ,lowasa ni mmoja wao nadhani umenisoma
 
Hii taarifa sio ya kuaminika ila kama Chadema wamemkubali Lowasa ni kwa lengo tu la kuipunguza nguvu CCM.

Kama ni kweli CCM haitakua tena ile tunayoijua japo Lowassa naye hatapata Uraisi.
 
ukawa watakuwa wamefanya kosa kubwa sana, uadilifu tunaouimba kila siku utatoka wapi mbele ya mtu tuliyemwima fisaadi miaka yote hii? Labda km kuna mengine yamejificha lkn naanza kukosa raha

ukiambiwa utoe japo ushahidi mmoja tu kuwa lowasa amehusika na ufisadi wowote je utaweza kutoa?
 
Kwanini hamkubali lowasa kuhamia chadema? Kwani ccm ni mama yake? Karibu Mzee wetu tupige vita umaskini wa watanzania. Tunataka MTU anayechukia umaskini
 
UKAWA watakuwa wamefanya kosa kubwa sana, Uadilifu tunaouimba kila siku utatoka wapi mbele ya mtu tuliyemwima FISAADI miaka yote hii? labda km kuna mengine yamejificha lkn naanza kukosa raha
Lowasa siyo fisadi na mungu ni shahidi wa hili. Yote yanayosemwa juu yake ni chuki za baadhi ya watu juu ya mafanikio yake. Wenye ushahidi wa ufisadi wake wauweke hapa au wampelekee IGP. Ikiwa Lowasa ataamua kwenda CHADEMA , CDM wanayo haki na waji wa kumpokea kama walivyokaribishwa wengine bila kujali hizi kelele za vyura. Naamini kupitia Lowasa Nchi yetu itasonga mbele kwani maovu yote ya CCM yatakoma. KARIBU CDM Mheshimiwa Lowasa-mkombozi wa Watanzania.
 
Quote: mhe. Mwijage
ukikakaa karibu na uwaridi utanukia tu!
Lowasa ndani ya CDM atakua msafi classic baby
 
Kwani ni ajabu Lowasa kujiunga CHADEMA??
Alijiunga Dr Slaa toka CCM,wakampokea,
Mtei mwenyewe alikuwa CCM,sasa nani
alikuwa KANU hapo??
Acheni utoto,
Wote hao unaowasema hawakuwa na kasfa yoyote,ni wazi CHADEMA ikimpokea itapoteza robo tatu ya wanachama wake na inaweza kuwa ndio mwisho wa siasa za upinzani Tanzania hadi generation nyingine,kwani watu wanachokichukia na ambacho kimewafanya wahamie upinzinzani kitakuwa hakipo kabisa,hii itakuwa ni highest degree of the betrayal of the people's trust.
 
Back
Top Bottom