Lucas Mwashambwa toa maoni yako kuhusu kauli ya Rais Paul Kagame

Lucas Mwashambwa toa maoni yako kuhusu kauli ya Rais Paul Kagame

Talks with proves, unauhakika na usemalo?
Kwani hatuoni kwenye vyombo vya habari hiyo misaada na mikataba ambayo serikali ya awamu ya Sita inaingia? Halafu cha kushangaza mambo yamezidi kuwa magumu huku mtaani vocha ya sh 1,000 inauzwa 1,100. Sasa kuna haja gani ya Rais na serikali yake kuzunguka huko duniani huku upatikanaji wa basic needs nao unazidi kuwa mgumu? 😂 😂 😂
Hii awamu imekuwa ya hovyo sana maana hata ule ujenzi wa miundombinu umekuwa wa kusuasua, Sielewei hawa viongozi wataishi everlasting life.
 
PK yuko sahihi. Viongozi wengi wa Afrika wana uwezo mdogo wa kufikiri. Haiwezekani nchi yako ina raslimali za kila aina! Halafu bado unaendekeza umatonya.
Hizi resources ni "HANDLE WITH CARE", kwa sababu dunia ni ya watu wote, hata aliye nje ya mipaka ya nchi yako naye pia anahesabu kuwa ana haki nazo. You don't, you die
Hayupo mtu hata mmoja duniani, ambaye ana uwezo mdodgo wa kufikiri kwenye pesa!
 
Ujue kuna kitu huwa kinaniumiza na kunihuzunisha sana.
Ukikaa na whites waliowengi huwa wanaona sisi blacks hatuna akili na bado hatujawa binadamu kamili kujitawala, wanatudharau na kututukana sana.
Mimi naona wanakosea sana kujumlisha wote kwa pamoja.
Wenye sifa hizo hapo hapo juu ni viongozi, Afrika bado inawatu bora sana. Ila aina za siasa za Afrika ndio inafanya wenye Karama za uongozi wakae pembeni na tuongozwe na watu wa hovyo wasiojali.
Inauma sana mkuu, hata aje nani atabadilishwa na system iliyozoeleka
Yaani bila uongo na wizi wanaona hapana
Watu wapumbavu wanalalamika ooh tumeingiliwa na wqhamiaji ila hawajui kuwa wanaowapitisha wengi ni sisi wenyewe
Mara rasilimali zinatoroshwa na wazungu
Hivi mzungu anaweza kuingia kwetu na kubeba kama mwizi?
Sasa hapo ni hao hao viongozi ndio wanakubali haya
Na ukijifanya kuzuia na mhafidhina wanakuuwa
 
Hili tatizo sio la viongozi wakuu wa nchi pekee ila ni changamoto sana hata kwenye jamii yetu, dada zetu, wafanyabiashara wetu, wakulima wetu, watumishi wa umma yaani kila kiumbe hafikirii namna bora ya kutumia rasimali zake kutatua changamoto zake ila wanafikiri kuomba na kukopa tu, wakati hata neno la Mungu linapinga haya maswala ya mikopo na kuomba omba kiufupi tumekua watu tusiemheshimu huyu Mungu hivyo laana inatusumbua sana. Nchi za magharibu hawa wanatuaminisha kuwa bila misaada wala mikopo mtu huwezi kuinuka kiuchumi na sisi tunajifanya hatuoni kuwa hakuna nchi wala mtu alietajiriki kwa mikopo ila kuchanganua rasimali zake na fursa sahihi. Tuamke jamani
 
Kuna mada nyingine zimemzidi kimo kutokana na elimu yake duni kwahiyo mumuonee huruma.
 
Back
Top Bottom