Ludovick Utouh: Tusijikombe sana, fedha ni za Umma sio za Rais

Ludovick Utouh: Tusijikombe sana, fedha ni za Umma sio za Rais

Hii tabia tunayoisikia ya tunamshukuru sana Mhe. Rais na hata kupiga magoti, this is not right (hii si sawa) kwa kuwa hatuwezi kumshukuru Rais..
Hawatamuelewa mzee Utto maana viongozi sasa wamevuka kwenye ujinga wako viwango vya juu yaani upumbavu ktk Tanzania ya leo Elimu haina maana tena utakuta profesa mzima naye anasema Rais Samia ametuletea fedha za miradi,ujinga mtupu.
 
Hii tabia tunayoisikia ya tunamshukuru sana Mhe. Rais na hata kupiga magoti, this is not right (hii si sawa) kwa kuwa hatuwezi kumshukuru Rais...
Kwa tatizo la kujikomba la watanzania labda Mungu aingilie Kati ama liwekwe kwenye katiba mpya. Hatuna watu tena nchi hii hili ni janga kama ushoga
 
Huyo kama anaona wivu kwa mamilioni ya watanzania kumpongeza mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania kwa kazi nzuri anayoifanya na iliyoleta tabasamu na matumaini katika mioyo ya watanzania basi na yeye aende akagombee Urais aone kitakacho mkuta...
Chawa aliyesahaulika 🙁
 
Hii tabia tunayoisikia ya tunamshukuru sana Mhe. Rais na hata kupiga magoti, this is not right (hii si sawa) kwa kuwa hatuwezi kumshukuru Rais...
Wanaipongeza atm kwa kutoa fedha zao wenyewe, shida uchawa na ujinga umezidi,

Yani unaweza ukamuona mwanaume mzima anavyompamba na kumsifia mwanamke mwingine au kipindi cha nyuma kwa magu hadi unajiuliza ana familia kweli huyu au?? Mambo mengine hadi ukiangalia unaona aibu
 
Kumekuwepo na tabia sasa ya wananchi kumshukuru rais kila wanapo pata mradi.

Utasikia tunamshukuru sana rais,
Huku ni kujikomba kutoka kwa wahusika ili kupalilia nafasi zao makazini kwao.

Wakitaka kushukuru basi waseme tunaishukuru serikali au tunaishukuru nchi yetu.

Maneno yenye busara sana kutoka kwa mzee wetu Ludovic Utoh.
 
Back
Top Bottom