Lugha ya kiswahili imepata nguvu sana kongo ni tishio kwa lingala

Kiswahili kilizaliwa Zanzibar,kikaugua Kenya ,kikafia Uganda, kikazikwa Congo...
 
Swahili to the world
 
Kwanza kwa hali halisi ninayoiona nina shaka kama hata hapa Tanzania watu wengi wanauwezo wa kuongea na kuandika kiswahili kwa ufasaha unaokidhi.

Btw, nimekutana na Mkongo mmoja anafundisha kiswahili na kifaransa katika shule moja Afrika ya Kusini. Pia Mkongo mwingine anayefundisha kiswahili Belgium. Nimetokea Wakenya kadhaa wakifundisha Kiswahili katika international schools za baadhi ya nchi za Afrika hata hapa Tanzania. Bado sijamuona Mtanzania akifanya kazi hiyo.

Yawezekana tatizo likawa uenezi hafifu kwa upande wa Tanzania kuhusu vipaji vya lugha vilivyopo na fursa zilizopo. Pia inawezekana ni tatizo la kusisitiza lugha moja tu ya Kiswahili na kupuuza zingine ambazo nazo zina muhimu katika kuelewana na kusaidia kuelewesha wageni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…