Hiyo ndio demokrasia, sio lazima kila ninachopinga mimi kifuatwe. Alikuja Lowassa akapewa nafasi, tulipiga kelele kuhusu mwenendo ule, hatimaye uchaguzi huu mgombea wa Cdm alipatikana kwa kura za mkutano mkuu, na sio watu wachache. Nyalandu hakupewa nafasi kwa upendeleo, bali aligombea kwenye utaratibu wa chama akapata nafasi. Lakini kwa ule utaratibu wa watu wachache, Nyalandu angeweza kuwa mgombea wa Cdm. Kelele zetu ndio zinaamua mambo yaendeje, hizo nyingine ni porojo tu.
Wakati tulipogoma kujiandikisha kwenye uchaguzi wa SM za mitaa 2019 baada ya dhalimu kuwa na tabia ya kunajisi chaguzi, Mbowe na Halima Mdee walienda kujiandikisha wakidhani watatushawishi kushiriki ule upuuzi, tulichowaambia huku mitandaoni walijuta kwanini walienda kujiandikisha,na hatimaye walikitoa chama kushiriki ule ukhanithi. Hizo nguvu mnazoomini anazo dhidi yetu wafuasi kwenye mambo ya msingi ni upepo mnajilisha.