Lugha za wasakatonge wa awamu ya 5 zilizoyeyuka mithili ya theluji wakati wa kiangazi

Lugha za wasakatonge wa awamu ya 5 zilizoyeyuka mithili ya theluji wakati wa kiangazi

Hatarii Sana, tulionya kitambo Sana, Kitendo cha shujaa kuimaliza kazi yake ya hapa duniani na kwenda huko Kwa njia ambayo kila mmoja ataipitia, hili jukwaa tusipoangalia litakosa hoja za maana kipindi kirefu Sana,

Kipindi chake, kila alilokuwa akilisema lilionekana ni kama geni masikioni mwa wengi hasa wapinzani wake, na ndio Maana kulikuwa kunazaliwa mijadara kibao, na Kwa sasa kumebakia mijadara ya kijinga tu kama Uzi huu, si ni upumbavu tu wala hakuna hoja yoyote

Kilichobaki Kwa wandishi wengi ni zile dhihaka zisizosaidia chochote!
Jukwaa hili limekuwepo toka Magufuli hajaingia madarakani. Amelikuta, amelia cha. MaGT bado wapo na wataendelea kuingia. Huwezi kuwazuia watu aina ya Musiba na Polepole. Kwenye msafara wa mamba...
 
Muda unaenda kasi sana! Wale wapambe wa kusifia kulikozidi kuabudu na misamiati yao ya kishamba naona sasa wanapukutika utadhani mbelewele za Mtama wa Kongwa.

Eti Tunampambania, anatupambania! Too low! Hivi mtu anayetekeleza majukumu yake na analipwa pesa ndefu na nyingine anabeba na kugawa barabarani huyo anakupambania nini? Hivi mtakuwa watu duni hadi lini wanafiki nyie! bora mmetoweka wenyewe, mlikuwa mnatia aibu sana!

Wamegeuka wapiga miluzi.
 
Wasamehe mkuu,

Hawa akili huwa zinawarudi kila oktoba ya mwaka wa uchaguzi.

Kwa sasa wako kipindi cha mpito
Kama mnajivunia aina hii ya chaguzi, basi poleni sana. Kuna wanaccm ambao huona aibu. Hao huwa nawaelewa
 
Muda unaenda kasi sana! Wale wapambe wa kusifia kulikozidi kuabudu na misamiati yao ya kishamba naona sasa wanapukutika utadhani mbelewele za Mtama wa Kongwa.

Eti Tunampambania, anatupambania! Too low! Hivi mtu anayetekeleza majukumu yake na analipwa pesa ndefu na nyingine anabeba na kugawa barabarani huyo anakupambania nini? Hivi mtakuwa watu duni hadi lini wanafiki nyie! bora mmetoweka wenyewe, mlikuwa mnatia aibu sana!

Wanamtisha kwa miluzi eti aache kipi afanye kipi
 
Narudia tena, huna hoja Kwa sasa, zaidi Sana hoja zenu ni zile dhihaka zisizo badirisha chochote
Mbona hata TBC na Bungeni, kusifu na kuabudu hamna tena. Yaani hata mimi sasa naweza kutazama TBC angalau mara moja moja
 
Mbona rushwa na hongo za Magufuli kwa wapinzani zilikuwa wazi kabisa? Watu wanachukuliwa na kupewa vyeo, fedha, utadhani ccm hakuna wanaofaa? Eti anapambana na rushwa, wakati Magufuli ndio mtoa rushwa nambari moja!
shida sio magufuli kumnunua mtu,shida ni chadema kupokea mwana ccm,kisha kumsafisha.
 
shida sio magufuli kumnunua mtu,shida ni chadema kupokea mwana ccm,kisha kumsafisha.
Siyo ishu Magufuli kutoa rushwa? Duuuuu!!!! Ama kweli CCM kuna vichwa. Kwanza hiyo siyo rushwa tu, ni UFISADI pia, maana hiyo pesa siyo yake wala siyo ya CCM, Ni pesa ya walipakodi, inatakiwa kutumika kwa uaminifu na uadilifu na kwa maslahi ya wananchi.

Sasa kama Lowasa na wengine walikuwa mafisadi, si WAMERUDI NYUMBANI? Yaani nyumbani kwa Mafisadi. Na wamepokelewa kwa mikono miwili, nao wameeleza bayana furaha yao kurudi nyumbani. Tatizo kwa CHADEMA linatoka wapi?
 
kwani mh mbowe alipewa shingapi za uma na lowasa??
 
Magufuli aliwagaragaza wapinzani? Alijigaragaza mwenyewe, ndio maana sasa hivi yupo alipo.

Tungesema Magufuli kuwagaragaza wapinzani kama wangekuwa hoi kwenye uchaguzi wa 2019 na 2020. Baada ya kuwafunga mikono, miguu na midomo kwa miaka 5, tulishangaa CCM inaishia kucheza faulo kubwa, hata aibu hawana. Magufuli anawaogopa wapinzani balàa.
Tundu Lissu naye wala hakuwapo nchi ni miaka, lakini uliona kile kimbunga? Mtu mpaka anakataliwa makusudi kutua mikoa kadhaa.

Watanzania ni kweli bado hawajafikia kiwango cha kuprotest kama ilivyo Kenya na kwingineko. Angalia mfaño Palestina wanauwawa na majeshi ya Israeli, Kenya wameandamana, sisi kimyaaaa. Lakini hiyo itabadilika tu, vizazi vinabadilika. Umeona kule Myanmar?
Magufuli alikuwa mtu wa dhulma, na mama Samia kasema wazi hataki dhulma. Tunaendelea kumsoma tuone je, vitendo vyake vinaendana na kauli.
Na usubiri 2025 atakugaragaza tena akiwa kaburini
 
Lissu alisababisha shoti kwenye betri kutokana na kufunua na kufichua uchafu wote yakiwemo mauaji ya wavuvi Lubondo

Jiwe alichanganyikiwa ukweli wake wazi huku akiwa ameshurutisha watu waamini kuwa yeye ni msafi.
 
kabla ya maandamano hao viongozi wote walikamatwa, na vyombo vya dola vilivyotumika kupora kura ndio vilikuwa vimejiandaa kufanya mauaji. Mbona wanaccm hamkujitokeza kupambana na hao waliotaka kuandamana, na vyombo vya dola vitazame kama watu wasingeandamana?
Ukiona mtu anaandamana ujue ameshiba na anatafuta kufanya mazoezi
 
Lissu alisababisha shoti kwenye betri kutokana na kufunua na kufichua uchafu wote yakiwemo mauaji ya wavuvi Lubondo
mbona asisababishe marekebisho ya mguu wake!!!

mkiishiwa hoja mnakiwa kama wasen£
 
Mbona hata TBC na Bungeni, kusifu na kuabudu hamna tena. Yaani hata mimi sasa naweza kutazama TBC angalau mara moja moja
Sjajua ulini quote ili uzungumze nini...? Mbona hiyo Tbc hainihusu mkuu, au ulitaka kujenga hoja gani Yani??

Eebhana...! Uwe na jioni njema
 
Back
Top Bottom