Magufuli aliwagaragaza wapinzani? Alijigaragaza mwenyewe, ndio maana sasa hivi yupo alipo.
Tungesema Magufuli kuwagaragaza wapinzani kama wangekuwa hoi kwenye uchaguzi wa 2019 na 2020. Baada ya kuwafunga mikono, miguu na midomo kwa miaka 5, tulishangaa CCM inaishia kucheza faulo kubwa, hata aibu hawana. Magufuli anawaogopa wapinzani balàa.
Tundu Lissu naye wala hakuwapo nchi ni miaka, lakini uliona kile kimbunga? Mtu mpaka anakataliwa makusudi kutua mikoa kadhaa.
Watanzania ni kweli bado hawajafikia kiwango cha kuprotest kama ilivyo Kenya na kwingineko. Angalia mfaño Palestina wanauwawa na majeshi ya Israeli, Kenya wameandamana, sisi kimyaaaa. Lakini hiyo itabadilika tu, vizazi vinabadilika. Umeona kule Myanmar?
Magufuli alikuwa mtu wa dhulma, na mama Samia kasema wazi hataki dhulma. Tunaendelea kumsoma tuone je, vitendo vyake vinaendana na kauli.