Sababu nyingine, huenda ambayo ni kubwa zaidi ni ile ambayo marehemu alisema kuwa Mpina ni kichaa kama yeye. Kama wameamua wasiwe na MNEC kichaa, sidhani kama angepitishwa. Labda itolewe kauli nyingine ya kubatilisha kauli ya marehemu itakayosema Mpina siyo kichaa, na marehemu alidanganya kudai kuwa alikuwa kichaa kama yeye. Na ili kauli mpya ikubaliwe, ni muhimu ikapatikana taarifa ya kitabibu.
Kutokana na yaliyotokea awamu iyopita, iwekwe sheria inayozuia kabisa mtu aliyewahi kupatwa na tatizo la afya ya akili, kuwa kiongozi mahali popote pale, hata kama matabibu watasema amepona. Magonjwa ya akili yana kawaida ya kujirudia.