Luhaga Mpina aenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC)

Luhaga Mpina aenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC)

Acha wivu wa kimalaya , tofautisha Mpina akiwa waziri na sasa ni mbunge,acheni afanye kazi ya kibunge,wewe ni [emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706] kabisa,hutaki mbunge atimize majukumu yake?narudia tena wewe ni nyoko kabisa
We tukana unavyoweza ila ndio imetoka hiyooo 2025 atafute kazi nyingine ya kufanya tumechoka wanafiki.

Eti majukumu ya mbunge? Kwani alipokua mbunge mwaka Jana JPM hakuwepo hai? Mbona hakumkataza kufanya manunuzi ya ndege nje ya bajeti? Mbona sikusikia akipinga JPM kuchukua mkopo wa SGR? Sikusikia akisema trillion 360 zilipwe!! Eti JPM kafariki ndio anagundua kuwa Trillion 360 hatukulipwa??

Kama amekutuma mwambie waTanzania tunajitambua CCM msituchezee akili kabisa, unafiki wenu tumeuchoka.
 
Huyu jamaa ni mnafiki sana Wacha wamnyooshe. Wakiwa serikalini walikopa eeh kujenga miradi sikusikia kelele eti katoka ndio anagundua mikopo ni mibaya. JPM malipo kibao alifanya nje ya bajeti iliyopangwa mfano manunuzi ya ndege ila ilionekana sio shida but ujinga ule ule ukiendelezwa na awamu hii eti ndio anapinga!!!

Nasema hivi anyooshwe na 2025 afyekwe kabisa kura za maoni. Hawa wanafiki tumewachoka, kesho akipewa uwaziri utashangaa anaanza kumpamba Tena Mama.
Na akija upinzani asipokelewe.
 
Acha wivu wa kimalaya , tofautisha Mpina akiwa waziri na sasa ni mbunge,acheni afanye kazi ya kibunge,wewe ni [emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706] kabisa,hutaki mbunge atimize majukumu yake?narudia tena wewe ni nyoko kabisa
2025 mpina anagombea ubunge kupitia cdm
 
Ungehoji mantiki ya hoja zake ungekuwa umetoa mchango kwenye platform ila kudai kuwa hata zamani mambo hayo yalikuwepo hujasema kitu
Kwenye siasa credibility ndio kila kitu mfano Dk Gwajima alisema chanjo zina madhara ghafla kaingia Samia eti ooh chanjo ni salama je ulitaka hapo tuchukue "mantiki"?

Embu kuweni serious, kama hakudai Trillion 360 JPM akiwa hai basi akae kimya mile hatutaki unafiki maana kesho akipewa Tena uwaziri utasikia oooh Hakuna kama Mama...
 
Reasoning capacity ya vijana wengi humu jukwaani ni zero kabisa,mfano ni huyo uliemjibu,wanapambana na Luhaga as personal badala ya hoja zake
Wewe ndio una reasoning ndogo sana maana wanasiasa wanakupindua kama chapati!!!

Kesho akirudishwa wizarani utasikia ooh Mama Samia ni Rais Bora Toka uhuru.... Mara oooh mikopo ni mizuri maana inajenga miradi!!

Alafu utakuja Tena humu kulia Lia.... Kama haiwezi kujifunza na wanafiki waliopita kama Polepole na Kabudi then una reasoning ndogo kuliko hao unaowazodoa!!

Embicile
 
kwa mfumo huu ukishatemwa CCM huna la kufanya - sababu jamaa wana kila kitu ushauri ni kuwa mpole.
Uwe mpole au useme kuwa nitaendelea na msimamo wangu, liwalo na liwe.
 
wamekwambia hafai kwa sababu zipi na kama unayosema ni kweli si asingekuwa Mbunge maana pia anapitishwa na vikao hivyo hivyo
Kwani wabunge wa awamu hii walichaguliwa na wananchi? 75% ya wote waliogombea kupifia CCM, yalikuwa ni maamuzi ya marehemu, walikuwa wamekataliwa na wajumbe ndani ya CCM.

Halafu hao 75% pamoja na 25% ambao majina yao yalipitishwa na wajumbe, wakurugenzi waliagizwa wawatangaze kuwa ni wabunge.

Mpina na wenzake wote ni wabunge wa marehemu. Na kwa sababu marehemu, ambaye ndiye aliyewachagua, na ndiye waliyekuwa wanamwakilisha, kwa sasa hayupo Duniani, ina maana hakuna wanayemwakilisha. Wanapiga porojo kwa namna inavyowapendeza. Lakini wananchi hawana mwakilishi.
 
Apunguze usukuma gang na kuimba taarabu bungeni.....asipoangalia vizuri kwenye kura za maoni za kugombea nafasi ya ubunge hapiti😃
Labda kutokee mageuzi ya kiuongozi kama yaliyotokea vinginevyo aende kule alikodhulumu ardhi ya wanakijiji akalime bange tu
 
Hahahahaha, Mkuu umemaliza kila kitu! Huyu Mpina hata haeleweki anataka nini, ndiyo maana kapuuzwa
Kwa ujumla, hata siku moja usimwamini mnafiki kwa jambo lolote.

Huyu Mpina, aliyewatia umaskini wavuvi na wafanyabiashara wa samaki, na kuwapiga faini kubwa wenye mabasi eti kwa vile tu ndani ya mabasi yao kulipatikana abiria waliokuwa wamebeba samaki wa mboga, leo eti ana huruma na wananchi! Siwezi kuamini.

Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka, 'kiongozi akitamka kuwa anachukia rushwa, umtazame na usoni anapoyaongea hayo. Anakuambia, mimi nachukia sana rushwa, unamtazama usoni, unasema, huyu! Huyu anachukia rushwa, hapana'.

Mpina huyu, aliyefikia mpaka kuwapima samaki waliopo kwenye sahani kwa rula, aliyewafuata wavuvi wenye makokoro ambao walikuwa wameyaondoa makokoro yao toka ziwani, yapo majumbani mwao, lakini bado akawapiga faini ya zaidi ya sh 200m, leo eti anawatetea Watanzania.

Tujiulize, ikitokea kuna jambazi sugu mtaani kwenu, na mnamjua maana amekwishawaumiza wengi hapo mtaani, halafu siku moja huyo jambazi akawa anapita kila nyumba kuwaambia majambazi ni watu wabaya, tuchukue hatua dhidi yao, mtamwamini?,
 
PANGA LA NEC LAMFYEKA LUHAGA MPINA- JINA LAKE LAENGULIWA KUGOMBEA UJUMBE WA NEC.

* Mambo 11 yaliyomponza yatajwa

HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi imeliengua jina la Mbunge wa Jimbo la Kisesa wilayani Meatu Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) Mkoa wa Simiyu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Chama hicho mara baada ya vikao vya Taifa vya uteuzi na kuthibitishwa pia na Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mohamed Ali Khalfan alisema jina la Mpina halimo kwenye orodha ya majina ya wagombea wa nafasi ya NEC Mkoa wa Simiyu yaliyopitishwa na vikao vya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

Mpina alikuwa ni miongoni mwa makada wa CCM waliochukua na kurejesha fomu kuomba nafasi ya MNEC Mkoa wa Simiyu na NEC Viti 15 Tanzania Bara.

Hata hivyo katibu huyo wa CCM mkoani Simiyu hakuweza kuyataja majina ya walioteuliwa kwa kuahidi kuyataja baadae kwani wakati anazungumza na mwandishi wa habari hizi alisema yuko kwenye mkutano wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Mkoa.

Baadhi ya makada wa CCM wamesikika wakidai huenda ikawa jina la Mpina limeenguliwa kutokana na misimamo yake anayoionyesha bungeni katika kuhoji mambo mbalimbali ya wananchi.

Makada hao wamedai miongoni mwa mambo yanayoweza kuwa yamemponza Mpina ni kuhoji bungeni kuhusu madai ya fedha za makinikia Trilioni 360 akitaka kujua nani alisamehe na kama ana mamlaka kisheria kusamehe madai halali ya watanzania ya kiasi cha shilingi Trilioni 5.5 kama ilivyoamuliwa na Mahakama za rufani za Kodi za TRAB na TRAT.

Lingine ni kuhoji bungeni juu ya Serikali kushindwa kudai madai halali ya Shilingi Trilioni 1.5 kwa ucheleweshaji wa mradi na CSR kutoka kwa Kampuni ya Arab Contractors ya Misri inayojenga mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Julius Nyerere. Lakini pia Serikali kuendelea kutoa taarifa zinazokinzana juu ya ukamilishaji wa mradi huo.

Mpina pia kupitia Bunge alihoji kuhusu kupaa kwa Deni la Taifa kutoka wastani wa kukua kwa asilimia 4 hadi asilimia 13 na kutojulikana zilipo shilingi Trilioni 5 zilizokopwa nje ya bajeti kwa mwaka 2022.

Mbali na hilo Mpina pia alihoji bungeni kitendo cha TRA kushindwa kukusanya malimbikizo ya kodi yasiyo na kesi mahakamani kiasi cha shilingi Trilioni 7.5 na ucheleweshaji wa maamuzi ya mapingamizi ya kodi katika mahakama za rufani za kodi kiasi cha shilingi Trilioni 5 bila kuwepo sababu za msingi.

“Kuhoji bungeni uhalali wa malipo yaliyofanywa na Serikali kwa Kampuni ya Symbion LLC ya shilingi Bilioni 350 nje ya bajeti na bila kuzingatia madai halali ya Serikali ikiwemo kodi na gharama nyinginezo” alisema Jumanne Mashauri

Jambo lingine ni linalodaiwa kumponza ni kukataa bungeni juu ya uamuzi wa Serikali kujenga Bandari ya Bagamoyo bila kuwepo tathmini ya kina juu ya uwezo wa kiuchumi kugharamia mradi huo.

Suala lingine linalodaiwa kumponza Mpina ni kitendo chake cha kuhoji bungeni kuhusu Serikali kuingia mikataba mibovu, kushindwa kurejesha ngombe 6,000 za wafugaji walioshinda kesi mahakamani, kushindwa kudhibiti tembo wanaovamia mashamba na makazi ya wananchi na kusababisha vifo na majeruhi.

Jambo lingine ni kuhoji bungeni kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta kwa kisingizio cha vita ya Urusi na Ukraine hali iliyoilazimu Serikali kuweka ruzuku ya shilingi bilioni 100 kila mwezi bila kuwepo unafuu wowote kwa wananchi.

Hata hivyo makada hao walisema huenda pia msimamo wake wa kuhoji bungeni suala la katakata ya umeme na migao ya umeme isiyoisha nchini iliyopelekea kuathiri uchumi na utoaji wa huduma zinazotegemea nishati ya umeme huenda pia likawa limemgharimu kuenguliwa.

Maeneo mengine ambayo Mpina amekuwa akihoji bungeni ni kuhusu suala la usimamizi mbovu na kupanda kiholela kwa bei ya mbolea na namna ilivyowaathiri uzalishaji na upatikanaji wa chakula nchini

Pia amekuwa akihoji bungeni juu ya kupanda kiholela kwa bei za bidhaa na gharama za maisha hali iliyopelekea mfumko mkubwa wa bei nchini huku Serikali ikishindwa kudhibiti hali hiyo.

Mpina alipoulizwa kuhusiana na madai ya kuengeliwa kwenye kinyang’anyiro cha NEC Mkoa wa Simiyu simu yake iliita bila kupokelewa na baadaye alituma ujumbe mfupi wa maandishi kuwa yuko kwenye kikao cha Kamati ya Fedha, Utawala na Uongozi cha Halmashauri ya Meatu.`
View attachment 2420267
Huyo Sukuma gang si ana chama Chao kile chenye picha ya Mwendazake? Umma Party 😆😆.

Akajikite huko akishindwa Chadomo wapo
 
Siku tutakapoacha kujadili watu na kujadili issues hii inchi itapiga hatua sana...Until then wacha tuendelee kua kichwa cha wendawazimu kila kinyozi anajifunzia kunyoa...
Of course mm simkubali kwa unafiki maana hapa Tanzania ukiona mtu anashupalia kitu anakuwa kajwruhiwa sehemu au anatafuta kitu..

Hoja za Mpina zinatakiwa kujibiwa
 
Kipindi Cha mwendazake,huyu ni mmoja wa waliokuwa wakitamba sana,hata hayo anayoyapigia kelele yalikuwepo kipindi Cha mwendazake,lakini hakuyazaungumzia,maana alikuwa upande wa wenye asali na Ikulu,sasa baada ya kutupwa nje ya ulaji,imekuwa makasiriko!!!wacha ashikishwe adabu!!
Wewe ni mbumbumbu tu, mbona hawayahoji hayo kumhusu? Roho mbaya tu inakusumbua
 
Back
Top Bottom