Pre GE2025 Luhaga Mpina amshtaki Spika Tulia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuondolewa Bungeni kinyume na Sheria

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa nini Watanzania wengi inaonekana hawaelewi hii point ya msingi kabisa?

Hivi watu wetu hawajui basic separation of powers hivi?
Mkuu naamini maamuzi ya bunge ambayo hayawezi kuingiliwa na chombo chochote ni pale bunge linapofanya debates zake juu ya miswada mbalimbali ama mijadala ya kibunge lakini sio kila kitu kinachohusiana na ukiukwaji wa haki ya mbunge.
 
Mahakama inaweza kutoa hukumu kuhusu uendeshwaji wa mhimili unaojitegemea wa Bunge na Spika?

Hukumu hiyo haitaharibu uhuru wa Bunge kama mhimili unaojitegemea?
Halijashitakiwa Bunge, wameshitakiwa viongozi wa bunge kwa ukiukwaji wa kanuni, mahakama inaenda kutoa tafsiri ya sheria kanuni hizo
 
Mfano wako si mzuri kwa sababu umeongelea mtu aliyeanzia kufukuzwa na mamlaka ya chini.

Mfano mzuri ungekuwa mtu aliyeteukiwa na Rais, akatenguliwa na Rais, halafu akataka kwenda Mahakamani kumshitaki Rais kwa sababu Rais kamtengua bila sabahu halali.

Hapa anashitakiwa Spika, mkuu wa muhimili, kwa tuhuma za kumuadhibu Mpina visivyo.

Mahakama haiwezi kuingilia kwa kutoa hukumu kuhusu jinsi Spika (mkuu wa muhimili)anavyoendesha Bunge na kuwajibisha wabunge wala jinsi Rais (mkuu wa muhimili) anavyoteua na kutengua watu serikalini.
 
Ety mahakama inatafsiri sheria za nchi tu, vipi kesi ya magoma na yanga au mwabukusi na TLS zote wameshinda.
Dr. nshala ni mtu mwenye PHD ya sheria hawezi kufanya oversight ya kitu ambacho hakipo
Nadhani ego inakufanya usikubali kishindwa
 
Halijashitakiwa Bunge, wameshitakiwa viongozi wa bunge kwa ukiukwaji wa kanuni, mahakama inaenda kutoa tafsiri ya sheria kanuni hizo
Kwani wapi nimesema limeshitakiwa Bunge?

Nakwambia hivi, suala lolote la kuhusu Spika anavyoendesha Bunge halitolewi hukumu na Mahakama.

Ukipeleka kesi hiyo Mahakamani, Mahakama itakwambia hilo ni suala la Bunge, Mahakama haihusiki, lirudishe suala hilo Bungeni mkalimalize Bungeni.

Kwa sababu, kanuni za separation of powers zinaikataza Mahakama kutoa hukumu kwenye mambo ya jinsi gani muhimili wa Bunge unajiendesha.

Kama Spika kakosea, kuna mpaka mchakato wa kumuondoa Spika Bungeni na kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Mahakama itasema fuatisheni kanuni zenu za kibunge za kuwajibishana ndani ya Bunge, hili si suala la Mahakama, ni suala la Bunge.
 
Mpina angerudi vipi bungeni kupiga kura na kasimamishwa?
 
Mahakama itasema fuatisheni kanuni zenu za kibunge za kuwajibishana ndani ya Bunge, hili si suala la Mahakama, ni suala la Bunge.
Mtu wa programming na huku upo kumbe?
===
Tunaomba vifungu vya sheria ama katiba vinavyozuia Spika na wengine wasishitakiwe kwenye mahakama.
 
Vipi kesi ya chadema dhidi ya covid 19 mbona haijatupiliwa mbali bado inasikilizwa na mahakama
 
Tangu mwanzo nilijua unazungumzia separation of power, hii bongo haipo
 
Mpina angerudi vipi bungeni kupiga kura na kasimamishwa?
Kwani hatarudi Bungeni? Kafukuzwa milele?

Point yangu ni kwamba Mahakama haiwezi kutoa hukumu kesi ya Spika anavyoendesha Bunge, that is against separation of powers. Mahakama itasema hili ni jambo la Bunge, limalizeni Bungeni.

Unaelewa hilo?

Muhimilinwa Bunge ni kamili katika kujiendesha, haupangiwi na Mahakama unavyojiendesha.

Unaelewa hilo?
 
30 July 2024

Moto wa Mpina Hauzimiki, Athibitisha Mawakili Zaidi ya 100 Wanamuunga Mkono Kwenye Kesi Alizofungua​


Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina akizungumza baada ya mawakili wake kueleza msingi wa kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, amesema kuwa zaidi ya mawakili 100 wameahidi kumuunga mkono......

Mpina amefungua kesi tatu Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu sakata la sukari ambapo amewashitaki Waziri wa Kilimo, Waziri wa Fedha na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Pia kesi nyingine ni dhidi ya Spika wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo amewashitaki kupinga kitendo cha kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya Bunge kwa madai ya kukiuka kanuni za Bunge....

Source : The Chanzo

NCHI JIRANI WAMEWEZA KUUPINGA MUSWADA WA FEDHA WA BUNGE MAHAKAMANI

31 July 2024

MAHAKAMA ya Rufaa imepiga msumari wa mwisho kwenye jeneza la Sheria ya Fedha 2023, kwa kukubaliana na uamuzi wa Mahakama Kuu uliotaja sheria hiyo kuwa kinyume na katiba.

Wakikatalia mbali sheria hiyo ambayo ilikuwa na aina mbali mbali za ushuru ikiwemo Ushuru wa Nyumba ambao ulizua vurumai kote nchini, majaji walisema mchakato wa kuunda sheria hiyo ulikuwa na dosari na kwamba ulikiuka Katiba.

“Kwa sababu hiyo, tunatangaza kwamba kutekelezwa kwa Sheria ya Fedha, 2023 kuwa kulikiuka vifungu 220 (1) (a) na 221 vya Katiba vikisomwa pamoja na Sehemu 37,39A na 40 vya PDMA ambavyo vinaeleza bayana hatua za kutengeneza bajeti, hivyo kufanya Sheria ya Fedha 2023 kuwa kinyume na sheria,”majaji Kathurima M’Inoti, Agnes Murgor na John Mativo wakasema Jumatano, Julai 31
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…