Pre GE2025 Luhaga Mpina amshtaki Spika Tulia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuondolewa Bungeni kinyume na Sheria

Pre GE2025 Luhaga Mpina amshtaki Spika Tulia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuondolewa Bungeni kinyume na Sheria

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa nini Watanzania wengi inaonekana hawaelewi hii point ya msingi kabisa?

Hivi watu wetu hawajui basic separation of powers hivi?
Mkuu naamini maamuzi ya bunge ambayo hayawezi kuingiliwa na chombo chochote ni pale bunge linapofanya debates zake juu ya miswada mbalimbali ama mijadala ya kibunge lakini sio kila kitu kinachohusiana na ukiukwaji wa haki ya mbunge.
 
Mahakama inaweza kutoa hukumu kuhusu uendeshwaji wa mhimili unaojitegemea wa Bunge na Spika?

Hukumu hiyo haitaharibu uhuru wa Bunge kama mhimili unaojitegemea?
Halijashitakiwa Bunge, wameshitakiwa viongozi wa bunge kwa ukiukwaji wa kanuni, mahakama inaenda kutoa tafsiri ya sheria kanuni hizo
 
Mfano Rais yupo muhimili wa Executive ambapo mwajiriwa aliyefukuzwa kazi na mwajiri wake anaweza kuanzia ngazi za usuluhishi kama CMA akakata rufaa hadi kwa Rais akitka arejeshwe kazini lakini Rais anaweza kushikilia msimamo wa mtu huyo kutorejeshwa kazini.

Mtu huyo akienda mahakamani (Labour division) kudai haki yake ya kurejeshwa kazini haina maana kwamba mahakama itakataa kusikiliza shauri lake kisa tu muhimili mwingine ulishamfukuza kazi.

Shauri litasikilizwa na kama mtu huyo ana haki basi atarejeshwa kazini.

Rejea mamlaka ya kuteua ambayo yapo vested to the President.
Rais anaweza kumteua mtu yeyote kushika madaraka ya ofisi yoyote ya umma lakini kama kuna ukiukwaji uliofanyika kwenye zoezi zima la uteuzi labda mtu huyo kukosa sifa fulani basi mtu yeyote anaweza kwenda mahakamani kupinga uteuzi huo.

Rejea kesi ya Addo Shaibu dhidi ya Rais Magufuli na mwanasheria mkuu wa serikali ambapo Addo Shaibu alipinga uteuzi wa Ardelarus Kilangi kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali.
Mfano wako si mzuri kwa sababu umeongelea mtu aliyeanzia kufukuzwa na mamlaka ya chini.

Mfano mzuri ungekuwa mtu aliyeteukiwa na Rais, akatenguliwa na Rais, halafu akataka kwenda Mahakamani kumshitaki Rais kwa sababu Rais kamtengua bila sabahu halali.

Hapa anashitakiwa Spika, mkuu wa muhimili, kwa tuhuma za kumuadhibu Mpina visivyo.

Mahakama haiwezi kuingilia kwa kutoa hukumu kuhusu jinsi Spika (mkuu wa muhimili)anavyoendesha Bunge na kuwajibisha wabunge wala jinsi Rais (mkuu wa muhimili) anavyoteua na kutengua watu serikalini.
 
Kesi ya Mpina ni kuhusu nini?

Kanuni na sheria za Bunge zinapokiukwa hilo ni jambo la Bunge, mwenye mamlaka ya kuzitafsiri ni muhimili wa Bunge, si Mahakama. Mahakama inatafsiri sheria za nchi, si kanuni za Bunge.

Mawakili wanaweza kujazana hata 1,000 kuonesha solidarity na Mpina kwamba kaonewa, au hata kula hela za Mpina, au hata kusikia Mahakama itasemaje, wakijua kwamba kesi haina mashiko Mahakamani na itakataliwa.

Na kwa mawakiki wetu hawa wengine siwezi jushangaa hata wakiamininkwamba wana kesi wanayoweza kushinda, tuangalie mahakama itasemaje.

Mimi natabiri kuwa, kwenye hoja yoyote ya kumshtaki Spika kwa jinsi alivyoliendesha Bunge, mahakama itatupilia mbali shauri hilo, kwa kisema haiwezi kuingilia suala la Spika anavyoendesha Bunge, hilo ni suala la kumalizwa Bungeni.

Hizi kesi nyingine ni za kisiasa za kujenga sympathy kwenye public opinion kuliko kutafuta ushindi Mahakamani.
Ety mahakama inatafsiri sheria za nchi tu, vipi kesi ya magoma na yanga au mwabukusi na TLS zote wameshinda.
Dr. nshala ni mtu mwenye PHD ya sheria hawezi kufanya oversight ya kitu ambacho hakipo
Nadhani ego inakufanya usikubali kishindwa
 
Halijashitakiwa Bunge, wameshitakiwa viongozi wa bunge kwa ukiukwaji wa kanuni, mahakama inaenda kutoa tafsiri ya sheria kanuni hizo
Kwani wapi nimesema limeshitakiwa Bunge?

Nakwambia hivi, suala lolote la kuhusu Spika anavyoendesha Bunge halitolewi hukumu na Mahakama.

Ukipeleka kesi hiyo Mahakamani, Mahakama itakwambia hilo ni suala la Bunge, Mahakama haihusiki, lirudishe suala hilo Bungeni mkalimalize Bungeni.

Kwa sababu, kanuni za separation of powers zinaikataza Mahakama kutoa hukumu kwenye mambo ya jinsi gani muhimili wa Bunge unajiendesha.

Kama Spika kakosea, kuna mpaka mchakato wa kumuondoa Spika Bungeni na kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Mahakama itasema fuatisheni kanuni zenu za kibunge za kuwajibishana ndani ya Bunge, hili si suala la Mahakama, ni suala la Bunge.
 
Mahakama inafuata sheria. Usifanye kosa la kuchanganya sheria na haki.

Mahakama zishawahi kutupa kesi za mashauri ya bunge kwa msingi wa kutenganisha nguvu za Bunge na Mahakama.

Nimeuliza swali hujanijibu, sijui kama hata umelielewa.

Mahakama haiingilii Bunge. Hii ni mihimili tofauti na yote inajitegemea. Sijui watu hawaelewi hii kanuni au vipi?

Hii kesi ya Spika na masuala ya Bunge linavyoendeshwa itasikilizwaje na Mahakama bila Mahakama kuingilia uhuru wa Bunge?

Huoni kwamba Mpina alitakiwa kwenda Bungeni na kuweka motion ya kumpigia Spika kura ya kukosa imani, Spika awe impeached? Wabunge wamalize mambo yao Bungeni bila ya kuingia kwenye mtego wa kupeleka kesi Mahakamani halafu Mahakama ikatae kusikikiza kesi kwa sababu ni jambo la uendeshwaji wa Bunge, na Mahakama haiwezi kuingilia mambo ya uendeshwaji wa Bunge?
Mpina angerudi vipi bungeni kupiga kura na kasimamishwa?
 
Mahakama itasema fuatisheni kanuni zenu za kibunge za kuwajibishana ndani ya Bunge, hili si suala la Mahakama, ni suala la Bunge.
Mtu wa programming na huku upo kumbe?
===
Tunaomba vifungu vya sheria ama katiba vinavyozuia Spika na wengine wasishitakiwe kwenye mahakama.
 
Kwani wapi nimesema limeshitakiwa Bunge?

Nakwambia hivi, suala lolote la kuhusu Spika anavyoendesha Bunge halitolewi hukumu na Mahakama.

Ukipeleka kesi hiyo Mahakamani, Mahakama itakwambia hilo ni suala la Bunge, Mahakama haihusiki, lirudishe suala hilo Bungeni mkalimalize Bungeni.

Kwa sababu, kanuni za separation of powers zinaikataza Mahakama kutoa hukumu kwenye mambo ya jinsi gani muhimili wa Bunge unajiendesha.

Kama Spika kakosea, kuna mpaka mchakato wa kumuondoa Spika Bungeni na kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Mahakama itasema fuatisheni kanuni zenu za kibunge za kuwajibishana ndani ya Bunge, hili si suala la Mahakama, ni suala la Bunge.
Vipi kesi ya chadema dhidi ya covid 19 mbona haijatupiliwa mbali bado inasikilizwa na mahakama
 
Hao wanasheria wengine hata kama wanajua hapa hakuna kesi, wanaweza kumjaza ujinga Mpina ili wale pesa zake tu.

Ila kiukweli hapa Mahakama itaitupilia mbali hii kesi kabla hata ya kuisikikiza kwa kina.

Kwa sababu ya "separation of powers".

How do people not see something that is so obvious?
Tangu mwanzo nilijua unazungumzia separation of power, hii bongo haipo
 
Mpina angerudi vipi bungeni kupiga kura na kasimamishwa?
Kwani hatarudi Bungeni? Kafukuzwa milele?

Point yangu ni kwamba Mahakama haiwezi kutoa hukumu kesi ya Spika anavyoendesha Bunge, that is against separation of powers. Mahakama itasema hili ni jambo la Bunge, limalizeni Bungeni.

Unaelewa hilo?

Muhimilinwa Bunge ni kamili katika kujiendesha, haupangiwi na Mahakama unavyojiendesha.

Unaelewa hilo?
 
30 July 2024

Moto wa Mpina Hauzimiki, Athibitisha Mawakili Zaidi ya 100 Wanamuunga Mkono Kwenye Kesi Alizofungua​

1722437460273.png

Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina akizungumza baada ya mawakili wake kueleza msingi wa kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, amesema kuwa zaidi ya mawakili 100 wameahidi kumuunga mkono......

Mpina amefungua kesi tatu Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu sakata la sukari ambapo amewashitaki Waziri wa Kilimo, Waziri wa Fedha na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Pia kesi nyingine ni dhidi ya Spika wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo amewashitaki kupinga kitendo cha kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya Bunge kwa madai ya kukiuka kanuni za Bunge....

Source : The Chanzo

NCHI JIRANI WAMEWEZA KUUPINGA MUSWADA WA FEDHA WA BUNGE MAHAKAMANI

31 July 2024

MAHAKAMA ya Rufaa imepiga msumari wa mwisho kwenye jeneza la Sheria ya Fedha 2023, kwa kukubaliana na uamuzi wa Mahakama Kuu uliotaja sheria hiyo kuwa kinyume na katiba.

Wakikatalia mbali sheria hiyo ambayo ilikuwa na aina mbali mbali za ushuru ikiwemo Ushuru wa Nyumba ambao ulizua vurumai kote nchini, majaji walisema mchakato wa kuunda sheria hiyo ulikuwa na dosari na kwamba ulikiuka Katiba.

“Kwa sababu hiyo, tunatangaza kwamba kutekelezwa kwa Sheria ya Fedha, 2023 kuwa kulikiuka vifungu 220 (1) (a) na 221 vya Katiba vikisomwa pamoja na Sehemu 37,39A na 40 vya PDMA ambavyo vinaeleza bayana hatua za kutengeneza bajeti, hivyo kufanya Sheria ya Fedha 2023 kuwa kinyume na sheria,”majaji Kathurima M’Inoti, Agnes Murgor na John Mativo wakasema Jumatano, Julai 31
 
Back
Top Bottom