Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mkuu Maalum wa chama cha ACT Wazalendo kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho kwa kupata kura 559 sawa na asilimia 92.3 ya kura 610 zilizopigwa.
Aidha aliyekuwa akigombea naye nafasi hiyo, Aaron Kalikawe Aaron amepata kura 46 sawa na asilimia 7.7 ya kura.
Wajumbe wa ACT waliopiga kura walikuwa 610, waliopiga kura 610, kura halali ni 605, kura zilizokataliwa au zlizoharibika ni 5.
Katika hatua nyingine, Katibu wa Ngome ya Wanawake wa ACT Wazalendo, Fatma Abdulhabib Ferej ameteuliwa kuwa mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupitishwa na mkutano mkuu maalumu wa chama hicho.
Kabla ya kutangazwa, jina la Fereji kutajwa kuwa mgombea mwenza, lilijadiliwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya ACT Wazalendo kisha kuliwasilisha mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa ajili ya kuthibitisha uteuzi wake.
Katibu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu ndiye aliyewasilisha jina hilo usiku wa kuamkia leo Alhamisi Agosti 7, 2025 mbele ya mkutano huo, kwa ajili ya kuwaomba wajumbe kulipitisha.
" Halmashauri Kuu inapendekeza kwenu jina la Ferej," baada ya maelezo hayo ukumbi ulilipuka kwa shangwe kwa wajumbe kwenda eneo aliloketi Ferej kumpongeza.
Baada ya maelezo ya Ado, Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo (Bara), Isihaka Mchinjita aliwahoji wajumbe wa mkutano mkuu ambao wote waliitikia ndio wakimaanisha jina limepita.
Ferej ni mmoja wa wanawake shupavu visiwani Zanzibar, mwaka 2013 alitunukiwa tuzo ya mwanamke jasiri na serikali ya Marekani, kupitia ubalozi wake, jijini Dar es Salaam.