Hapo Wanakisesa wanatakiwa wasimpigie kura maana huo ni uroho wa madaraka sio uzalendo .
Kama Mpina na wabunge wa CCM walikua anasema kuwa mama Samia amewapekekea Maendeleo makubwa sasa yeye anataka ubunge wa nini wakati Samia bado ni Rais na ataendelea kuwapelekea Maendeleo makubwa .
Wabunge wote wa CCM hawana sababu ya kuchaguliwa tena kwa sababu kila kitu kilifanywa na Samia na kazi yao ilikua ni kupiga makofi na kujiongezea mishahara huku watumishi wa umma kama Wanajeshi ,walimu ,manesi ,Mapolisi n.k wakiwa wanaongezewa mishahara kama kiini macho kwa kuishia kwenye makato ya benki ,miamala ya simu ,madeni yanayotokana na riba kubwa za mabenki , mifuko mfu ya wafanyakazi isiyo na msaada wowote kwa watumishi wa umma zaidi ya kuwanyonya na kuwatajirisha mafisadi .