GE2025 Luhaga Mpina apitishwa kuwania urais kwa tiketi ya ACT kwa 92.3%

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
​

Mkuu Maalum wa chama cha ACT Wazalendo kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho kwa kupata kura 559 sawa na asilimia 92.3 ya kura 610 zilizopigwa.

Aidha aliyekuwa akigombea naye nafasi hiyo, Aaron Kalikawe Aaron amepata kura 46 sawa na asilimia 7.7 ya kura.

Wajumbe wa ACT waliopiga kura walikuwa 610, waliopiga kura 610, kura halali ni 605, kura zilizokataliwa au zlizoharibika ni 5.

Katika hatua nyingine, Katibu wa Ngome ya Wanawake wa ACT Wazalendo, Fatma Abdulhabib Ferej ameteuliwa kuwa mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupitishwa na mkutano mkuu maalumu wa chama hicho.

Kabla ya kutangazwa, jina la Fereji kutajwa kuwa mgombea mwenza, lilijadiliwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya ACT Wazalendo kisha kuliwasilisha mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa ajili ya kuthibitisha uteuzi wake.

Katibu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu ndiye aliyewasilisha jina hilo usiku wa kuamkia leo Alhamisi Agosti 7, 2025 mbele ya mkutano huo, kwa ajili ya kuwaomba wajumbe kulipitisha.

" Halmashauri Kuu inapendekeza kwenu jina la Ferej," baada ya maelezo hayo ukumbi ulilipuka kwa shangwe kwa wajumbe kwenda eneo aliloketi Ferej kumpongeza.

Baada ya maelezo ya Ado, Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo (Bara), Isihaka Mchinjita aliwahoji wajumbe wa mkutano mkuu ambao wote waliitikia ndio wakimaanisha jina limepita.

Ferej ni mmoja wa wanawake shupavu visiwani Zanzibar, mwaka 2013 alitunukiwa tuzo ya mwanamke jasiri na serikali ya Marekani, kupitia ubalozi wake, jijini Dar es Salaam.
 
Yaan mtu si mwenzenu kwa miaka nenda rudi anakuja leo Kesho anakuwa bora kuliko nyote 😆

Tanzania Upinzani una safari ndefu sana
Nina uhakika tarehe 17/10 ambapo Samia anaandika barua ya kutogombea ama kujisikia vibaya kiafya akawekwa Mwingine kugombea, Mpina atarejea

Britanicca
 

Haoni kua ndo atakua amejimaliza kisiasa? Heri mwanzo mbaya kuliko mwisho mbaya
 
Lowasa ,Sumaye nk walikuwa wenzenu?

Mbowe ni mwenzenu?
 
Kwani mpina afahamu bila reforms ni SAWA na kupoteza MUDA


Kwishaaaaaa
 
Mwanachama Mpya wa Act Ndugu Abdulamepinga kuteuliwa Kwa Ndugu Mpina Kwani hajakaa kwenye chama Kwa Muda mfupi. Ninaota Tu
 
Another project...
 
Kama si kama Edward Lowassa
 
Muvi la kihindi
Kawasaliti wa kisesa au ndio mpango mzima wa ccm….


Hapo Wanakisesa wanatakiwa wasimpigie kura maana huo ni uroho wa madaraka sio uzalendo .

Kama Mpina na wabunge wa CCM walikua anasema kuwa mama Samia amewapekekea Maendeleo makubwa sasa yeye anataka ubunge wa nini wakati Samia bado ni Rais na ataendelea kuwapelekea Maendeleo makubwa .

Wabunge wote wa CCM hawana sababu ya kuchaguliwa tena kwa sababu kila kitu kilifanywa na Samia na kazi yao ilikua ni kupiga makofi na kujiongezea mishahara huku watumishi wa umma kama Wanajeshi ,walimu ,manesi ,Mapolisi n.k wakiwa wanaongezewa mishahara kama kiini macho kwa kuishia kwenye makato ya benki ,miamala ya simu ,madeni yanayotokana na riba kubwa za mabenki , mifuko mfu ya wafanyakazi isiyo na msaada wowote kwa watumishi wa umma zaidi ya kuwanyonya na kuwatajirisha mafisadi .
 
Tunaomba iwe hivyo.
 
Hapo zitto ana chakelea maana ameshaingiziwa mabilioni yake tayari kwaajiri ya maigizo ya democracy kwenye uchaguzi.

Madai yeye hasusii uchaguzi.
Zitto akili kubwa, kwenye siasa za Tanzania Zittokabwe ndio mwansiasa mwenye uwezo wa kukabiliana na ccm, wapinzani wengine wote wamejaa jazba na mihemko, ndio maana wanashia jela na uhamishoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…