Pre GE2025 Luhaga Mpina: Nchi sita za Afrika zilizopindua Serikali zao zilikuwa sahihi

Pre GE2025 Luhaga Mpina: Nchi sita za Afrika zilizopindua Serikali zao zilikuwa sahihi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wanaodai Katiba Mpya ndio hao hao wanatumia Rushwa na ngumu kuchaguana ,mpaka hapo hao wanataka madaraka ya Umma Kwa malengo binafsi.

Mwisho Katiba Mpya haijawahi leta ugali walakutatua shida za watu ila ni njia ya Wanasiasa walioko Nje ya serikali kuingia humo wapate ulaji
Nani amekuambia katiba mpya ni unga Hadi ilete ugali mezani?
 
Waliopindua mbona wanaendelea kufanya hayo hayo anayoyasema Mpina?

Utawala upi wa Kijeshi ambao jmewaletea Neema Wananchi? Na mbaya zaidi wanajeshi huwezi walalamikia kwamba umekosa Haki unapigwa tuu.

So hakuna uhalali wa kupindua Wala haijawahi kuwa na faidia popote zaidi ya kuongeza umaskini Kwa watu
Unaonekana kiazi kwenye historia.
Gamal Nasser Hussein,Muamar Gadaffi,Napoleon Bonaparte na Vladimir Lenin wote walifanya mapinduzi na maendeleo waliyofanya kwenye nchi zao ni undisputable.
Hii serikali ya mama yako Samia inatakiwa kupinduliwa ASAP.
 
Hizo nchi anazozitaja Mpina ni jeshi ndio limepindua serikali sio wananchi waliofanya mapinduzi.
Jambo muhimu hapo ni kutafiti ikiwa wananchi waliofurahia MAPINDUZI au waliyapinga?

CCM ilifanya MAPINDUZI pia, na MAPINDUZI hayo yanaitwa " Mapinduzi matukufu".

Nia ikiwa njema, njia yoyote ni sawa!!
 
Sababu zilizotajwa na Mpina zisipokuwa ni sababu za kufanya hivyo, basi mtueleze sababu zinazoweza kupelekea kufanya hivyo ni zipi
Tusubiri press ingine,

Labda ndugu Mpina wa CCM atafafanua zaidi.
 
Jambo muhimu hapo ni kutafiti ikiwa wananchi waliofurahia MAPINDUZI au waliyapinga?

CCM ilifanya MAPINDUZI pia, na MAPINDUZI hayo yanaitwa " Mapinduzi matukufu".

Nia ikiwa njema, njia yoyote ni sawa!!
Nakuelewa Sana...

Ila historia inaendelea kuonyesha hakuna mapinduzi ya kijeshi hapa Africa yaliyoziletea nchi hizo suluhisho la matatizo yao mengi ya kijamii na kiuchumi.

Ila wanapinduzi wapya baada ya muda na wao hugeuka madikteta, mafisadi na ving'ang'anizi vya madaraka
 
Luaga amechoka kukuvuta oxgen,awaishwe haraka safari yake
Watainuka akina Mpina milioni Moja,

Unaweza kumjua " Mpinzani", lakini it is impossible kuua " Upinzani", maana upinzani ni mfumo, uko ndani ya NAFSI.

Amekufa Mtikila, madai ya Tanganyika hayajafa, wanaendelea wengine kudai.

Na usilolijua ni kuwa, Mchimba mashimo, Huwa anatumbukia mwenyewe!!
 
Nakuelewa Sana...

Ila historia inaendelea kuonyesha hakuna mapinduzi ya kijeshi hapa Africa yaliyoziletea nchi hizo suluhisho la matatizo yao mengi ya kijamii na kiuchumi.

Ila wanapinduzi wapya baada ya muda na wao hugeuka madikteta, mafisadi na ving'ang'anizi vya madaraka
Funzo hapo ni kuwa,

CCM iheshimu Sanduku la kura Ili isiwe sababu ya nchi kufika huko pabaya.

Kwa Hali iliyopo,

Inahitajika Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya kabla ya Uchaguzi wowote Ili kuihakikishia Nchi utulivu wa Kweli.
 
Kutumia Demokrasia ni bora kuliko kupinduana.
Iwapo walioko madarakani hawaendi kinyume na misingi ya demokrasia, mfano, eti matokeo ya mshindi wa uchaguzi wa Rais hayahojiwi na chombo chochote cha serikali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Halafu, eti hata TUME haishitakiwi wakiwemo watumishi wake!!!!!!!
 
Waliopindua mbona wanaendelea kufanya hayo hayo anayoyasema Mpina?

Utawala upi wa Kijeshi ambao jmewaletea Neema Wananchi? Na mbaya zaidi wanajeshi huwezi walalamikia kwamba umekosa Haki unapigwa tuu.

So hakuna uhalali wa kupindua Wala haijawahi kuwa na faidia popote zaidi ya kuongeza umaskini Kwa watu
Wanajeshi wakwetu naona wapo kimya tu sjui wanasubilia nini,nchi hii inanuka rushwa sana kila mahali matumizi ya nguvu ya baadhi ya vyombo dhidi ya Raia..kwakweli nashangaa kuona sisi ni masikini sana wakati tuna kila rasilimali ya kutupatia utajiri.
 
Unatakiwa ueleze, nini Hasa sababu kuu ya nchi hizo kupindua Serikali zao kabla ya kuelezea faida na HASARA za baada ya MAPINDUZI.
Uroho wa madaraka kama walionnao Chadema,wanatafuta weak reason wanapindua nao wanaendelea kufanya Yale Yale.

Yaani wewe Kwa akili Yako unadhani wanajeshi watapindua wewe upate maisha? 😁😁

Labda uwe sehemu ya Utawala husika.
 
Salaam, Shalom!!

Akiongea kupitia press aliyoitisha nje ya Bunge amedai kuwa UMOJA wa Afrika haupasi kuzisimamisha uanachama Nchi SITA zilizopindua Serikali zao Kwa sababu Watawala waliopinduliwa hawakujali sauti na matakwa ya wananchi.

Amedai kuwa RUSHWA ikitamalaki, ukiukwaji wa HAKI za binadamu ukiota mizizi, Wizi wa kura ukitamalaki, wizi wa Raslimali za umma ukitamalaki, dhuluma ikizidi katika JAMII, hakuna njia ingine wananchi wanaweza kufanya zaidi ya kupindua Serikali zao Kwa njia mbalimbali.

Ndugu Mpina ameitaka Serikali ya Rais Samia Kutoa tamko kushauri Nchi hizo zisizuiliwe uanachama katika ushirika wa AU.

Chanzo: Uhondo Tv.

Mungu ambariki na kumlinda ndugu Mpina,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

HAKI ikatawale katika Taifa. Amen

Karibuni 🙏
Huu ni ukweli unao umiza..........alichoongea ni ukweli mtupu.
 
Uroho wa madaraka kama walionnao Chadema,wanatafuta weak reason wanapindua nao wanaendelea kufanya Yale Yale.

Yaani wewe Kwa akili Yako unadhani wanajeshi watapindua wewe upate maisha? 😁😁

Labda uwe sehemu ya Utawala husika.
Sababu kuu za mapinduzi ni RUSHWA kutamalaki, wizi wa kura na WA raslimali za nchi.

Kwani imeshindikana CCM kujitenga na wizi wa kura Ili tusiende huko kama Nchi?
 
Wanajeshi wakwetu naona wapo kimya tu sjui wanasubilia nini,nchi hii inanuka rushwa sana kila mahali matumizi ya nguvu ya baadhi ya vyombo dhidi ya Raia..kwakweli nashangaa kuona sisi ni masikini sana wakati tuna kila rasilimali ya kutupatia utajiri.
Kwani wao hawanuki Rushwa? Putin tuu amejaribu kuwadaka na kuwatia ndani Kwa sababu za Rushwa.

View: https://twitter.com/bbcswahili/status/1796059028784644145?t=YwlExrzH1Yr9hQnEH5RJQg&s=19

Nakuhakikishia hawawezi fanya lolote maana nao sio wasafi.Ukifanyika ukaguzi wa manunuzi ya zana utashangaa au hata matumizi ya kawaida
 
Back
Top Bottom