Luhaga Mpina: Pesa za Kununua Mashine za Kuongeza Makalio Mloganzila zimetoka wapi?

Kiukweli hata mimi nilishtuka kusikia taarifa hii. Nchi hii maskini ambayo bado watu wanakufa kwa magonjwa yanayozuilika kwa kukosa hata x ray tunanunua mashine na kuajiri madaktari wa kuongeza makalio?

Huko CCM sijui nini kinaendelea lakini ni dalili za chama kuharibika beyond repair! Zamani wangetifuana kwenye vikao kwa maamuzi hayo ya kijinga ya serikali! Sasa wamejazana machawa ....
 
Kitu Mpina anashindwa kuelewa ni kwamba katika utabibu kuna tawi la "plastic surgery" na walengwa wa utabibu huu ni makundi mawili....

1. Wanaotaka kufanya skin reconstruction baada ya kupatwa na madhara kama kuungua, kumwagiwa tindikali, ngozi kukaka kwa sababu za kijenetiki n.k

2. Wanaotaka kufanya skin reconstruction kwa sababu za urembo (cosmetic reconstruction) baada ya deformations zilizosababishwa na unene kupitiliza n.k

Madaktari wa namba 1 ndio hao wa namba 2, baadhi ya vifaa vya namba 1 vinatumika pia kwa namba 2...

Utabibu si pekee kwa ajili ya watu wanaojiita "wanyonge toka wamepata uhuru" bali pia ni kwa ajili ya wenye pesa ambao ni wachache...

Hizo mashine anazolalama bwana Mpina, mathalani bei ya liposuction machine ni sawa na mshahara wa mbunge huyo wa miezi kadhaa...
 
🚮
 
Kumbe mwanasiasa hugeuka kuwa mkweli pale ambapo ugali wake unakatwa na kubakiwa na robo...

Nampongeza kada mwenzangu Luhanga kwa kujivika ujasiri.
Mfano ni spika mstaafu kipindi cha mwendazake akakata mpaka posho za Tundu lisu kipindi cha mama akaponda utaratibu wa kukopa nje wakati watanzania wanakamuliwa kwa tozo!!!!
 
Naibu Waziri wa Afya kamjibu vizuri tu, nadhani uelewa wake kuhusu plastic surgery ulikuwa mdogo na nina imani baada ya maelezo ya Naibu Waziri ameelewa vilivyo, hatapotosha tena.
 
Kumbe mwanasiasa hugeuka kuwa mkweli pale ambapo ugali wake unakatwa na kubakiwa na robo...

Nampongeza kada mwenzangu Luhanga kwa kujivika ujasiri.
Jikite kwenye hoja yake,achana na Luhaga Mpina as person

Kwanini huwa mnakwepa hoja?
 
Samia anatafuta Kik tu, chochote, kinachomletea cheap popularity, ye ye ni huko huko, upuuzi wa mpira,kununua kila gori kwa milioni moja, kutoa milioni 500! Kwa taifa star, na upuuzi mwingine,
 
Hii nchi kuna watu ni wabinafsi sana utafikiri wao wanalipa kodi zaidi kuliko wengine.

Muimbili mpaka wameanzisha hio huduma washajua wateja wapo na kwa gharama hiyo hizo pesa za machine zinarudi na tunapunguzia watu gharama za kwenda uturuki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…