Luhaga Mpina: Waziri Mwigulu Nchemba anahusika na ufisadi wa trilioni 1.7 mradi wa SGR

Ni wazi, kuna jambo linaloendelea chini kwa chini kati ya CCM na CHADEMA.
Tena umetoa mfano sahihi kabisa kuhusu "uchambuzi wa ripoti ya CAG" kulikofanywa na akina Mnyika na baada ya uchambuzi huo yaliyosemwa hadharani yakawa maigizo!
Siku hiyo hiyo, uchambuzi aliotoa Zitto, pamoja na kumjua anachokisimamia, ripoti aliyoitoa ikawa ndiyo yenye nafuu zaidi ya ile ya CHADEMA!

Nilishasema humu mara kadhaa, na hainichoshi kurudia, kwamba CHADEMA kwa sasa hivi ni sehemu ya CCM ya mama Samia. Ajenda anazosimamia Samia ndizo zile zile Mbowe anazitamani miaka yote; kwa hiyo Samia kabeba furushi lote na Mbowe kabaki hana kitu.
Kilichobaki sasa, hasa ifikapo 2025, kuwasikia tu CHADEMA wakijisalimisha rasmi kwa CCM ya Samia.

Ninachowaza sasa hivi kuwa kinaweza kutokea ni kile ambacho hutokea kila nyakati za chaguzi zinapowadia kule Kenya. Ile miungano ya kutafuta ulaji, yaani uundwaji wa umoja "coalitions"
CHADEMA na CCM na ACTWazalendo na hivi vitakataka vinginevyo, watatuletea Muungano wao ili watutafune vyema.
Inawezekana tayari hata Jina la muungano huo lipo tayari, linasubiri tu kutangazwa rasmi.

Nisichokielewa vizuri kwa sasa ni chama gani kitakuwa mpinzani wa muungano huo wa walaji. Nikitazama huko ndani ya CCM, hata yale masalia ya Magufuli, hakuna mwenye ubavu wa kutotaka kuwepo mezani kutafuna mali za waTanzania.
Kwa hiyo ni vigumu sana kutegemea upinzani unaoongozwa na genge hilo.
 
Wengi wamekuwa wakisema humu ndani kwamba kwenye maridhiano unapata baadhi, na kupoteza baadhi, kwa hali ya mambo ilivyo naona kama Chadema ndio wamepoteza vikubwa zaidi.

Zile kelele za Katiba Mpya toka kwao siku hizi siziskii tena, kama ambavyo imekuwa kwa CCM wenyewe, hili siamini kama linatokea bahati mbaya, kuna namna...

Nimekuja kuona panatakiwa kufanyika mabadiliko ya uongozi Chadema kabla ya 2024, ili wajiandae kwa serikali za mitaa, na uchaguzi mkuu wa 2025.

Mbowe alishasema atajiuzulu this year, bahati mbaya naona kimya kimetawala, kuna wakati nahisi kama anamsindikiza Samia kuelekea 2025, hasa kwa kutazama mwendelezo wa matukio yanayotokea chamani kwao.

Kuhusu Chadema kujisalimisha kwa CCM 100% tukifika 2025 haitakuwa rahisi, naona watakachofanya wataokoteza ajenda nyepesi nyepesi waende nazo 2025 ili kumlinda Samia, kama ambavyo wameshafanya kwa uchambuzi wa nusu ripoti ya CAG.
 
Mmeongeza na biswalo sasa. Mnateseka sana kmmmk dah. Sahizi uzushi wa trillion moja mmeona hautoshi muongeze na wa Biswalo
 
Ishu ni raia kugoma kulipa kodi wazi wazi na kuanzisha mgomo kabisa hadi serikali itapochukua hatua. Kama haichukui hatua kuwajibisha hao wezi basi TRA wasisumbue watu.
 
Raisi amesema zimefunguliwa akaunti huko Uchina au ulikuwa umelala?
Hakuna hela ilioko china. Hela zao walizoiba wao na mwigulu ndio wamezipeleka China halafu wanataka kusingizia ni za Magufuli... Bi Tozo asitafute cheap popularity
 
Mzee anawaacha vizuri vijana wake. Watoto wa Omary Ali Juma hadi kesho wanalipwa mpunga mrefu kila mwaka. Around $2M kila mwaka toka serikali ya wakaburu sababu kuna jambo baba yao alilifanya kwa mzee Mandela.
 
Niliwahi kusema madehu sio mzalendo hata kdg!
Mtu kuvaa skafu na tai za bendera ya Taifa sio dalili za uzalendo hata mara moja!
Kwanza ni mtu aliyejaa kiburi na dharau nyingi sana!
Ile mikataba ya single source aliyowapa wachina ilijaa ufisadi mkubwa sana na hili litakuja kujulikana hadharani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…