Wakati Bangala yupo Yanga alikuwa kwenye schedule ya benchi inayofanana sawa na hii anayowekwa saizi Mkude?
Bangala ilikuwa ni nadra kumkosa kwenye 1st eleven na ndio maana alipewa hadi ukapteni msaidizi.
Sasa replacement ya namna gani hiyo ambayo kuziba gape la Bangala ni kukaa benchi karibia mechi zote za muhimu?
Mshahara sio factor ya msingi hususan ukizingatia kwa wachezaji wazawa.
Skudu anaweza kuwa analipwa mshahara mrefu kuliko hata Backa, lakini tunapokuja kwenye kipimo cha nani ambaye anaisaidia timu kupitia uwezo wake hapo ndio tunapomuengua Skudu..
Okrah aliyetoka Simba ndio yule yule aliyerudi Yanga. Vile vigoli alivyokuwa akifunga huko kwao Ghana viliwadatisha bila kupima intensity ya ligi yao kufananisha na yetu.
Ni sawa na ukachukue mchezaji ligi ya Sudan Kusini kwa kina Zalan, ukamleta bongo eti kisa huko kwao alikuwa ni top score.